jovetha
Member
- Apr 16, 2016
- 40
- 18
Naombeni msaada wa mawazo maana nahisi nitakufa kwa mawazo ila ninajikaza. Mimi ni mama wa miaka 30 Nina mtoto mmoja, nina ndoa ya kimila. Nampenda sana mme wangu lakini tumekuwa hatuna maelewano mazuri mimi na yeye kwa sababu ni mtu wakusikiliza ndugu na pia ni mtu ambaye anaona mawazo ya ndugu zake ndio mawazo sahihi especially his mum, mpaka ikafika hatua ya yeye kuhama nyumbani na kwenda kuishi kwa wazazi wake ambao hawako mbali na tunapoishi yapata mwaka sasa tangu aondoke vikao vya kifamilia tumeshakaa lakini hakuna suluhu mpaka Sasa ambayo imefanikiwa.
Sasa hapa ninapoishi tuna nyumba mbili, nyumba Moja ni mpya bado hatujahamia hivyo tumeifanya kama store pia tulikuwa tumeshaweka na vitu vingine kama makabati ili tuweze kuhamia, kutokana na migogoro yetu mpaka sasa hatujahamia.
Hivi karibini nilipoteza ufunguo wa hiyo nyumba mpya hivyo ikanibidi nimuite Fundi ili aweke kitasa kipya ili niweze kufanyia nyumba usafi maana hapa tunapoishi Kuna mchwa wengi hivyo nilazima kufanya usafi vitu visiharibiwe na mchwa. Baada ya kubadilisha kitasa nikamwambie dada apafanyie usafi, wakati dada akiendelea na usafi,
Mara shemeji akaja amkamfukuza yule mdada na kuchukua zile funguo za nyumba na baadae mama mkwe alifika nyumbani na rafiki yake akinigombeza kwanini nimevunja mlango wa nyumba, nikamwambia sijavinja nimebadikisha kitasa, akaniambia kwanini nabadilisha kitasa cha nyumba bila kumpa taarifa, nikamwambie, nyumba si yangu na mme wangu ndio maana sijawapa taarifa kama nimebadilisha kitasa na baada kama ya siku 10 kupita nikapigiwa simu nahitajika kituo cha police kufika pale nikaambiwa nimeshitakiwa na mama mkwe kwa uharibifu wa Mali na kesi ikapelekwa mahamani mind you kwenye kiwanja tulichojenga tulipewa na baba mkwe.
Naombeni msaada wa kisheria juu ya hii case