Mbona unahaha sana??? wao kama wamemdhihaki Mungu mimi inanihusu vipi??? Kwani Mungu si anajua mahusiano yake na watu wake??? Kama watu hawana uelewa juu ya Mungu, kwanini awauwe badala ya kuwapa imani na kuwaelimisha???...mimi nahitaji majibu wewe unaniforwadia jumbe zisizo na mashiko....Kwahiyo ambao hawakumdhihaki Mungu waliishi milele???HAWA NI WATU WALIOMDHIHAKI MUNGU NA KUPATWA NA MAJANGA.
1. JOHN LENNON (MUIMBAJI)
Wakati alipokuwa akihojiwa na mwandishi wa habari wa gazeti la American alinukuliwa akisema hivi "Ukristo utakufa na kutoweka duniani, siwezi kuwa na wasiwasi na hilo kwa kuwa nina uhakika nalo. Mafundisho ya Yesu yalikuwa sahihi na wala sipingi hilo ila mafundisho yale yalikuwa mepesi sana ambayo mtu yeyote anaweza kuyafundisha. Hebu angalia leo, tumekuwa maarufu hata zaidi yake (Hapo alilitaja kundi lake la muziki the beatles. Ilikuwa mwaka 1966.
Wiki moja baada ya kutamba kwamba yeye na kundi lake lilikuwa maarufu hata zaidi ya Yesu, akapigwa risasi sita na kufariki.
2. TANCREDO NEVES (RAIS WA BRAZIL)
Alisema kwamba endapo angepata kura laki tano kutoka katika uchaguzi mkuu wa Brazil na kuwa rais, hata MUNGU asingeweza kumtoa katika urais huo. Akafanikiwa, akapata kura zaidi ya hizo, akashinda uchaguzi, siku moja kabla ya kuapishwa, akafariki dunia.
3. CAZUZA (MWANAMUZIKI WA BRAZIL)
Alipokuwa katika shoo yake ndani ya jiji la Rio De Janeiro, alichukua sigara, akaanza kuivuta, akachukua nyingine na kisha kuirusha juu na kusema "Mungu, hiyo yako, chukua nawe uvute"
Alifariki akiwa na miaka 32 kwa ugonjwa wa kansa ya mapafu ambayo iliyaharibu sana mapafu yake kuliko mgonjwa yeyote yule.
4. MTENGENEZAJI WA MELI YA TITANIC.
Baada ya kutengeneza meli ya Titanic, mwanahabari akamuuliza ni kwa kiasi gani ilikuwa salama nae akajibu "Ni salama sana, haiwezi kuzama na hata Mungu hawezi kuizamisha"
Nafikiri unajua kilichotokea kuhusu Titanic.
5. BON SCOTT (MUIMBAJI)
Mwimbaji huyu ambaye alitamba miaka ya 70 alitoa wimbo wake mmoja mwaka 1979 wenye maneno haya
"Don't stop me; I'm going down all the way, down the highway to hell'.
Tarehe 19 February mwaka 1980, alikutwa amekufa baada ya kupaliwa na matapishi yake.
6. Mwanamke mmoja alikuwa akihofia sana kuhusu ulevi wa marafiki wa mtoto wake. Wakati wanataka kuondoka na gari, akamshika mtoto wake mkono garini na kumwambia "Binti yangu, Mungu awatangulie katika safari yenu" Yule binti akajibu "Gari imejaa mama, huyo Mungu labda akae kwenye boneti la gari".
Baada ya masafa fulani ya safari yao, gari lile lilipata ajali kiasi ambacho hata polisi hawakujua ni aina gani ya gari lilikuwa. Lilikuwa limebondeka sana na watu wote walikutwa wamekufa. Kilichowashangaza polisi, trey la mayai wala halikuonekana kuguswa na hakuna hata yai moja lililokuwa limevunjika na wakati gari lilibondeka mpaka kutokutambulika.
