Mafyangula
JF-Expert Member
- Jan 16, 2025
- 557
- 1,039
Aliyewahi kuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais, John Malecela, amewaasa Watanzania kudumisha amani na utulivu kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Jumatano Oktoba 29, 2025, akisisitiza kuwa hakuna kitu cha thamani zaidi ya amani.
Pia, Malecela amewataka wananchi waendelee kumwamini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kuendelea kuliongoza Taifa kutokana na mafanikio yaliyopatikana chini ya uongozi wake katika nyanja za kiuchumi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyoboresha huduma za kijamii nchini.