DOKEZO Malalamiko kwa NHIF: Nashindwa kupata huduma za Afya pamoja na kulipia kifurushi cha Tsh. Milioni 1.4

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Madaktari naomba niwaulize, kwani miwani sio matibabu ya macho? Kama uono wako unategemea miwani na usipovaa sio tu kwamba huoni bali unaumwa sana na kichwa, kwanini sasa NHIF wanagoma kulipia huduma ya miwani katika vifurushi vyao?

Wiki mbili hizi nimepata mitihani ya kuuguza mzazi wangu na watoto, kwa mpigo na nimekuwa nikilalamikia sana kuhusu NHIF bahati mbaya kila ninayemlalamikia ananishanga kuwa ilikuwaje nikaenda kukata bima hiyo? Yani ni kama watu wamekubali kuwa hii inatakiwa kuwa last option.

Nikiri, naongea kutoka kwenye tabaka la kati. Kwa kipindi hiki ambacho sina muajiri nikaona ni busara nikate bima binafsi. Nilipoenda NHIF niliulizia package ya juu kabisa, nikaambiwa ni TIMIZA, nikalipa 1.4m nikijua yakinikuta makubwa bima itaniokoa - ndio dhana kuu ya bima.

Mara ya kwanza naenda hospital, naambiwa ahaa, bima za makampuni tu ndio zinaweza kutumika hospital hii, bima za vifurushi lazima ukaanzie hosp ndogo umepewa rufaa ndio uje huku. Nikajiuliza kwa nini matabaka ya walioajiriwa na wasioajiriwa yanaendelezwa? wangapi wameajiriwa?

Kwanini hatumpi mtu ambaye hayuko kwenye kampuni options za kuwa na bima yenye faida kama walio kwenye makampuni? Kwanini watu binafsi wanaonekana wote ni walala hoi? Mimi nilidhani, NHIF itafaidika zaidi kama watu wengi watajiunga na mfuko na si kutegemea tu watumishi.

Nikakung'uta dira nikaenda kwenye kituo, baada kumuona daktari akaniomba niende kwa dr mwengine specialist, nikaamua kumsubiri mana alikaribia kuanza clinic yake, nikaambiwa bima inalipa 1 consultation kwa siku hivyo nije kesho. Nikaona hizo hela za wese na time bora nilipe tu.

Mara Bi mkubwa akaumwa, nae ana bima yake ya kifurushi, tukaambiwa tulipie MRI na baadae operation, nikauliza NHIF inatusaidiaje, naambiwa inalipa kitanda, dawa na kumuona dr? I was like seriously? kwanini bima wanachukua majukumu madogo makubwa wanamuachia mgonjwa?

Wakati bado napambana na bi mkubwa yuko wodini, bint karudishwa kutoka shule hoi. Dr kaandika kipimo, nikaambiwa nilipe cash kwa kuwa ni gharama na hakiko kwenye bima, chozi lilinidondoka. Nikajikung'uta nikalipa mtoto akapata matibabu.

Tumeenda kwenye macho, tunaambiwa hapa unalipiwa tu kumuona Dr ila miwani hakuna. Nikamuuliza Dr kwa hiyo kwa taaluma yako hapa tunywe dawa gani ili tuone vizuri? kati yenu na NHIF nani anatakiwa aseme macho yangu yanatibiwaje? Nikaambiwa huduma hiyo inapatikana kwa kampuni.

Anyways to make long story short, NHIF naweza kurudishiwa tushilingi kwangu kaliko baki nikamnunulie kijana miwani? kama huduma zenyewe naishia kuingia mfukoni hiyo chenji itanisaidia sana. Pili natamani viongozi wawe wanajaribu kutumia hizi huduma ili wajue ufanisi wake.

Tatu, bado naamini kuna potential kubwa kwa NHIF kutoa universal coverage kwa watanzania, ila kwanza muondoe hili tabaka la watumishi/kampuni na binafsi. Muwe na huduma kwa segment mbalimbali, kama mtu binafsi anaweza kuafford the best cover, let it be.

