Mbali na kuwa DP World hawajaanza rasmi kazi ya Bandari nchini, ajabu wamefanikiwa kutugawa kidini

Nsanzagee

JF-Expert Member
Jun 28, 2023
1,939
4,122
Hivi naotaa ama ni ukweli dhahiri?

Kwamba: badala ya hoja zetu kujikita kwenye utatuzi wa vipengele tata vya mkataba wa Dp world na hatimaye tufikie hatima njema kama taifa na kutuacha kwenye umoja wetu.

Sasa watu maarufu kabisa, wasomi na viongozi wakuu wa dini na serikali wanaacha kwa maksudi kujikta kwenye hoja na badala yake wanazunguza udini kwenye jambo la kitaifa!!?

Huku ni kupungukiwa hekima na kujiona mwenye haki kuliko wengine! Tukumbuke, Sisi sote ni watanzania, na siyo kwamba tulijileta hapa, hapana, tumezaliwa hapa na tukawa watanzania!

Tunafanya hivi kwa sababu ya kifilisika hoja? Ama nini? Au mtu mzima hovyo? Unapandikiza udini ili upate nini? Hovyo kabisa.

Chanzo cha mpaka tunafika hapa nini?, ni kwamba tokea kitambo kama Nchi tumekuwa hatumpendi Rais wetu?? na je, kumewahi kujitokeza chuki dhidi yake huko nyuma na kwenye mihadhara ya kidini kumewahi kusemwa kwamba mh Rais hatakiwi?? Sina hakika na hili halijawahi tokea!

Chanzo ni nini? Chanzo ni Mkataba wa DP? Kwa nini isiwe sisi na mkataba wa DPWORD?

Kwa nini chanzo cha hili hatutaki kukumbuka tena na badala yake tunajadili udini?

Je? Mkataba wa DPWORD umekuja na nini? Umekuja kutugawa? Umekuja kuleta hamaki katika nchi yetu? Kuna nini nyuma yake?

Na watu wanaojadili udini badala ya kile kimesababisha, tunaajenda gani nyuma ya udini huu usio na faida katika hili la mkataba na hatima ya nchi yetu!

Kwa nini tuko hapa sasa, kwamba tunabiongozi wa dini wao kwao kila ajenda juu ya nchi wanaitazama kidini?? Ni kukosa upeo wa mambo yasiyo na kidini na kidini?

Si kila mahali ibada na udini zinatakiwa, kuna mambo ya kitaalam, yafanywe wataalamu, mambo ya kisiasa, yafanywe na wanasiasa, mambo ya kijamii, yafanywe na wanajamii, na mambo ya kidini, vilevile yaende kidini!

Suala la Nani yupo kwenye kiti cha uraisi, huyu huwajibika kwa watu wote na kwa dini zote, na pia naye bado ni mtanzania ingawa ana dini yake.

Hapa labda niseme, ni makosa makubwa kwa wanadini, kiongozi wa nchi inapotokea amekosea kama ilivyo kawaida ya binadamu, ikitokea jamii inalalamika kumhusu, na kwa kuwa tu ana jina linalotokana na dini fulani, basi hao wa dini yake wanaanza kunung'unika wakiwa na sababu za dini yake! Hii siyo hekima, mambo haya huleta mgawanyiko sana kwenye nchi.

Tukumbuke, Kuna haya mabaraza ya wana dini, huwa yanatoa waraka waje pindi Rais anapokosea, nauliza, Kuna Rais amewahi kusalimika kwa kupewa waraka kutokea kwenye mabaraza ya dini hizi?

Kama ni hapana, Tuanzeni kuwaona viongozi wetu wa Kiserikali kwamba, wanapokuwa kwenye uongozi, hawabebi dini zetu bali wamebeba watanzania wote.

Tuwaombee na kuwatia moyo, inapotokea kuna makosa katika uongozi wao, wakemewe bila kujali dini zao!

Mpaka sasa DPWORD wamefanikiwa kututoa kwenye hoja ya mkataba wao mbovu na badala yake tunalumbana kidini.

