Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,398
- 39,547
a. Sababu ya kwanza na ya msingi ni kuwa Mzee JM ni kiongozi aliyeshindwa. Hakuna kiongozi mwingine yeyote katika historia ya Jamhuri yetu ambaye ameshindwa kiuongozi kuliko Mzee JM. Katika muda wake wote wa uongozi akiwa ameshika nafasi nyingi sijui ni kitu gani alichokifanya (na watu wakakiona) na kuacha alama nzuri ya kukumbukwa. Hapa sizungumzii mambo yanayofanywa kwa siri au nyuma ya Pazia. Hivi ukimuuliza Mtanzania wa kawaida akuambie ni kitu gani alichokifanya Malecela ambacho Taifa litamkumbuka kwacho (zaidi ya nafasi za uongozi na kugombea nafasi Urais) ni nini atakutajia? Ukiwauliza watu hivi Mrema alifanya nini, Mwinyi alifanya nini? Warioba alifanya nini, au Kawawa, Salim etc kuna vitu kadha wa kadha ambavyo vitawajia kichwani. Labda wananchi wa Mtera wanaweza kutupa majibu
b. Alishindwa kuitetea Ilani ya CCM na sera ya CCM juu ya Muungano ilipoibuka mwanzoni mwa miaka ya 1990. Kama kuna kitu ambacho kimetia doa kubwa la kiuongozi dhidi ya Bw. Malecela ni kushindwa kwake kuizuia hoja ya Tanganyika kujadiliwa Bungeni yeye akiwa ni Waziri Mkuu. Kama kuna kitu ambacho kitamfuata mpaka kaburini ni jinsi gani alishindwa kabisa kutetea msimamo wake huo dhidi ya mashambulizi yaliyoongozwa na Mwalimu. Kama ni mtu mwenye msimamo basi wakati ule ndipo angeonyesha uwezo wake wa kutetea hoja (kumbukua alikuwa na wabunge 55 nyuma yake). Hoja ya Mwalimu ilikuwa ni kama anayoitoa Mhe. Mzee Es hapa, kuwa ni lazima kufuata Katiba ya Chama na Ilani ya Chama, na kitu kingine nje ya hicho ni uzandiki na usaliti. Sera na Ilani ya CCM ni kuwa na Serikali Mbili. Kitendo cha Mhe. Malecela kuruhusu wabunge wa CCM kujadili serikali tatu kilikuwa kisichosameheka! Hayo yote yalisababishwa na kuthubutu kwa Zanzibar kujiunga na ile Jumuiya ya nchi za Kiislamu. Badala ya kuvunja hoja na kuweka msimamo wa Jamhuri ya Muungano, Mhe. Malecela akaungana na Wabunge wengine wa bara (kundi 55) kudai "Tanganyika yao".
c. Mzee JM hana jipya. Licha ya madai ya kuwa Mzee huyo anaheshimika sana ndani ya Chama, inaonekana bila ya shaka yoyote, mvuto na heshima hiyo ni hewa. Ameshindwa kujitetea kikamilifu au kujenga hoja zinazoonyesha msimamo wake zaidi ya kukaa chini na kuendelea kupigwa ngumi kulia na kushoto na watu ambao wanaendelea kuimba sifa zake lakini pembeni wanaendelea kumbomoa kisiasa. Baada ya varangati la IOC, Muungano, madai ya Mwalimu dhidi yake, kuenguliwa hatua za mwanzoni, Mzee JM anaendelea kuamini (au kuna watu wanamtaka aamini..) kuwa ana mvuto mkubwa na nguvu kubwa katika Chama. Ukweli ni kuwa Mzee JM hana nguvu hizo isipokuwa ana heshima ya kusikilizwa tu!
d. Amefanya kila aliloweza ndani ya ubinadamu wake kukitumikia chama na Taifa. Ni wakati umefika wa kumuachia mtu mwenye mawazo mapya na nguvu mpya kuungana na timu mpya ya Kikwete katika kutelekeleza majukumu ya chama. Ni kweli alitaka kujiengua huko nyuma lakini "akabembelezwa" akaamua kubakia. Kuna watu ambao wanamfanya aamini kuwa bila yeye CCM itayumba. CCM ni zaidi ya Malecela, Mkapa, RA, EL, EN etc. Itakuwa ni kitendo cha kimahiri na cha kisiasa kuachia umakamu kwani atakaa pembeni na kuona jinsi gani CCM itajaza nafasi hiyo. Sitaki Mzee JM awe kama mzee aliyezoea kusimamia watoto wake kwa kila kitu hadi wamekuwa na nyumba zao lakini bado anaendelea kuendesha maisha yao. Hadi siku mzee huyo anakaribia kufa anabakia kujiuliza kama aliwaandaa watoto kuishi pamoja vizuri. Mzee JM asije akabakia kujiuliza hivi kweli nikiondoka itakuwaje kwenye CCM. Atafanya kitendo cha Kimapinduzi akiamua kung'atuka na kuwaachia kizazi kipya (siyo lazima wawe vijana) kuanza kushika hatamu za uongozi wa Chama.
Ni kwa sababu hizo nne, ninasema kuwa, Mzee JM aamue kustaafu kwa manufaa yake binafsi na kwa ajili ya kukipa Chama nafasi ya kujaza nafasi hiyo kwa wakati mmoja na ile ya Uenyekiti. Atajifanyia mwenye fadhila na familia yake. Anaweza kuendelea kuwa Mbunge wa Mtera na kumaliza kipindi chake lakini hana sababu yoyote ya msingi ya kuendelea kuwa M/Mwenyekiti wa CCM (Bara). Aanze kupumzika kabla baiolojia haijamlazimisha.