Hii dhana ya kama una hela kanunue bima kwenye kampuni binafsi haisaidii sana, mana ili mfuko uimarike mnahitaji watu wengi wachangie, na ili watu wachangie inabidi wapate huduma stahiki, kwa ubora. Sio una bima unaanza kwenda kukopa. Haisadii mchangiaji wala mfuko wenyewe.

Ukweli ni kwamba watanzania sisi wa tabaka hili wengi tunatibiwa na wafamasia, unajisikia ndivyo sivyo unaibuka phamacy unapewa dawa siku inaenda sasa kama coverage ni kumuona Daktari na dawa mnakuwa hamjasaidia sana. Ni vizuri mkafanya tena ethnographic study ya kundi hili letu.

Mwisho mkiona hayo yote hayafai, basi anzisheni bima za viungo, kama bima ya macho miguu, mgongo, kichwa, nk ili niwe na uhakiki kuwa kiungo changu hiki kikipata mushkeli kitatibiwa in full. Tutaongea na viungo vingine visiume na magonjwa ambayo hayako kwenye coverage yasije.
 
Kwanza pole sana
Niliwahi kukutana na hyo changamoto, nakumbuka nilikuwa natumia jubilee insurance ila walikataa kata kata kunipatia matibabu ilihali mzee kila siku anakatwa kwenye mshahara
Kuhs NHIF na miwan, niliwahi kumuulizia daktari akasema bima inachangia 20k tu kwenye miwan ambayo kwenye hospital nyingi, hyo ni bei ya miwani ya kusomea tu
Kama unataka kuchonga miwan, basi itabidi uchangie pesa ya lensi tu, maana fremu itakua imeshalipwa na bima! (Experience fome mbeya zonal referral hospital, MZRH)
Pia, Kuhusu baadhi ya vitu kutolipwa na bima, ni common...bima Iko na baadhi ya vitu vyake ambavyo inaweza kulipa na baadhi haiwezi kulipa na hvyo itakubidi uongeze cash, so ni kawaida
 
Kiufupi kama unajali familia yako hyo 1.4m ungeiweka kwenye hifadhi yako binafsi ukawa unatumia kulingana na huduma uitakayo. Mm sikati bima hata siku moja kwakua najua hakuna hospitali inayokataa cash ikalazimisha uwe na bima kwahyo uamuzi ni wako kulingana na ustaarabu wako wa matumizi.
 
Pole sana mkuu ila hua wanaandika vigezo na masharti kwenye form kabla usign. Kuna matibabu mengine lazima uwe mwanachama uliyechangia miaka miwili ndio unayapata.

Sema watu ambao sio wafanyaz wa serikalini tunateseka na vibima uchwara. Wanapendelewa wafanyakazi wa serikalini sana
 
Tema mate chini ptuuuuu
 
Alafu nikishatema. Acha uoga wa maisha bima za bongo ni utapeli. Mdau hapo kashaliwa hela na bado anatoboka mfuko kwa kitu alichokua anakwepa.
Of coz, kuwa na bima ni kama kujifunga sana kwa sababu kuna matibabu hutayapokea kwa muda au itakubidi uweke cash nyingine
By the way, bima kuna muda inasaidia ukiwa haina hyo cash
 
Kiufupi kama unajali familia yako hyo 1.4m ungeiweka kwenye hifadhi yako binafsi ukawa unatumia kulingana na huduma uitakayo. Mm sikati bima hata siku moja kwakua najua hakuna hospitali inayokataa cash ikalazimisha uwe na bima kwahyo uamuzi ni wako kulingana na ustaarabu wako wa matumizi.

Ipo siku utalia machozi
1.4 sio kitu kene swala la afya likiamua kuibuka

Shukuru tu Mungu kwa uzima ulio nao basi
 
Alafu nikishatema. Acha uoga wa maisha bima za bongo ni utapeli. Mdau hapo kashaliwa hela na bado anatoboka mfuko kwa kitu alichokua anakwepa.
ukienda hosptal ndio utaona umuhimu wa bima. Ndio bima za vifurushi zinalimit lakini zinasaidia sana. Kama hapo bill ya siku moja ukiongeza 50k unapata bima ya najali ya mtu mmoja.
 
Attachments

  • Screenshot_20230812-225545_Messages.jpg
    Screenshot_20230812-225545_Messages.jpg
    21.9 KB · Views: 6
Bima ya afya ni kamali kama kamali zingine. Ila yenyewe imehalalishwa na kubarikiwa. Lengo mama (huwa halisemwi) la kuanzisha bima ya Afya ni Mapato. Lengo la kuzugia (linalowekwa wazi) ni kuwasaidia walengwa kupata matibabu kwa bei nafuu. Mwisho wa siku ni upigaji tu na wachangiaji ndio wanaopigwa.
 
Kwanza pole sana
Niliwahi kukutana na hyo changamoto, nakumbuka nilikuwa natumia jubilee insurance ila walikataa kata kata kunipatia matibabu ilihali mzee kila siku anakatwa kwenye mshahara
Kuhs NHIF na miwan, niliwahi kumuulizia daktari akasema bima inachangia 20k tu kwenye miwan ambayo kwenye hospital nyingi, hyo ni bei ya miwani ya kusomea tu
Kama unataka kuchonga miwan, basi itabidi uchangie pesa ya lensi tu, maana fremu itakua imeshalipwa na bima! (Experience fome mbeya zonal referral hospital, MZRH)
Pia, Kuhusu baadhi ya vitu kutolipwa na bima, ni common...bima Iko na baadhi ya vitu vyake ambavyo inaweza kulipa na baadhi haiwezi kulipa na hvyo itakubidi uongeze cash, so ni kawaida
Mimi sijawahi kuelewa hii logic hasa kwa bima ya NHIF, majuzi nimeenda kufanya vipimo, tena Hospital kubwa ya serikali, nikaambiwa kipimo cha homa ya ini, ambacho ni sh 30,000 hakipo kwenye bima, ila vipimo vingine mpaka vya sh 125,000 vipo kwenye bima!!
 
Pole sana mkuu ila hua wanaandika vigezo na masharti kwenye form kabla usign. Kuna matibabu mengine lazima uwe mwanachama uliyechangia miaka miwili ndio unayapata.

Sema watu ambao sio wafanyaz wa serikalini tunateseka na vibima uchwara. Wanapendelewa wafanyakazi wa serikalini sana
Sasa kwa nini wanaendelea kuhasisha hii bima daily?
 
Mimi sijawahi kuelewa hii logic hasa kwa bima ya NHIF, majuzi nimeenda kufanya vipimo, tena Hospital kubwa ya serikali, nikaambiwa kipimo cha homa ya ini, ambacho ni sh 30,000 hakipo kwenye bima, ila vipimo vingine mpaka vya sh 125,000 vipo kwenye bima!!
Wanabagua sana
Ila Kila bima Iko na rank yake
 
Kiufupi kama unajali familia yako hyo 1.4m ungeiweka kwenye hifadhi yako binafsi ukawa unatumia kulingana na huduma uitakayo. Mm sikati bima hata siku moja kwakua najua hakuna hospitali inayokataa cash ikalazimisha uwe na bima kwahyo uamuzi ni wako kulingana na ustaarabu wako wa matumizi.
Mimi naombaga uzima tu haya masuala ya bima naonaga ni kichefuchefu kitupu 🚮
 
Bima ya afya ni kamali kama kamali zingine. Ila yenyewe imehalalishwa na kubarikiwa. Lengo mama (huwa halisemwi) la kuanzisha bima ya Afya ni Mapato. Lengo la kuzugia (linalowekwa wazi) ni kuwasaidia walengwa kupata matibabu kwa bei nafuu. Mwisho wa siku ni upigaji tu na wachangiaji ndio wanaopigwa.
Ukweli mchungu huuu 👍
 
Back
Top Bottom