Mama mkwe nakupenda sana ila bora uende

Mama mkwe nakupenda sana ila bora uende

Mana kwa sisi waislamu tunaamini pepo yetu ipo chini ya nyayo za mama zetu kwa hiyo mama ni mtu muhimu kuliko kiumbe chochote
So wake zetu mara nyingi wanataka kupimana ubavu na mama zetu huwa wanaishia kupata talaka la muhimu ni kuwa mvumilivu tuuuuuuu
So hata kama anakufanya umkosee huyo anayekupa hiyo pepo then ni sawa tu!!!
 
Haya maneno umeyaandika tu humu JF au umeshamwambia na kumshirikisha mumeo?
 
Mvumilie tu. . Atajiona mjinga, ukitaka kushindana nae atafanya ndoa yako chungu
 
Hahahahaha lol! Huu msemo wa tuanzie hapo nimetokea kuupenda sana. Hizo ndiyo changamoto za JF, humu kuna watu niliwahi kudhani ni njemba kisha nikadhani ni bi dada halafu nikapata uhakika kwamba ni njemba🙂🙂🙂 na vice versa lol! Kuna mwingine juzi alitaka kutongoza jamaa akamwambia we tongoza tu lakini angalia usije kuliwa wewe lol!
Imebidi nimuulize mana ushauri anao mshauri mtoa uzi haujengi bali unabomoa.
 
Mana kwa sisi waislamu tunaamini pepo yetu ipo chini ya nyayo za mama zetu kwa hiyo mama ni mtu muhimu kuliko kiumbe chochote
So wake zetu mara nyingi wanataka kupimana ubavu na mama zetu huwa wanaishia kupata talaka la muhimu ni kuwa mvumilivu tuuuuuuu
Sina haja ya kupimana ubavu na mtu mwenye taswira ya kuijenga nyumba yangu lakini yule aliyeazimia kuibimoa lazima nimkemee maana ukicheka na nyani utavuna mabua
Tangu tulipofanikiwa kutoka kupanga chumba kimoja mpaka tukaja kupanga vyumba viwili na sebure ndipo nilipoanza kuishi na shemeji yangu mdogo wake anayemfuata na baadae akaniletea mwingine wote hawa nimewalea kama ndugu zangu,na mpaka hii Leo mmoja anatafuta kazi mwingine chuo,sio kwamba tulikua hatupishani tulipishana bila heshima ilikuwepo na lazima tufahamu kua heshima ni kitu cha bure hata kama labda namkosea huyu mama sio wa kuniingilia maamuzi ya nyumba yangu,sio wa yeye kuutumia karibu muda wangu wote kukaa chumbani kwake kuongea na mwanae,mchana Mimi nakua nipo kazini bora basi wangetumia muda huo lakini kwa makusudi tu jioni ndio wanaitana mazungumzo yasiyokwisha
 
Mbona simple tuu.? Kwa mujibu wako Mzozo ni chakula kuchelewa kupikwa na umesema mama mkwe kumzungumzia mkemwenzio huna shida nalo.kwani mchana anapika nani.? Si house girl.? Usipopika wewe mmeo hashibi.? Wewe huyo umemkuta ukubwani, huyo mkweo kakaa naye toka anazaliwa. So simply ukiamua kuingia vita na mama mkwe hutoshinda kamwe.

Kwani Kuna ubaya gani ukitoa idhini katika kipindi kwa housegirl apike chakula.? Hususan kipindi hiki ambacho mkweo yupo.? Weekend ukiwepo ama siku ukiwahi kurudi utapika. Sometimes inabidi ubadilike ili kuendana na mazingira, na ukifanya hivyo kama mumeo ni muelewa ataelewa umemaanisha nini.
 
Hapo mnapoishi ni kwako au kwa mumeo?
Uliza maswali ya kuumiza kichwa,sio vijiko na sahani ni vya mumeo au wewe, ili swali ni la kijinga sana,kama nyumba ni ya mume wake ndiyo inatoa kibali anyanyaswe??
 
Mbona simple tuu.? Kwa mujibu wako Mzozo ni chakula kuchelewa kupikwa na umesema mama mkwe kumzungumzia mkemwenzio huna shida nalo.kwani mchana anapika nani.? Si house girl.? Usipopika wewe mmeo hashibi.? Wewe huyo umemkuta ukubwani, huyo mkweo kakaa naye toka anazaliwa. So simply ukiamua kuingia vita na mama mkwe hutoshinda kamwe.

Kwani Kuna ubaya gani ukitoa idhini katika kipindi kwa housegirl apike chakula.? Hususan kipindi hiki ambacho mkweo yupo.? Weekend ukiwepo ama siku ukiwahi kurudi utapika. Sometimes inabidi ubadilike ili kuendana na mazingira, na ukifanya hivyo kama mumeo ni muelewa ataelewa umemaanisha nini.
Hivi mama zenu majumbani kwao chakula cha usiku huwa wana kula saa ngapi? Maana Mimi hapa wakati taarifa ya habari ya saa 2 inaendelea chakula huwa tayari kwa kuliwa,hakuna siku niliyorudi saa 4 usiku, nipo radhi kugombana na boss wangu lakin niwahi kurudi maana na Mimi nina watoto wadogo wanahitaji kula mapema walale mapema na zaidi ya yote msichana wangu wa kazi ni kama ndugu yangu japo anatoka kijijini kwao lakini majukumu aliyo nayo ni mengi sana maana pamoja na kazi zote ananisaidia kulea mtoto wangu huyu mdogo wa mwisho hivyo nae bila shaka anahitaji mapumziko ya jiko angalau Mara moja kwa siku
 
Mana kwa sisi waislamu tunaamini pepo yetu ipo chini ya nyayo za mama zetu kwa hiyo mama ni mtu muhimu kuliko kiumbe chochote
So wake zetu mara nyingi wanataka kupimana ubavu na mama zetu huwa wanaishia kupata talaka la muhimu ni kuwa mvumilivu tuuuuuuu
Wala uislam haulalishi vitendo vya huyu mama,Utamtii mzazi wako ktk mambo ambayo hayaendi kinyume na maamrisho ya Mola Mlezi,Je anachokifanya huyu mama kwa mmkwewe ni haq? Kwa vitendo vya huyu mama ni kama anataka kuisambaratisha ndoa ya mwanawe,Je wajua ktk halal zenye kumchukiza Allah ni yule mwenye kuoa na kuacha? Ktk uislam kuna haq za mume na haq za mke, Kwa mujibu wa mtoa mada haq zake ziko hatarini kwa huu mwenendo wamkwewe. KAMA ALICHOSEMA DADA HUYU NDIO UHALISIA! BASI MKWE NI TATIZO NA JUHUDI ZA HARAKA ZICHUKULIWE KABLA HALI HAIJAWA TETE
 
And it hurts alot pale ambapo unakuta na mwanae ni mtu mzima aliegoma kukua!!
Aisee, mtu mzima aliyegoma kukua? Pale utakapotaka mama afurahi, mke/mume afurahi ili kulinda furaha ya nyumba yako, ndio utajua hakuna aliyekomaa katika ndoa. Wakati mwingine tuwaulize waliopiga 50+yrs kwenye ndoa, they might add value to our way of thinking.
 
Back
Top Bottom