Mama mkwe anataka nimuuzie samani za ndani

Kaboom

JF-Expert Member
Nov 6, 2011
10,828
14,996
Habari Wapendwa

Mimi na familia yangu tunahamia mkoa mwingine..Nilipoenda kutoa taarifa za hizi pilika pilika za kuhama kwa wakwe, Mama mkwe akaniuliza juu ya vitu vyangu vya ndani..Nikamwambia vingi nitaviuza...Nitaondoka tu na vitu vidogo vidogo..

Juzi kanipigia simu akaniambia anaomba nimuuzie baadhi ya vitu..Sikumpa jibu la moja kwa moja nikamyumbisha kidogo then nikamwambia ntakutafuta tuongee..Nimemshirikisha wife akaniambia tuviuze kwa mtu mwingine Kwa madai kuwa mama yake Ataleta longolongo tu na kujuana kwingi..

Wakuu embu niongezeeni busara juu ya hili,Nahisi zangu hazitoshi...Nifanyaje??
Kando ya hizo longolongo zake,Kumuuzia Mama mkwe hivi vitu ni sawa.???
Ningeweza kumpa bure sema hii pesa nahiitaji sana iweze kutubusti huko tunakoenda.. vile hali ya maisha ni tight kwa sasa
 
Kuna short term and long term relationship. Mkwe wako ataendelea kuwa mkweo tu. Mpe hivyo anavyovitaka kama akikupa fedha sawa asipokupa potezea.

Narudia mkweo ni mkweo tu bora usingekuwa umemwambia kabla utajenga chuki isiyoisha na siku ukienda kwake kwa ushauri hutopata la maana.

Mimi ningempa kwa kumuuzia ila asipolipa sitomdai pia
 
Ushauri wangu kwako Kaboom, mpe mama hivyo vitu. Maisha hayataishia hapo na utapata vingine.

Ndoa ni zaidi ya vitu.

Mkeo anakupima tu lakini angependa sana umpe mama yake hivyo vitu. Wala usimuuzie. Utapata thawabu.

Pamoja na kubana kwa maisha, ndani ya moyo wako assume unaanza upya.

Mungu na akubariki sana
 
Mwambie umeahirisha kuviuza na utahama navyo..ukishindwa vipeleke mwambie huviuzi tena ila unaviwekesha kwake basi.kama kakuchokonoa na wewe mchokonoe
 
Mama mkwe anavitamani hivyo vitu na anajua huwezi kumdai pesa. Kama uchumi uko vizuri mwachie, mwisho wa siku watoto wako wakienda kwa bibi yao watavitumia.
Mkuu kinachonitatiza ni kuwa baadhi ya vitu anavyovitaka anavyo
 
Mwambie: Mama mie kwa sasa nimekosa muda wa kuongea na wewe lile suala la kukuuzia vyombo, ila naomba uwasiliane na mama.... kwa ajili ya kuliweka sawa
Mtupie mpira mwanae ndie aongee na mamaye
 
mpe mama akikuuliza bei mwambie halafu potezea .. huu ni mtego unahitaji uwe na busara na hekima ya hali a juu la sivyo badae italeta shida
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom