Kambona na Mwalimu, ninaamini walianza kutokubaliana kuhusu muelekeo wa nchi yetu kisiasa na kiuchumi, na pia Mwalimu alianza kumtumia Kawawa kwa ajili ya kumtia nyongo Kambona, hatimaye Kambona akaamua kutimua,
(1). Baada ya Kambona kuondoka, victim wa kwanza alikuwa Dr. Marsha, aliyekuwa katibu mwenenzi wa kwanza wa TANU, alifukuzwa TANU na kupigwa marufuku kuajiriwa na muajiri yoyote bongo, mpaka kibali kitoke kwa Butiku, kila alipojaribu kibali hakikutoka, akapeleka kesi yake UN, wakamchukua na kumsomesha zaidi na kumpa kazi kama Director wa Information kwa angalau 30 years, hadi sasa ni mbunge wa EAC!
(2). Next on line alikuwa General Nyirenda, aliyedaiwa kuhusika na coup, alihamia in exile Zambia, mara ya mwisho nilimuona Lusaka mwaka 1980 kwenye uwanja mmoja wa tenis pale Katima Muliro Road, kwenye viwanja vya bunge la nchi hiyo, nilipoomuuliza kulikoni, alisema kuwa Mwalimu hamtaki bongo, kwa hiyo alimuombea aishi huko!
(3). Bibi Titi na Kamaliza, walihusika na njama za mapinduzi, Mwalimu aliwasamehe kwenda jela, lakini ikawa ndio mwisho wao katika siasa!
(4). Sarakikya, became too powerful na popular huko jeshini, alihamishiwa wizara ya utamaduni, baadaye ubalozi Lagos, Adis, na Nairobi, kwenye uchaguzi uliopita alimwabia Muuungwana in his face kuwa haitakuja kutokea yeye kuwa rais wetu! Sasa hivi ni majority share wa Azania Bank!, siasa kaputi!
(5). Lusinde, alihamishiwa China, baadaye Nairobi, mchezo ukaisha!
(6). Malecela, alifichwa kwenye EAC, baadaye akapewa second chance ya kuwa foreign minister, akajaribu kuwa independent minister kwa kufanya maamuzi mengi on his own, kwa mfano aliposuluhisha vita kati ya Somalia na Idd Amin, hakufuata kabisa maagizo ya Mwalimu, na pia kwenye suluhisho la kwanza la amani kati yetu na Uganda, pia alienda huko na kuamua maamuzi yake mwenyewe, ingawa yalikuwa ni kwa manufaa ya taifa, lakini hayakuwa maagizo ya Mwalimu, na kwa mara ya kwanza Mwalimu akagundua kuwa alianza kuwa na ambitions za urais, akatupwa kilimo, mawasialiano, na Madini, kabla ya kukoseshwa ubunge kabisaa wakati Mwalimu akiwa ana-retire, the plan ilikuwa asirudi tena kwenye siasa,
Mwinyi, akamrudisha as an-act of rebellious against Mwalimu, tena kwa kumtoa Warioba, baada ya hapo Mkapa, Warioba, Apiyo, Butiku na the likes, wakaanza kupishana kwa zamu kwenda Butiama, kumlalamikia Mwalimu, kuhusu Malecela, Mwinyi, na Diria.
......Itaendelea.....