Hakuna baba Mokaze bila Mokaze. Unakubali hili? Nalo pia linahitaji tafakari kidogo. Nami ninakuomba ujipe muda zaidi kutafakari.
Bado ninauliza, katika hali yako ya kutokuwepo, kipi haswa kipo? Bado ninakuomba tena, jipe muda zaidi wa kutafakari. Unaweza kuona mantiki yake. Just give yourself some more time.
Ndugu yangu Oltung'anyi.,
Unaposema kuwa "hakuna baba Mokaze bila Mokaze", hiyo ni kauli tata (ambiguous sentence) ambayo inahitaji ufafanuzi ili ieleweke, na mimi nitakusaidia kuifafanua, mfano Baba mokaze anaitwa Rashid, kwa hiyo unaposema hakuna baba Mokaze bila Mokaze kwa maana ya Rashid, hapo siyo kweli, kwani Rashid atabaki kuwa Rashid regardless of Mokaze yaani Mokaze na Rashid ni entities mbili tofauti (personification) na Rashid alikuwepo kabla ya Mokaze, Lakini ukisema hakuna Baba Mokaze bila Mokaze kwa maana ya Majina (identification) kwamba Baba Mokaze ndiye alimzaa Mokaze, hapo upo sahihi.
Na mimi ninamzungumzia Mungu kama "independent entity" (nafsi inayojitegemea) na siyo identification ya majina. Naye Mungu alikuwepo kabla ya chochote na atabaki kuwepo hata baada ya vyote kuondoka.
Unauliza tena swali lilelile kwamba;- " katika hali yako (yangu) ya kutokuwepo kipi hasa kipo"---- labda hapo ungefafanua, kipi kipo wapi??, lakini lazima ujue tunazungumzia juu ya "medium" ya hapa duniani, hivyo tunaposema kuwepo kwa kitu maana yake ni kuwepo hapa duniani tunapoishi na si mahali pengine.
Sasa katika hali ya mtu kutokuwepo, vitu na watu wanakuwepo/watakuwepo, mfano kabla hujazaliwa (hukuwepo) lakini dunia na vilivyomo ilikuwepo, wazazi wako walikuwepo, na tunaona kila siku ndugu na jamaa zetu wakifariki na sisi pia tutafariki (kutokuwepo) lakini "they leave behind" dunia na vilivyomo na watu nk.vikiwepo.
Hivyo kuwepo na kutokuwepo kwetu hakuna mahusiano/effect yoyote na kuwepo au kutokuwepo kwa vitu vingine.
Bottom line:- Mungu yupo na kuwepo kwake haku athiriwi na kuwepo au kutokuwepo kwa vitu vingine isipokuwa hivyo vitu vinaonyesha "utambulisho" wa Mungu kwa sababu ni yeye aliyeviumba na Yeye alikuwepo kabla vitu hivyo kuwepo.
👆🏻Ndugu yangu Oltung'anyi tafakari sana juu ya maneno hayo.