Malumbano ya Hoja ITV: Kama wanaochangia ndiyo wanavyuo wetu acheni tu DP World wainunue hata Tanzania yote!

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,694
109,133
95% ya wasomi wa sasa hivi wa hasa kuanzia mwaka 2010 mpaka mwaka jana 2022 kichwani hamna kitu, hawajiamini na ujengaji wao wa hoja si tu ni mbovu bali ni wa kimasikini mno kifikra.

Kwa huu uchangiaji wa hawa wasomi (wana vyuo wetu) na wengi wakitokea UDSM ninaouona sasa (mubashara) ITV daima natamani hawa DP World wasiishie tu kuzichukua Bandari zetu zote, Maziwa na Mito yetu pamoja na Vijito hadi Mabwawa yote kama wakitaka, bali watununue na hata sisi Watanzania na Taifa letu la Tanzania liwe lao.

Vyuo Vikuu vya sasa (ukikiondoa tu Chuo Kikuu kilichobarikiwa na Mungu cha SAUT Mwanza) havizalishi Rational and Critical Thinkers bali vinazalisha sana walalamikaji, wakurupukaji na wapenda mihemko katika Mijadala yenye kuhitaji Akili Kubwa kuijadili.
 
Lakini kuongea mbele za watu ni sanaa, mtoa mada ,haitaji elimu ya udsm kuwa MTU mzungumzaji.kuna wengine sio watu wa kuongea licha ya kwamba ni wasomi lakini kiutendaji ni moto wakuotea mbali
How can you be an Intellectual and you feel shy / uncomfortable to speak before the audience? That tantamounts you to Academic Bogus.
 
95% ya Wasomi wa sasa hivi wa hasa kuanzia mwaka 2010 mpaka mwaka jana 2022 Kichwani hamna Kitu, hawajiamini na ujengaji wao wa Hoja si tu ni mbovu bali ni wa Kimasikini mno Kifikra.

Kwa huu Uchangiaji wa hawa Wasomi ( wana Vyuo Wetu ) na wengi wakitokea UDSM ninaouona sasa ( mubashara ) ITV Daima natamani hawa DP World wasiishie tu Kuzichukua Bandari zetu zote, Maziwa na Mito yetu pamoja na Vijito hadi Mabwawa yote kama wakitaka bali watununue na hata Sisi Watanzania na Taifa letu la Tanzania liwe lao.

Vyuo Vikuu vya sasa ( ukikiondoa tu Chuo Kikuu kilichobarikiwa na Mungu cha SAUT Mwanza ) havizalishi Rational and Critical Thinkers Bali vibazalisha sana Walalamikaji, Wakurupukaji na Wapenda mihemko katika Mijadala yenye kuhitaji Akili Kubwa kuijadili.
Lawama ziende kwa wanachuo au wahadhiri?
 
Lakini kuongea mbele za watu ni sanaa, mtoa mada ,haitaji elimu ya udsm kuwa MTU mzungumzaji.kuna wengine sio watu wa kuongea licha ya kwamba ni wasomi lakini kiutendaji ni moto wakuotea mbali
Huwezi kujua unachokizungumza halafu ukawa na baridi au aibu au kigugumizi kukizungumza. Unatia mashaka.

Kuna mwaka tulifukuzwa kwa muda kama wa miezi 6/7 wengi tukajua ndio imeisha safari ya elimu ya juu.. kwa kosa la kugoma, kipindi cha Hayati Mzee Mkapa.

Waliosalia walikuwa first year, lengo la serikali lilikuwa ni kuzalisha kizazi kitakachoogopa mamlaka, si kuheshimu, ili vyuo vipoe na vitawalike.

Imefanya kazi kwa zaidi ya miaka 12 hakujawa na migomo katika vyuo vikuu, hii haimaanishi Hali ni nzuri sana, ila serikali imefanikiwa kutengeneza kizazi Cha wasomi wenye inbuilt hofu ya mamlaka na wenye mamlaka.

Tatizo ni kuwa na wasomi wasiojiamini, wavivu wa kwenda extra mile.. as a result persistence na that urge to defy the status quo for the pursuit of knowledge and excellence inakufa among wasomi, wengi sio wanaishia kuheshimu mamlaka tuu, ila wanaishia kuheshimu notice za mwalimu tuu.. now that's deadly
 
Totally malumbano ya hoja yenyewe inapokea wachangiaji wa ajabuajabu siku hizi. Wamepotelea wapi wale wachangiaji wa miaka ile ya nyuma? Hawa wa siku hizi ni vilaza watupu, mbaya zaidi wanajitambulisha ni wasomi wa vyuo, aibu tupu kwa jinsi wasivyojua kujenga hoja maridhawa
 
The wealth of a country comes from the minds of its people
 

Attachments

  • Ehno2NgWsAA8X9J.jpeg
    Ehno2NgWsAA8X9J.jpeg
    36.1 KB · Views: 4
Back
Top Bottom