Tunaowajibu mkubwa wa kuendelea kujielimisha hasa kuhusu kufahamu ni lipi la kitaifa na lipi la kidini!

La sivyo tutaendelea kubaki kwenye udini udini huu usio na maana kwenye mambo ya kitaalamu yanayohusu jamii nzima ta kitanzania.

Africa na Tanzania, tunachelewa kwa sababu ya udini mwiiingi utadhani watu waishi kwa kula dini!
 
Hivi naotaa ama ni ukweli dhahiri?

Kwamba: badala ya hoja zetu kujikita kwenye utatuzi wa vipengele tata vya mkataba wa Dp world na hatimaye tufikie hatima njema kama taifa na kutuacha kwenye umoja wetu,

Sasa watu maarufu kabisa, wasomi na viongozi wakuu wa dini na serikali wanaacha kwa maksudi kujikta kwenye hoja na badala yake wanazunguza udini kwenye jambo la kitaifa!!?

Huku ni kupungukiwa hekima ama uzalendo wa kulinda mali zetu kama taifa??

Au ni kifilisika kwa hoja? Ama nini?

Chanzo cha mpaka tunafika hapa, ni kwamba tokea kitambo kama Nchi tumekuwa hatumpendi Rais wetu na kumewahi kujitokeza chuki dhidi yake huko nyuma na kwenye mihadhara ya kidini kumewahi kusemwa kwamba mh Rais hatakiwi??

Chanzo ni nini?

Kwa nini chanzo cha hili hatutaki kukumbuka tena na badala yake tunajadili dini?

Je? Mkataba wa DPWORD umekuja na nini? Umekuja kutugawa? Umekuja kuleta hamaki katika nchi yetu? Kuna nini nyuma yake?

Na watu wanaojadili udini badala ya kile kimesababisha, tunaajenda gani nyuma ya udini huu usio na faida katika hili la mkataba na hatima ya nchi yetu!

Kwa nini tuko hapa sasa, kwamba tunabiongozi wa dini wao kwao kila ajenda juu ya nchi wanaitazama kidini?? Ni kukosa upeo wa mambo yasiyo na kidini na kidini?

Si kila mahali ibada na udini zinatakiwa, kuna mambo ya kitaalam, yafanywe wataalamu, mambo ya kisiasa, yafanywe na wanasiasa, mambo ya kijamii, yafanywe na wanajamii, na mambo ya kidini, vilevile yaende kidini!

Suala la Nani yupo kwenye kiti cha uraisi, huyu huwajibika kwa watu wote na kwa dini zote, na pia naye bado ni mtanzania ingawa ana dini yake

Hapa labda niseme, ni makosa makubwa kwa wanadini, kiongozi wa nchi inapotokea amekosea kama ilivyo kawaida ya binadamu, ikitokea jamii inalalamika kumhusu, na kwa kuwa tu ana jina linalotokana na dini fulani, basi hao wa dini yake wanaanza kunung'unika wakiwa na sababu za dini yake! Hii siyo hekima, mambo haya huleta mgawanyiko sana kwenye nchi

Tukumbuke, Kuna haya mabaraza ya wana dini, huwa yanatoa waraka waje pindi Rais anapokosea, nauliza, Kuna Rais amewahi kusalimika kwa kupewa waraka kutokea kwenye mabaraza ya dini hizi?

Kama ni hapana, Tuanzeni kuwaona viongozi wetu wa Kiserikali kwamba, wanapokuwa kwenye uongozi, hawabebi dini zetu bali wamebeba watanzania wote,

Tuwaombee na kuwatia moyo, inapotokea kuna makosa katika uongozi wao, wakemewe bila kujali dini zao!

Mpaka sasa DPWORD wamefanikiwa kututoa kwenye hoja ya mkataba wao mbovu na badala yake tunalumbana kidini

Tunawajibu wa kuendelea kujielimisha ili kuondokana dhana hizi za kidini, hazitatufikisha popote kama nchi
Udini, ukabila na unafiki ni vitu vya kupigwa vita kabisa.
 
Back
Top Bottom