7. CHRISTINA HEWITT (MWANDISHI WA HABARI)
Huyu alikaririwa akisema hivi "Nimesoma vitabu vyote duniani, ila hakuna kitabu kibaya...kibaya na kibaya kama Biblia"
Siku chache baada ya kusema maneno hayo, mwili wake ulikutwa umeunguzwa na moto ambao haikujulikana mpaka leo ule moto ulisababishwa na nini.
8. MARILYN MONROE (MUIGIZAJI)
Huyu alifuatwa na Bill Graham na kumwambia kwamba alitumwa na Roho wa Mungu kwa ajili ya kumhubiria. Alimkaribisha ndani, akamsikiliza kwa makini, alipomaliza akasema "Simhitaji Yesu wako, unaweza kuondoka nae". Wiki moja baadae, alikutwa amekufa katika makazi yake. Polisi walijaribu kuchunguza kipi kilimuua, mpaka leo hawajapata jibu.
Kwa wale wanaotaka kujua mengi, wafungue GOOGLE na kisha kusearch haya "People who mocked GOD and died" Utasoma mengi tu.
*Watumie ujumbe huu ndugu na jamaa,ujumbee huu utawasidia kumuheshimu Mungu na kumtii.
Hali ya kumcha Mungu iongezeke ndani yako na kama nikuuliza maswali basi yafaa kuuliza kwa lengo la kujifunza na siyo kutengeneza ubishi usio na lazima.
Amina
Umetoa majibu mazuri sana, ila yapo OP na hoja zangu...mf. kwenye zab. 14:1 inasema ''Mpumbavu anasema moyoni mwake hakuna Mungu, matendo yao ni maovu kabisa, hakuna atendaye mema'' Je kunasehemu niliyosema hakuna Mungu??? kama ipo onesha.,,,,Ayubu 1:22 wewe jua kunatofauti kati ya kulaumu na kuuliza, mimi sijalaumu bali nimeuliza, ndio maana niliweka alama za kuuliza. Mathayo 12:36, kwani maswali yangu hayana maana??? mbona Yesu aliulizwa maswali na kujibu??Mtoa mada unajaribu ku-temper na mziki mzito sana, kwa Upumbavu.
Ayubu 1;22
Ayubu 24;12
Mathayo 12:36
Zabur 14:1
Ukatubu.
wanasema tufumbe macho tuite uwepo wa Mungu, wakati biblia inasema Mungu yupo kila sehemu, na kipengele kingine kinasema wakusanyikapo wawili kwa ajili ya neno langu, mimi nipo kati yao.. hii ya kuita uwepo wa Mungu ndo kama ile ya mganga kupandisha mashetani kuwaita WAUNGWANA, hamna tofauti.. sasa kama hizi practice za kiganga zipo hadi makanisani hili ni tatizo pia.. kumuita Mungu angali yupo mahala popote ni sawa na kutafuta peni wakati umeishika mkononi.. HII NI ISHARA YA KUTOKUAMINI NA KUTOJIAMINI.Walevi WA dini hao ndiyo hawajiulizagi wanao wasisitiza waamin uwepo wa mungu., wenyewe ni illuminat wakubwa sana..kiukweli mungu amuondowe shetani Kwa mana naona anamzidi kete aisee.
Hahahahaa nimecheka sana mkuu....kwahiyo baada ya kukosa cha kujibu umeamua kutiririsha maombi??? lol aya bhana."Ee baba Mungu Wa mbinguni, naomba unisamehe kwa sababu nimefungua Uzi huu nikakuta matusi yanatukanwa juu yako, baba naomba uwasamehe watu hawa kwa sababu hawajui kuwa wewe ndie Mungu ulie waumba, samehe uovu wao.
Wape rehema bwana. Akili hizi sio zao Bali ni akili za yule mwovu.
Ninaomba ktk jina LA Yesu, Amen"
Watu wawili walipanda kwenda Hekaluni kusali: mmoja Mfarisayo, na mwingine mtoza ushuru."Ee baba Mungu Wa mbinguni, naomba unisamehe kwa sababu nimefungua Uzi huu nikakuta matusi yanatukanwa juu yako, baba naomba uwasamehe watu hawa kwa sababu hawajui kuwa wewe ndie Mungu ulie waumba, samehe uovu wao.
Wape rehema bwana. Akili hizi sio zao Bali ni akili za yule mwovu.
Ninaomba ktk jina LA Yesu, Amen"
Hata baada Ya Yesu kusurubishwa msalabani, aliwaombea msamaha wale waliomtesa.Hahahahaa nimecheka sana mkuu....kwahiyo baada ya kukosa cha kujibu umeamua kutiririsha maombi??? lol aya bhana.
Mimi ni mpole, pia ninalotumaini kuu ndani ya kristo Yesu.Watu wawili walipanda kwenda Hekaluni kusali: mmoja Mfarisayo, na mwingine mtoza ushuru.
Luka 18:11 Huyo Mfarisayo akasimama, akasali kimoyomoyo: `Ee Mungu, nakushukuru kwa vile mimi si kama watu wengine: walafi, wadanganyifu au wazinzi. Nakushukuru kwamba mimi si kama huyu mtoza ushuru.
18:12 Nafunga mara mbili kwa juma, natoa zaka sehemu ya kumi ya pato langu.`
18:13 Lakini yule mtoza ushuru, akiwa amesimama kwa mbali bila hata kuinua macho yake mbinguni, ila tu akijipiga kifua kwa huzuni, alisema: `Ee Mungu, unionee huruma mimi mwenye dhambi.`
Nawaambieni, huyu mtoza ushuru alirudi nyumbani akiwa amesamehewa. Lakini yule mwingine, sivyo. Kwa maana kila anayejikweza atashushwa, na kila anayejishusha atakwezwa."
KUWA MPOLE BLAZA.
tatizo ni kuelewa huu uzi unataka nini..sistaajabu sababu hata maswali ya short notes watu huandikaga essay.. bado hujatoa elimu, umehukumu.Mimi ni mpole, pia ninalotumaini kuu ndani ya kristo Yesu.
Na nimemkiri Yesu kama Bwana na mwokozi Wa maisha yangu.
Mkuu usiwe mkali sana na jaribu kupunguza ukali wa maneno hata kama hauamini uwepo wa Mungu.Mbona unaimba Ngonjera? Kwaiyo walio na kansa, wanaojinyea na walioko mahospitali ndio tuseme kuna mungu muweza au mungu dhaifu?
Wewe kijana unaabudu uoga!
Narudia tena kwamba hakuwezekani kuwe na Mungu mjuzi wa yote, mwenye upendo, muweza wa yote, muumbaji wa vyote.
Kama atakuwepo mungu wa hivo atakuwa sio mungu bali ni mshindwa wa mwisho.
Fikiri kijana acha kukalia akili zako
HAKUWEZEKANI KUWE NA MUNGU MSHENZI NAMNA HIYO.
Watu wanateseka hovyo, watu wanakufa, watu wanadhulumiana, watu wanaibiana, watu wanateseka na njaa hadi kufa alafu uje uniambie kuna mshenzi kajikalia eti ndio aliyeumba vyote na anaweza yote na ana upendo.
Huo utakuwa ni ulimbukeni wa Mungu
"Ee baba Mungu Wa mbinguni, naomba unisamehe kwa sababu nimefungua Uzi huu nikakuta matusi yanatukanwa juu yako, baba naomba uwasamehe watu hawa kwa sababu hawajui kuwa wewe ndie Mungu ulie waumba, samehe uovu wao.
Wape rehema bwana. Akili hizi sio zao Bali ni akili za yule mwovu.
Ninaomba ktk jina LA Yesu, Amen"
Hahahha!Nachofurahia hii thread itawaunganisha wakristu na waislam, wapagan ndo watakuwa kivyao