Mama mkwe anataka nimuuzie samani za ndani

Mama mkwe anataka nimuuzie samani za ndani

Hii ngumu kweli kweli, kuwauzia wengine vyote mama mkwe ataona kama vile umemzalau. Mpe binti yake (Mkeo) jukumu la kumuelimisha mama yake na hata jukumu la kuviuza pia, wewe ukiwa unachungulia kwa mbali.

Na mwisho mwambie ni mwiko kwenu kumuuzia Mama ama Baba mkwe kitu chochote. Usingekuwa na shida ya pesa hiyo ningekushauri umpe tu vitu anavyotaka, lakini kama usawa wenyewe ndio huo, ndg komaa uuze upate pa kuanzia huko uendako kwenye mkoa mwingine
 
Mpe tu hivyo vitu
wamama wengi hela imeishia kusomesha
hata ndani hawana vitu vya thamani;

Mpe tu;

Mwenzako amekuambia akiuza hivyo vitu ndio atapata pesa ya kwenda kuanzia maisha huko aendako, amesema usawa sio mzuri, kwa uwazi kabisa na hata mke wake analijua hilo ndio maana amegoma mama yake asiuziwe sasa wewe unamtumbika shimoni, jamani Mamndenyi , au kwa vile mwanamke mwenzako?
 
Ww uza baadhi ya vitu na
Hvo vingne mpe bure
Na,c kumuuzia maana ukimuuzia mtaishia

kusumbuana tu cha
Msingi mpe tu bure ameshakua mama mkwe
Mzaz hua hauzwi vitu na
Mwanae
 
Bro, mi nitakuwa interested na duka lako la vizibo kama nalo linauzwa. Kuhusu mama mkwe, mwambie kama hana hela mkononi ajibebe; you already took their daughter off their hands, when will it end(no more favors)?
 
Kama ingekuwa mimi ningetumia busara tu namwachia mama mkwe anavyovihitaji namwambia na bei vingine nauza. Plan sometimes hubadilika .

Asiponipa pesa sawa
Nikikwama niendako utanipiga tafu?
 
Vitu gan hivyo mkuu. Weka bei mezani mateja tupo hapa
 
Huyo mama anataka bure, tatizo sio kumpa bure tatizo naww unataka uviuze upate hela. Usawa mgumu huu kaka usimwonee haya mwambie nshauza mama kama mbwai mbai tu.
 
Hapo akili kichwani tafuta gari zuri wapeleke vitu vyako taratibu mpaka vifike kila kilicho ndani kinahitajika na ukifika uko lzm utakiitaji na utajikuta unakinunua ghali mara mbili au zaidi ya ulichouza
 
Kama ingekuwa mimi ningetumia busara tu namwachia mama mkwe anavyovihitaji namwambia na bei vingine nauza. Plan sometimes hubadilika .

Asiponipa pesa sawa
Tatizo sio kumwachia mkwewe vitu hivo

Issue ni kwamba wanauza baadhi ili hiyo hela iwasaidie huko waendako. Afu kumbuka usawa huu unavobana ati
 
Habari Wapendwa

Mimi na familia yangu tunahamia mkoa mwingine..Nilipoenda kutoa taarifa za hizi pilika pilika za kuhama kwa wakwe, Mama mkwe akaniuliza juu ya vitu vyangu vya ndani..Nikamwambia vingi nitaviuza...Nitaondoka tu na vitu vidogo vidogo..

Juzi kanipigia simu akaniambia anaomba nimuuzie baadhi ya vitu..Sikumpa jibu la moja kwa moja nikamyumbisha kidogo then nikamwambia ntakutafuta tuongee..Nimemshirikisha wife akaniambia tuviuze kwa mtu mwingine Kwa madai kuwa mama yake Ataleta longolongo tu na kujuana kwingi..

Wakuu embu niongezeeni busara juu ya hili,Nahisi zangu hazitoshi...Nifanyaje??
Kando ya hizo longolongo zake,Kumuuzia Mama mkwe hivi vitu ni sawa.???
Ningeweza kumpa bure sema hii pesa nahiitaji sana iweze kutubusti huko tunakoenda.. vile hali ya maisha ni tight kwa sasa
Hapo soma alama za nyakati. Unachoweza kumpa, apewe bure free of charge. Ndiyo maana sisi wengine hatumalizi kulipa mahari. Hiyo itakuwa sehemu ya mahari !
 
Kama binti yake amesema usimuuzie bas usimuuzie kwel, Hakuna kaz ngumu kama kumdai mzazi esppecialy akiwa mkweo.
Mwambie tu nmeshapata mteja mwengne amenunua na pia kama kuna kitu unaweza kumpa mpe bure tu.
Naomba unisaidie kumfikishia ujumbe huyu mwathirika..

Kosa kubwa kuliko yote ni kumuuzia mama mkwe samani zake...

Kitanda anachomgegedea mwanae pia atamuuzia??

Na kwanini mtu anaenda kuripoti kwa wakwe jambo analotaka kulifanya???
 
Tatizo sio kumwachia mkwewe vitu hivo

Issue ni kwamba wanauza baadhi ili hiyo hela iwasaidie huko waendako. Afu kumbuka usawa huu unavobana ati
Sasa chukulia wanamnyima mkwe hata mwiko baadae anasikia wametafuta dalali atafute mteja. Je atamchukuliaje Kaboom!
Watoto wakiwa kwa bibi watavitumia tu.
 
Naomba unisaidie kumfikishia ujumbe huyu mwathirika..

Kosa kubwa kuliko yote ni kumuuzia mama mkwe samani zake...

Kitanda anachomgegedea mwanae pia atamuuzia??

Na kwanini mtu anaenda kuripoti kwa wakwe jambo analotaka kulifanya???
Ha ha aha haya ndio mammbo mkwe analala usiku anaota gegedo la mkwewe tu kila siku, Sijajua mahusiano yao yakoje labda kwasababu anahama mkoa so ni kama kumuaga ila hili ni mawazo yangu.
Naamin mkewe angemfikishia mama yake ujumbe wa kuhama kuliko alivyoenda yeye mwenyewe
 
Ha ha aha haya ndio mammbo mkwe analala usiku anaota gegedo la mkwewe tu kila siku, Sijajua mahusiano yao yakoje labda kwasababu anahama mkoa so ni kama kumuaga ila hili ni mawazo yangu.
Naamin mkewe angemfikishia mama yake ujumbe wa kuhama kuliko alivyoenda yeye mwenyewe
Exactly!!!!
 
Ushauri wangu kwako Kaboom, mpe mama hivyo vitu. Maisha hayataishia hapo na utapata vingine.

Ndoa ni zaidi ya vitu.

Mkeo anakupima tu lakini angependa sana umpe mama yake hivyo vitu. Wala usimuuzie. Utapata thawabu.

Pamoja na kubana kwa maisha, ndani ya moyo wako assume unaanza upya.

Mungu na akubariki sana
Issue sio kupta vitu vingine tatizo anashida na pesa ambayo itakidh mahitaji aliyonao kwa muda huu.tukiwa na mawazo finyu tutabak kulia tu tuendako!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom