Makosa 10 aliyotenda Mungu

Makosa 10 aliyotenda Mungu

Akili zake mbovu za kushika nyeti zako unazielezeaje mkuu?
Like father like son....unafikiri atakuwa kajifunza kwa nani??? Baba mkaa uchi, mtoto mchoma d*le....wote hawana akili!!!!
 
Mkuu nimesoma na kucheka sana.Ni vizuri kukaa na kujiuliza namna hii.Kuna maswali hayana majibu hadi sasa.Wakatoliki kwa majiulizo ambayo tumekosa majibu tumeyaita "Fumbo la Imani". Kuhoji hoji namna hii sio dhambi.
Wakatoliki tunafundishwa kuwa sababu za Mungu kutuumba ni ili:
1.Tumjue
2.Tumpende
3.Tumtumikie
4.Kisha Tufike au tuwepo kwake Mbinguni

Ukitafakari hayo mambo manne utagundua kuwa mtu yeyote ili amjue Mungu lazima atajiuliza maswali kama yako kwenye huu uzi.Mimi niseme labda sio sahihi kuhitimisha kuwa Mungu alifanya Makosa kufanya yote kadri ya uzi wako ila labda ziko sababu mahususi tusizozijua bado.

Nihitimishe tu kwa kukushukuru sana kwa hojaji zako na uzidi kuutafuta ukweli.Ninakuona kama potential Philosopher of the future.
Sawa mkuu nimekupata kiasi flani,,,,wanaofundisha mengine hawayajui....mbona wengine walikufa bila kumjua Mungu????
 
"kama wote wanatoshana nguvu basi wasuluhishe ogomvi wao na kupatana ili maisha yawe ya amani"-mwisho wa kunukuu.
Duh wewe jamaa umenifanya niishie kucheka tu usiku huu,nna uhakika hakuna atakaekupa jibu kwenye maswali yako zaidi watakuletea vitisho tu na blah blah lundo maana sisi wafia dini wengi tumekariri kuhusu dini na tukishtukizwa kama ivi silaha yetu ni kukutisha umekufuru,naona hapa Wakristo kwa Waislamu wanahaha nini wajibu.
Nahitimisha kusema kwa hakika wewe ni GT haswaaaa umeleta mjadala ambao maswali yake mengi sisi tulio wengi hata kujiuliza kwenye nafsi zetu tunaogopa tukiamini ni dhambi ila wewe umethubutu kuuliza na ajabu wanaotakiwa wajibu nao wanaogopa haaaa haaaa.
 
Mlio soma bible na islamic knowledge naomba mjibu kwa hoja zenye mashiko na km hakuna jibu basi si vibaya Maana tunajua Mungu yupo ila kuna maswali ambayo sisi ambao hatujasoma dini kwa undani hua tunajiuliza na machache ni hayo aliyo yataja Chamiton ila sidhani km kuuliza swali sasa imkua ni kukufuru
 
Kwenye vitabu vya dini mungu kila kitu kaweka wazi shetani ni yupi na vitendo vyake ni vipi ukitaka kuamini binadamu ni kiumbe mmbishi ni hapa sigara imeandikwa kabisa inamadhara kwa afya ya mwanadamu na huyohuyo anavuta huku akijua kuwa amavuta kitu cha hatari hii imekaaje
Ndio mna fail watu wa dinii na dini zenu jibu maswali yangu kiifasaha.....
 
Mtoto kushindana na baba,mtoto hana adabu pia mtoto kumkosoa baba, wanasema mtoto amepata malezi ya upande mmoja, Hata kama ni u-great think sio namna hii labda u-great think wa shetan
 
Kweli hujakosea but mungu muache aitwe mungu kwasababu ni mungu.
 
Hewa ya oxygen ipo ni ordourless, colourless, tasteless and it support combustion....Chemistry uliicha form two eeh???
Nilijua tu kama utakuja hapo sasa kama utaitambua oxygen kwa kusupoti moto na sisi tunaamini kuwepo kwa mwenye ulimwengu huu ambae ni mungu kwa kupanda mbegu moja ya hindi lakini zinaota nyingi na ni yule anafanya usiku na mchana na yule anaeutembeza mwezi katika njia yake anaefanya maji dhariri kabisa shahawa zitoke kiumbe chenye kutoa kejeli zidi yake
 
I
Sawa mkuu nimekupata kiasi flani,,,,wanaofundisha mengine hawayajui....mbona wengine walikufa bila kumjua Mungu????
Iko hivi Mungu amekuwa akiwafundisha binadamu hatua kwa hatua.Ni kama wewe ulivyojifunza: hesabu kwa mfano ya 2-5 darasa la I na II ilikuwa haina majibu lakini darasa la tano ikaanza kupata majibu.Au Square root of a negative number kwa O'level haina majibu lakini Alevel majibu yapo.

