Malizia huu msemo: Ukivuliwa nguo sharti ………….....

Malizia huu msemo: Ukivuliwa nguo sharti ………….....

Nimesikiliza hotuba ya raisi akifungua rasmi bunge la 13 na nimeona ni kama ameanza kuinama na kujisitiri kutokana na yale yaliyotokea.

  1. Je, ili achutame kabisa kiungwana na kuepuka fedheha inabidi afanye nini?

  2. Kwa wenzangu mliosikiliza hotuba: je imewatia moyo au ndiyo imewaongeza hasira?

  3. Gen Z na wote wanaosapoti D9: kuna hoja hata moja imeongelewa ambayo inagusa malalamiko ya maandamano yaliyopita au yale yajayo?

Binafsi kwa niliyoyasikia nimeona ni inawezekana watawala wameona mabavu siyo suluhisho litakalotufikisha mahali pazuri kama taifa. 
Nafikiri haya mambo 5 yameashiria kwamba sauti za watanzania zina nguvu:
  • Kukiri kuhusu mauaji ya siku za uchaguzi na kutoa pole
  • Mchakato wa katiba mpya kurejea ndani ya siku 100 za kwanza
  • Kufuta kesi za uhaini kwa vijana
  • Tume ya kuchunguza mauaji ya Oktoba 29 na maridhiano (japo bado kna maswali:akina nani wapo hiyo tume na wamepatikanej)
  • Kuanzisha wizara maalum ya vijana na ajira mpya sekta za elimu na afya

Mambo mengine niliyoyasikia ni blah blah za kila mwanasiasa - Mikopo, uboreshaji miundombinu , kilimo, utalii, uwezeshaji madini, kuinua uchumi, tehama, mwendokasi, reli, madaraja mapya etc.

Kilichonishangaza: ni wabunge kupiga makofi mengi pale raisi aliposema anywe maji kidogo 😂😂
Inasikitisha sana. Rais haramu......
 
Kumbe kuna hotuba🙆‍♂️🙆‍♂️🙆‍♂️🤣🤣🤣🤣
Afu wewe 😂
giphy 2.GIF
 
Japo Amelia sana, ameonesha huzuni na majuto makuu, ila D9 iko pale pale.

Wala asituletee unafiki wake hapa, watu tumepoteza wapendwa wetu, vipi ataweza warudisha wawe hai km zamani?

Jamani waja tusihadaikee, tuanzie tulipoishia.
 
Nimesikiliza hotuba ya raisi akifungua rasmi bunge la 13 na nimeona ni kama ameanza kuinama na kujisitiri kutokana na yale yaliyotokea.

  1. Je, ili achutame kabisa kiungwana na kuepuka fedheha inabidi afanye nini?

  2. Kwa wenzangu mliosikiliza hotuba: je imewatia moyo au ndiyo imewaongeza hasira?

  3. Gen Z na wote wanaosapoti D9: kuna hoja hata moja imeongelewa ambayo inagusa malalamiko ya maandamano yaliyopita au yale yajayo?

Binafsi kwa niliyoyasikia nimeona ni inawezekana watawala wameona mabavu siyo suluhisho litakalotufikisha mahali pazuri kama taifa. 
Nafikiri haya mambo 5 yameashiria kwamba sauti za watanzania zina nguvu:
  • Kukiri kuhusu mauaji ya siku za uchaguzi na kutoa pole
  • Mchakato wa katiba mpya kurejea ndani ya siku 100 za kwanza
  • Kufuta kesi za uhaini kwa vijana
  • Tume ya kuchunguza mauaji ya Oktoba 29 na maridhiano (japo bado kna maswali:akina nani wapo hiyo tume na wamepatikanej)
  • Kuanzisha wizara maalum ya vijana na ajira mpya sekta za elimu na afya

Mambo mengine niliyoyasikia ni blah blah za kila mwanasiasa - Mikopo, uboreshaji miundombinu , kilimo, utalii, uwezeshaji madini, kuinua uchumi, tehama, mwendokasi, reli, madaraja mapya etc.

Kilichonishangaza: ni wabunge kupiga makofi mengi pale raisi aliposema anywe maji kidogo 😂😂
1000265298.jpg
 
Rais ni Haramu sasa sijui unamwongelea Rais yupi hapo, lkn pia hukumu ya muuaji ni kunyongwa mpaka kufa na hii ni kwa munibu wa Sheria za Tanzania.

Awajibishwe kwa mauaji ya halaiki.
 
HAUWEZI ELEWA NA HATA KAMA NIKIKWAMBIA, HAITABADILISHA UKWELI WA KWAMBA.

MOYO WANGU UMEJERUHIKA VIBAYA SANA.
Basi itoshe kukupa pole, mbali na siasa na hawa wanasiasa wakatili, kibinadamu natumai utapata faraja.
 
Hotuba ya kifala ikitolewa na fala na kupigiwa makofi na mafala. Huyu tunae mpaka ateme bungo.
 
Mkuu nafsi haimsuti hata robo, na akipata nafasi ya kurudia trust me atafanya vile vile. Shida ni kelel zenu zinaelekea kutia mchanga kitumbua chake.
Kweli, unakuta analala usingizi poa tu na wala haoni kama kuna lolote baya amefanya
 
  • Thanks
Reactions: naa
Hapa ametudanganya au huyu binadamu hana akili hata ya kwendea chooni. Tulishakubaliana kwamba waliofanya vurugu na kuuawa ni watu kutoka nchi jirani! Sasa hizi pole za nini wakati hapa kwetu hatuna vifo?
Labda anawapa pole hao watu wa nchi jirani waliokufa. Na alivyosema wenzetu, maybe alimaanisha wana Afrika mashariki 🤷‍♀️
 
Ni huzuni!
Japo ni ngumu na inaweza kuwa ni aibu ya kihistoria, Samia angekubali tu kujiuzulu ili kila mtanzania ataishije vinginevyo atarajie kuona miaka mitano migumu sana yenye upinzani ndani na nje ya serikali.
Maumivu na aibu ya kihistoria baba angu kapotea kindezi tu, hata kwenye hayo maandamano hakuwepo. halafu mpuuzi mmoja anakuja kuongea kirahisi tu.
 
Maumivu na aibu ya kihistoria baba angu kapotea kindezi tu, hata kwenye hayo maandamano hakuwepo. halafu mpuuzi mmoja anakuja kuongea kirahisi tu.
Daaah 💔💔 Pole sana mkuu.
Hili haliwezi kupita bila uwajibishwaji wa waliohusika.
 
huyu mama anauwezo mdogo sana wa kubambanua mambo .
Itoshe kusema mama yenu ni zero brain! Hizo pole alitakiwa azitoe siku ya kuapishwa! Halafu alichoharibu siku hiyo ni kutudanganya kwamba waliouawa ni wageni kutoka nchi jirani!
 
Back
Top Bottom