Mama mkwe anataka nimuuzie samani za ndani

Mama mkwe anataka nimuuzie samani za ndani

Mwenzako amekuambia akiuza hivyo vitu ndio atapata pesa ya kwenda kuanzia maisha huko aendako, amesema usawa sio mzuri, kwa uwazi kabisa na hata mke wake analijua hilo ndio maana amegoma mama yake asiuziwe sasa wewe unamtumbika shimoni, jamani Mamndenyi , au kwa vile mwanamke mwenzako?
Kwani kilichompeleka hadi kumwambia mama mkwe kuwa anauza samani ni nini?
Ampe tu, si unajuwa tena mama akinung'unika unaweza kuzaa watoto taahira?
Amalize kama alivyoaanza, hamna namna.
 
Ingekuwa mimi ningemwachia wife amalizane na mama, anaonekana kuwa na busara. After all hizo ni sehemu ya assets zenu, naamini mnauza ili huko mnakoenda mnunue vingine.
 
Mwanamke siku zote anakupima.
Anaweza kukupa ushauri ambao utaleta lasaña huko mbele.
Wewe amua tu kumpa hivyo vitu bure.
Kosa ulilofanya ni kumwambia unauza.
Ulitakiwa umwambie naondoka navyo.
 
Ameongea kikubwa tu hapo hakuna biashara kifupi mama mkwe anataka umpe bure kabisa.

Ni uamuzi mgumu ulio mbele yako ila amua kwa busara.
 
yaani unakula papuchi ya mwanae then umuuzie,mpe hata kimoja bure
 
Kwani kilichompeleka hadi kumwambia mama mkwe kuwa anauza samani ni nini?
Ampe tu, si unajuwa tena mama akinung'unika unaweza kuzaa watoto taahira?
Amalize kama alivyoaanza, hamna namna.

Amesema alienda kwa ajili ya kuaga, akaulizwa utaondoka na mizigo yako yote? Naye akajibu akisema nitauza baadhi ya mizingo yangu, ndio baadaye sasa Mama mke akaomba auziwe.

Kumpatia mama mkwe vitu sio shida, lakini jamaa anasema khari kwa sasa sio nzuri, hayo ya kwamba akinung'unika utazaa tahira ni kama jambo hilo utakuwa umemfanyia makusudi, otherwise hakuna laana wala nini.
 
Habari Wapendwa

Mimi na familia yangu tunahamia mkoa mwingine..Nilipoenda kutoa taarifa za hizi pilika pilika za kuhama kwa wakwe, Mama mkwe akaniuliza juu ya vitu vyangu vya ndani..Nikamwambia vingi nitaviuza...Nitaondoka tu na vitu vidogo vidogo..

Juzi kanipigia simu akaniambia anaomba nimuuzie baadhi ya vitu..Sikumpa jibu la moja kwa moja nikamyumbisha kidogo then nikamwambia ntakutafuta tuongee..Nimemshirikisha wife akaniambia tuviuze kwa mtu mwingine Kwa madai kuwa mama yake Ataleta longolongo tu na kujuana kwingi..

Wakuu embu niongezeeni busara juu ya hili,Nahisi zangu hazitoshi...Nifanyaje??
Kando ya hizo longolongo zake,Kumuuzia Mama mkwe hivi vitu ni sawa.???
Ningeweza kumpa bure sema hii pesa nahiitaji sana iweze kutubusti huko tunakoenda.. vile hali ya maisha ni tight kwa sasa
ushauri wa mkeo ni mzuri Hata ningekuwa mimi ningekushauri hivyo.

mwambie mama mkwe kuwa vitu vilishwa wekewa booking kabla yake.
 
Ushauri wangu kwako Kaboom, mpe mama hivyo vitu. Maisha hayataishia hapo na utapata vingine.

Ndoa ni zaidi ya vitu.

Mkeo anakupima tu lakini angependa sana umpe mama yake hivyo vitu. Wala usimuuzie. Utapata thawabu.

Pamoja na kubana kwa maisha, ndani ya moyo wako assume unaanza upya.

Mungu na akubariki sana
sidhani kama umemuelewa, ni kwamba angeweza kumpa tatizo ni kwamba ana uhitaji na pesa.
 
Ningekuwa mimi ningetangulia aafu vyombo namuachia wife.
Mama mkwe namwambia nimemwachia mwanao uongee naye.
Akimpa mama yake au akiuza atajua mwenyewe.
 
Anataka kubakia na kitanda, godoro, shuka, mto na taulo mlivyotumia na mwanaye?
 
makabila mengine mna tamaduni ngumu sana..

kikwetu mama mkwe hawezi ongea na mume wa mtoto wake kiasi cha kuuziana vitu
 
Weka hivyo vitu kwenye matangazo kule tununue.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom