Makosa 10 aliyotenda Mungu

Makosa 10 aliyotenda Mungu

1 Wakorintho 2:10-16
[10]Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu.
[11]Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu.
[12]Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu.
[13]Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni.
[14]Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni.
[15]Lakini mtu wa rohoni huyatambua yote, wala yeye hatambuliwi na mtu.
[16]Maana, Ni nani aliyeifahamu nia ya Bwana, amwelimishe? Lakini sisi tunayo nia ya Kristo.
 
Sasa mbona unamtisha akili aliyopewa anaitumia kufikiri kama una aya za kutosha mpe c kumwanbia eti anakufuru.
 
1.KUMUUMBA SHETANI:
Hili lilikuwa kosa kubwa sana. Makosa yate yamechepuka kutoka hapa. Shetani anawasababishia watu maovu, then Mungu anawahukumu watu dhaifu. Hapa Mungu inambidi amkamate shetani na kumtokomeza ili maovu yaishe, kama wote wanatoshana nguvu basi wasuluhishe ogomvi wao na kupatana ili maisha yawe ya amani.

2.KUISHI MAFICHONI:
Toka enzi na enzi, Mungu amekuwa akiishi mafichoni, kwanini asijitokeze na kujionesha kwa viumbe vyake? Anaishi mafichoni kwani yeye ni Joseph Kony? Hili limepelekea watu wake kudanganywa na manabii wa uongo na kutapeliwa bure. God come from your hidings and reveal yourself to your people.

3.MAFURIKO YA WAKATI WA NUHU:
Mungu alisababisha mafuriko ili kuangamiza watu waovu na kubakiza watu wema, Yes he did, sasa waovu wa leo wametoka wapi? mbona aliuwa watu wengi bila huruma? Kama mafuriko yalikuwa ni suluhisho la maovu, Yesu na mitume walijia nini? It seems he fought effects instead of causes.

4.SAFARI YA WANA WA ISRAELI:
Mungu aliwatoa wana wa Israel kutoka Misri kwa madai ya kuwapa nchi ya ahadi, matokeo yake aliwaamuru wafanye uvamizi wa nchi za watu(mf. waamori, wamoabu na wakanani). Kwanini asingebadilisha jangwa na kuwatengenezea waisraeli nchi yao? mbona Gadaffi aliweza? Imagine waje wapuuzi hapa TZ wachukue nyumba na ardhi kwa madai kwamba wameagizwa na Mungu, ungereact vipi? WE HAVE TO BE FAIR!

5.KUTOTIMIZA AHADI YAKE KWA ABRAHAM:
Mungu alimwambia Abraham kuwa atampatia uzao wa wana wengi kama nyota za angani au mchanga wa pwani. Sasa hivi ukichanganya walio wa Abrahamu na wasiyo wa kwake bado watu hawawezi kuwa sawa na nyota au mchanga wa pwani. Ata ukijumlisha na waliokufa back to Adam. Atatimiza lini hi ahadi? je kuna muda wa kutosha? mbona watumishi wake wanasema Yesu yuu karibu kuja ili kutamatisha nyakati?

6.KUWEPO KWA MZIO(ALLERGY):
Kwanini watu wengi ambao ni wema wana allergy na vitu alivyoumba Mungu? mbona maandiko yanasema kila alichoumba Mungu ni chema? Kwanini aumbe mimea na wanyama wenye sumu kwa watu wake awapendao? au hakujua?

7.MAJANGA ASILIA:
Kama Mungu aliumba dunia ili iwe sehemu ya amani kwa watu wake na wamwabudu yeye, kwani kuna matetemeko ya nchi, vimbunga na mafuriko. Kwani anawauwa watu kikatili hivi? au haya nayo tumsingizie shetani?

8.KUUMBA VIUMBE HATARISHI:
Kwanini Mungu aumbe bacteria, virusi, fangasi na viumbe wengine wanaosababisha magonjwa na kifo? Kwanini hawa viumbe wasingefia kwenye yale mafuriko ya Nuhu ili watu wema alio wabakiza waishi kwa amani? Je hawa viumbe hatari Mungu alimwamuru Nuhu awaingize wawili wawili kwenye safina?

9.JEHANAMU NA MOTO WAKE:
Kwanini Mungu aumbe jehanamu kuteketeza waovu? Kwani hajui kusamehe? Kwanini huruma yake ina kikomo kwa shetani? Kama wewe ni mzazi, mwanao akikukosea na hajaomba msamaha, itabadilisha uhalisia kuwa yule sii mwanao? SHETANI PAMOJA NA WAOVU NI KAZI YA MIKONO YAKE, PRODUCTS OF HIS OWN MIND BEFORE CREATING THEM. So aache kuweka vinyongo na kutamani kulipiza kisasi juu ya kazi yake.

10.KASORO KWENYE MWILI WA BINADAMU:
Kwanini pawepo na mabadiliko hasi kwenye jeni za binadamu(mutation)? kwani hakujua hicho ni chanzo cha viwete??? Kidole tumbo(appendix) ni cha kazi gani? mbona hajatoa maelezo namna ya kukitumia? Na chuchu za mwanaume ni za kazi gani?

TO THE RIGHT WING OR THE LEFT WING WE ARE NEITHER, NOT EVEN AT THE MIDDLE....R.I.P MOBUTU!

===================
Katika majivuno yake husema: “Mungu hatagundua.” Mawazo yake yote ni: “Hakuna Mungu.” Njia za mwovu hufanikiwa daima; kwake hukumu zako ziko mbali na mawazo yake, na huwadharau maadui zake wote.
Zab 10:4‭-‬5 BHN
 
Ndugu mleta mada, uelewa wapo juu ya MUNGU ni mdogo sana.MUNGU ni ROHO.Wewe unamchukulia MUNGU kama binadamu na hapa ndipo lilipo tatizo lako.
 
Kuna sred zingine humu ukizisoma tu unapata hasira, moja wapo hii.

Ndugu wacha kumzihaki Mungu, Mungu hakosei na kila analofanya ni sawa, wala haulizwi kwa nini umefanya hivi. Na ndio maana anaitwa Mungu
 
Mungu akusamehe na akurehemu, pia akupe kumjua yeye
Yaani mimi kutaka kujua jambo kuhusu Yeye ni kosa la kustahili rehema na msamaha?
Ni Mungu yupi huyo anayesapoti ujinga asiyetaka watu tumjue kwa kuuliza maswali.
 
Kuna sred zingine humu ukizisoma tu unapata hasira, moja wapo hii.

Ndugu wacha kumzihaki Mungu, Mungu hakosei na kila analofanya ni sawa, wala haulizwi kwa nini umefanya hivi. Na ndio maana anaitwa Mungu
Kwamba Mungu aulizwi kwanini umefanya hivi?.....Mbona kwenye maandiko kasema njooni tuhojiane?......Mungu asiyependa kuulizwa kitu huyo ni Dictator.
 
Ndugu mleta mada, uelewa wapo juu ya MUNGU ni mdogo sana.MUNGU ni ROHO.Wewe unamchukulia MUNGU kama binadamu na hapa ndipo lilipo tatizo lako.
Kama wewe umeshamjua Mungu kwa umbo kwamba ni Roho,....Kwa nini unaniona wa ajabu nitakapo kumjua Mungu kimatendo?....Nataka kujua kwa nini afanye hayo matendo yenye kuumiza watu.
 
1.KUMUUMBA SHETANI:
Hili lilikuwa kosa kubwa sana. Makosa yate yamechepuka kutoka hapa. Shetani anawasababishia watu maovu, then Mungu anawahukumu watu dhaifu. Hapa Mungu inambidi amkamate shetani na kumtokomeza ili maovu yaishe, kama wote wanatoshana nguvu basi wasuluhishe ogomvi wao na kupatana ili maisha yawe ya amani.

2.KUISHI MAFICHONI:
Toka enzi na enzi, Mungu amekuwa akiishi mafichoni, kwanini asijitokeze na kujionesha kwa viumbe vyake? Anaishi mafichoni kwani yeye ni Joseph Kony? Hili limepelekea watu wake kudanganywa na manabii wa uongo na kutapeliwa bure. God come from your hidings and reveal yourself to your people.

3.MAFURIKO YA WAKATI WA NUHU:
Mungu alisababisha mafuriko ili kuangamiza watu waovu na kubakiza watu wema, Yes he did, sasa waovu wa leo wametoka wapi? mbona aliuwa watu wengi bila huruma? Kama mafuriko yalikuwa ni suluhisho la maovu, Yesu na mitume walijia nini? It seems he fought effects instead of causes.

