Malecela and Dr. Salim - Into Oblivion?

Mchambuzi wa mambo, Bwana Joka Kuu ameibuka na kusema kuwa SAS anatuhuma za utovu wa maadili alipokuwa makotopora. Ameendelea kusema kwamba Bwana SAS alifanya kitendo kingine cha aibu kuhusiana na Balozi M, ambaye hakutaka kumalizia jina lake.

Kwa wachambuzi wengine, uamuzi wa Joka Kuu kuogopa kumwaga data kuhusu SAS unaweza kumfanya aitwe jina jipya la JOGA kuu.

Ama kama data zake zitakuwa ni za kweli, anaweza kujikuta katika kundi la kujulikana kama JINGA kuu.

........ndiyohiyo
 
Kwa kweli credibility ya Jokakuu iko matatani sana. Mimi namsihi aje hapa amwage hizo "ze dataz". Jana alijaribu kukwepa kwa kusema kumzungumzia Salim ktk thread ya Malecela ni kutoka nje ya mada. Shukurani kwa mwanzilishi wa mada hii maana sasa hana ujanja labda asingizie yuko katika maandalizi ya Thanksgiving na hana muda wa kuja hapa.
 
Pundit,Nyani Ngabu,

..hivi nyinyi mna umri gani lakini?

..mbona Bibi Ntilie amenielewa na kuamua kuyamaliza?

..thread hii ni ya CYGWIYEMWISI JOHN MALECELA. masuala ya SAS yalikuwa ni side show tu.

..naomba turudi kwenye mada kuu.

mkuu unaweza kutupa ze dataz
 
mkuu unaweza kutupa ze dataz
Kachanchabuseta,

..uchaguzi ukiwa kati ya Dr.Slaa na Dr.Salim, basi kutakuwa na side show ya Mhando vs Balozi.M.

..ukiona mwana CCM yeyote yule over 50 yrs halafu amefanya kazi kwenye system ujue lazima ana kashfa fulani.

..mchukulie mtu kama Ismail Aden Rage. Je, una habari kwamba miaka ya 90 aliwahi kufukuzwa kazi CDA[mamlaka ya ustawishaji makao makuu dodoma] kutokana na kashfa ya ufisadi??

cc: Nyani Ngabu
 
Last edited by a moderator:
Mkapa alifanya kosa kubwa kumwachia JK Urais. Sijawahi kusema kwamba Mkapa hakuwa na dosari. Hata hivyo, ubora wake ambao ninauzungumzia ni mlinganisho kati yake na waliopita, na kujenga kwake uchumi. Udhaifu ulikuwepo vile ile.

Itabidi nikukumbushe kwamba umewahi kutusimulia kuhusu MTANDAO ambao ulimshinikiza Mkapa ampe JK Urais. Kama ulisema kweli, basi huenda Mkapa hakuwa na njia bali kumwachia nchi JK. Tulaumu huo mtandao ndani ya CCM.

Tumetumia takwimu za BoT na za wachumi wengine wa ndani na nje ya nchi kusema wamba Mkapa alijenga uchumi. Wewe unasema hakujenga uchumi bila takwimu. Zipo takwimu zinazoonyesha kwamba unachosema sio kweli.

Nimekuuliza unitajie hao viongozi unaosema JK amewafukuza kazi, na umenipa mapolisi waliofikishwa mahakamani baada ya kuua huko Sinza. Sasa kweli Mzee Es, hao makoplo ndio viongozi unaosema JK amewafukuza kazi?

Kupata mali baada ya kufanya kazi za ngazi za juu ndani na nje ya nchi kwa miaka kama 40 sio kupata utajiri wa haraka. Nadhani Mkapa alikuwa na fedha za kutosha kujenga jumba hata wakati alipokuwa waziri wa Nyerere. Sote tunajua kwamba angejenga ghorofa zito au apartment block wakati huo Mwalimu angemtolea mijimacho mikali ajabu. Angemuita mhuni. Mwalimu alipendezwa zaidi na viongozi aina ya Sokoine ambao walikamata mtu yoyote aliyejaribu kutajirika.

Wizi ni mbaya, lakini kuwa na mali sio vibaya. Kuna wakati Sumaye alianzisha shamba Dodoma, watu wakapiga kelele. Akija mzungu akafungua shamba kubwa na akaweka wazawa wamfanyie kazi za kimanamba, hakuna mtu anazungumza. Lakini akianzisha shamba Sumaye au Mzindakaya, watu chungu mzima wanasema ameiba! Hii hali inaturudisha nyuma. Lazima tujifunze kufurahia wazawa wanapoinuka. Tusione uchungu.

Mimi nafurahi ninapoona wazawa wanavyoangusha majumba kule Mbezi. Kama wameanza kuangusha apartment blocks za nguvu Ubungo na sehemu nyingine vile vle, basi tuwapigie makofi, ili wazidi kuwekeza. Ndiyo nchi inavyojengwa. Sio kwa kuambatia umasikini tu!

Nigependa nione mwaziri na viongozi wakuu wote waliostaafu wanaanzisha mashamba makubwa ya kilimo cha kisasa. Waweke vifaa vya umwagiliaji, na nyumba za nguvu zakuishi kwenye hayo mashamba. Huo uwezo wa kufanya hivyo kwa fedha taslimu au kwa mikopo wanao, lakini wengi wao wanawaogopeni. Mtakasirika! Masikini, wastaafu wetu wamebaki wanafanya vijibiashara vidogo vya kujifichaficha, kama vya kuwa na teksi bubu na bar zinazouza kreti tano, mbuzi wawili na nusu kuku sita kwa siku!

Augustine Moshi
Haha haha kweli muda unapita na mambo yanaenda pia, yule yule aliyelalamikiwa kipindi kile ni yule yule anaye lalamikiwa sasa.

Kwamba alishindwa kurekebisha kile kilichojulikana kama ni makosa ?

Tanzania yetu ...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom