hii concept ya utatu mtakatifu inawachanganya wakristo wengi, ukisikiliza wahuburi utaskia wanasema Yesu mwana wa Mungu, baada ya dakika mbili tatu utaskia Yesu ni Mungu, sasa mtu huyohuyo Mungu, huyohuyo mwana wa Mungu!!! na ndo maana wakristo wengi wameona ili kuepuka huo mchanganyo ni bora wamuhalalishe Yesu kama Mungu, hakuna anaemkumbuka Mungu halisi, kwao Yesu ndo mpango mzima.
ukiskiliza pia kwa umakini utaona hata hizo nafsi tatu zenyewe zimepunguzwa otomatikali na kuwa nafsi mbili, yani Mungu mwana na Mungu Roho Mtakatifu, Mungu Baba hutokuja kumsikia kamwe katika maombezi, na ujue kwamba kila mkristo na wachungaji wote kwa ujumla wanapotamka neno Mungu, wanamaanisha Yesu, yani Mungu mwana. Huyo mungu Baba anaonekana hana kazi kabisa ya kufanya..
utasikia "nakukemea katika jina la Yesu", utasikia "karibu Roho mtakatifu", ila kamwe hutasikia karibu Mungu Baba, au nakukemea katika jina la Yahweh, jina ambalo huwezi kumsikia mkristo akilitumia.
mbaya zaidi ni pale mchungaji anaposoma neno kutoka kitabu cha agano la kale, akiwa anatoa tafakari utaskia "KATIKA NENO HILI YESU ANAMAANISHA...." kana kwamba Yesu ndo aliandika Agano la kale, si kufuru hii?
na wengine wamediriki kwenda mbali na kusema Yesu ndo alieumba huu ulimwengu.. mpaka kufikia steji hii unaona kabisa wameshamfutilia mbali Mungu Baba, yani hana alilofanya lolote lile.. NI KUKUFURU KABISA.
Wakristo wamedata na Yesu mpaka wanamsahau mkuu wa wakuu.. Sala ya NASADIKI YA KANISA KATOLIKI INASEMA "Nasadiki kwa Mungu baba Mwenyezi, Muumba wa mbingu na nchi, na vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana."
halafu unakuta kataahira flani humu kanasema Yesu ndo alifanya uumbaji.
kwa kumalizia ni kwamba, utatu mtakatifu sio utatu mtakatifu tena, ni upili mtakatifu, yani Yesu na Roho mtakatifu..
Kwa wakristo wengi Yule Mungu baba hana mpango tena hawezi hata kutoa pepo..
watajitetea kwamba Mungu baba alimpa mamlaka yote Yesu, kana kwamba Yesu alikua hana mamlaka, na hata Yesu alipopewa hayo mamlaka, Mungu baba hakubakiwa na mamlaka yoyote, WHICH MAKES HIM SEEM POWERLESS.
Unaweza kusema Mungu baba yupo tu pale kuukamilisha utatu mtakatifu, ila ukifikiria zaidi utaona HE IS NOT EVEN THERE, BECAUSE HE'S DYSFUNCTIONAL, hakuna hata mkristo mmoja anaemtumia kwa jambo lolote, wao na Yesu, Yesu na wao, na roho mtakatifu mwenyewe anatumika kama BACKUP yani PLAN B, Yesu ndo mpango mzima!!!
Hatari sana wakristo, mnakufuru bila kujijua.
Mathayo 11:27
[27]Akasema, Nimekabidhiwa vyote na baba yangu; wala hakuna amjuaye Mwana, ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba, ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana apenda kumfunulia.
Yohana 16:13-15
[13]Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.
[14]Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari.
[15]Na yote aliyo nayo Baba ni yangu; kwa hiyo nalisema ya kwamba atatwaa katika yaliyo yangu, na kuwapasheni habari. Huzuni Itageuka kuwa Furaha
Mathayo 28:17-20
[17]Nao walipomwona, walimsujudia; lakini baadhi yao waliona shaka.
[18]Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.
[19]Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
[20]na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
Yohana 14:6
[6]Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
Yohana 14:8-9,11,13-17,21,23,26
[8]Filipo akamwambia, Bwana, utuonyeshe Baba, yatutosha.
[9]Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba?
[11]Mnisadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu; la! Hamsadiki hivyo, sadikini kwa sababu ya kazi zenyewe.
[13]Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana.
[14]Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya. Ahadi ya kupewa Roho Mtakatifu
[15]Mkinipenda, mtazishika amri zangu.
[16]Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele;
[17]ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.
[21]Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.
[23]Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake.
[26]Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.
My take:-/kama wakristo wanakufuru basi Mung alianza kukufuru.
Yohana 8:54
[54]Yesu akajibu, Nikijitukuza mwenyewe, utukufu wangu si kitu; anitukuzaye ni Baba yangu, ambaye ninyi mwanena kuwa ni Mungu wenu.
Yesu yuko mkono wa kiume wa Mungu Baba.
Yohana 8:58
[58]Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi niko.
Matendo ya Mitume 4:12
[12]Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.