4.SAFARI YA WANA WA ISRAELI:
Mungu aliwatoa wana wa Israel kutoka Misri kwa madai ya kuwapa nchi ya ahadi, matokeo yake aliwaamuru wafanye uvamizi wa nchi za watu(mf. waamori, wamoabu na wakanani). Kwanini asingebadilisha jangwa na kuwatengenezea waisraeli nchi yao? mbona Gadaffi aliweza? Imagine waje wapuuzi hapa TZ wachukue nyumba na ardhi kwa madai kwamba wameagizwa na Mungu, ungereact vipi? WE HAVE TO BE FAIR!

5.KUTOTIMIZA AHADI YAKE KWA ABRAHAM:
Mungu alimwambia Abraham kuwa atampatia uzao wa wana wengi kama nyota za angani au mchanga wa pwani. Sasa hivi ukichanganya walio wa Abrahamu na wasiyo wa kwake bado watu hawawezi kuwa sawa na nyota au mchanga wa pwani. Ata ukijumlisha na waliokufa back to Adam. Atatimiza lini hi ahadi? je kuna muda wa kutosha? mbona watumishi wake wanasema Yesu yuu karibu kuja ili kutamatisha nyakati?

6.KUWEPO KWA MZIO(ALLERGY):
Kwanini watu wengi ambao ni wema wana allergy na vitu alivyoumba Mungu? mbona maandiko yanasema kila alichoumba Mungu ni chema? Kwanini aumbe mimea na wanyama wenye sumu kwa watu wake awapendao? au hakujua?

7.MAJANGA ASILIA:
Kama Mungu aliumba dunia ili iwe sehemu ya amani kwa watu wake na wamwabudu yeye, kwani kuna matetemeko ya nchi, vimbunga na mafuriko. Kwani anawauwa watu kikatili hivi? au haya nayo tumsingizie shetani?

8.KUUMBA VIUMBE HATARISHI:
Kwanini Mungu aumbe bacteria, virusi, fangasi na viumbe wengine wanaosababisha magonjwa na kifo? Kwanini hawa viumbe wasingefia kwenye yale mafuriko ya Nuhu ili watu wema alio wabakiza waishi kwa amani? Je hawa viumbe hatari Mungu alimwamuru Nuhu awaingize wawili wawili kwenye safina?

9.JEHANAMU NA MOTO WAKE:
Kwanini Mungu aumbe jehanamu kuteketeza waovu? Kwani hajui kusamehe? Kwanini huruma yake ina kikomo kwa shetani? Kama wewe ni mzazi, mwanao akikukosea na hajaomba msamaha, itabadilisha uhalisia kuwa yule sii mwanao? SHETANI PAMOJA NA WAOVU NI KAZI YA MIKONO YAKE, PRODUCTS OF HIS OWN MIND BEFORE CREATING THEM. So aache kuweka vinyongo na kutamani kulipiza kisasi juu ya kazi yake.

10.KASORO KWENYE MWILI WA BINADAMU:
Kwanini pawepo na mabadiliko hasi kwenye jeni za binadamu(mutation)? kwani hakujua hicho ni chanzo cha viwete??? Kidole tumbo(appendix) ni cha kazi gani? mbona hajatoa maelezo namna ya kukitumia? Na chuchu za mwanaume ni za kazi gani?

TO THE RIGHT WING OR THE LEFT WING WE ARE NEITHER, NOT EVEN AT THE MIDDLE....R.I.P MOBUTU!

===================
eti chuchu za nini kwa wanaume? we kweli kilaza, tubu mpokee yetu akisamehe
 
Mleta mada IQ yako ni ndogo sana. Na ujuzi wako wa biblia ni mdogo kiasi kwamba huelewi lolote. Mungu akusamehe tu. Ni wapi kwenye biblia umesoma kwamba Mungu alimuumba shetani? Mungu aliumba malaika na walipoasi wakageuka kuwa mashetani. Hujui uzao wa Ibrahim ni kina nani ndio maana unasema ni wachache. Na unaposema Mungu alifanya 'makosa' hayo makosa alimtendea nani? Yaani you dont even know definition ya kosa ni nini? Kosa ni kitendo kinachokwenda kinyume na amri ya mtu au mfumo fulani. Hayo unayosema ni 'makosa' ya Mungu yameenda kinyume na amri au mfumo uliowekwa na nani? Mungu akurehemu maana hujui lolote !
 
Back
Top Bottom