Ukiangalia mambo mengi tu huko nyuma kwenye historia ya mwanadamu uelewa wake ni tofauti na leo.Baadhi ya majibu yalikuja kutolewa na Yesu.Na hata mengine sasa yanatolewa ufafanuzi kwa njia ya Roho Mtakatifu kwa njia ya tafiti za Kisayansi.Kwa hiyo tuendako maishani tutapata pengine majibu kwa kila lisilo kuwa na maelezo yakinifu kwa njia muafaka kulingana na mazingira ya wakati huo.Mungu hana haraka kama binadamu maana hana deadline au timeline kama binadamu.Yeye hufunua mambo kutegemea na uwezo wa binadamu kupokea(perception capacity)
 
Naamini kwa kufuru hizi Chamiton unahitaji kutubu kwa Mungu ama sivyo siku zako si nyingi hautakuwepo duniani ,naapa kwa Mungu kwa jina la Yesu kwa hili umekosa kitu cha kudhihaki.
 
😡😡 Mpaka sasa hivi sijaona kosa la Mungu In all your thread,sema wewe ndo upo short minded
 
Ngoja niongeze Mkuu, kuwapa Wazungu maarifa kiasi cha kuonekana bila wao mambo hayaendi
 
Chamiton, miili yetu sisi binadamu ni dhaifu sana hatuwezi kustahimili tukiviona vya Rohoni, Mungu wetu yupo Kiroho ina maana unamwona kimatendo kama ukifata yale aliyoyaamuru kama Amri Kumi zilivo. Kiufupi tuliwekewa mipaka ya kumjadili Mungu
 
1.KUMUUMBA SHETANI:
Hili lilikuwa kosa kubwa sana. Makosa yate yamechepuka kutoka hapa.Shetani anawasababishia watu maovu, then Mungu anawahukumu watu dhaifu. Hapa Mungu inambidi amkamate shetani na kumtokomeza ili maovu yaishe, kama wote wanatoshana nguvu basi wasuluhishe ogomvi wao na kupatana ili maisha yawe ya amani.

2.KUISHI MAFICHONI:
Toka enzi na enzi, Mungu amekuwa akiishi mafichoni, kwanini asijitokeze na kujionesha kwa viumbe vyake??? Anaishi mafichoni kwani yeye ni Joseph Kony???..Hili limepelekea watu wake kudanganywa na manabii wa uongo na kutapeliwa bure...God come from your hidings and reveal yourself to your people.

3.MAFURIKO YA WAKATI WA NUHU:
Mungu alisababisha mafuriko ili kuangamiza watu waovu na kubakiza watu wema, Yes he did...sasa waovu wa leo wametoka wapi??? mbona aliuwa watu wengi bila huruma??? Kama mafuriko yalikuwa ni suluhisho la maovu, Yesu na mitume walijia nini??? It seems he fought effects instead of causes.

4.SAFARI YA WANA WA ISRAELI:
Mungu aliwatoa wana wa Israel kutoka Misri kwa madai ya kuwapa nchi ya ahadi, matokeo yake aliwaamuru wafanye uvamizi wa nchi za watu(mf. waamori, wamoabu na wakanani). Kwanini asingebadilisha jangwa na kuwatengenezea waisraeli nchi yao??? mbona Gadaffi aliweza???.Imagine waje wapuuzi hapa TZ wachukue nyumba na ardhi kwa madai kwamba wameagizwa na Mungu, ungereact vipi???...WE HAVE TO BE FAIR!!!

5.KUTOTIMIZA AHADI YAKE KWA ABRAHAM:
Mungu alimwambia Abraham kuwa atampatia uzao wa wana wengi kama nyota za angani au mchanga wa pwani. Sasa hivi ukichanganya walio wa Abrahamu na wasiyo wa kwake bado watu hawawezi kuwa sawa na nyota au mchanga wa pwani. Ata ukijumlisha na waliokufa back to Adam. Atatimiza lini hi ahadi??? je kuna muda wa kutosha??? mbona watumishi wake wanasema Yesu yuu karibu kuja ili kutamatisha nyakati???

6.KUWEPO KWA MZIO(ALLERGY):
Kwanini watu wengi ambao ni wema wana allergy na vitu alivyoumba Mungu??? mbona maandiko yanasema kila alichoumba Mungu ni chema??? Kwanini aumbe mimea na wanyama wenye sumu kwa watu wake awapendao??? au hakujua???

7.MAJANGA ASILIA:
Kama Mungu aliumba dunia ili iwe sehemu ya amani kwa watu wake na wamwabudu yeye, kwani kuna matetemeko ya nchi, vimbunga na mafuriko....Kwani anawauwa watu kikatili hivi???au haya nayo tumsingizie shetani???

8.KUUMBA VIUMBE HATARISHI:
Kwanini Mungu aumbe bacteria, virusi, fangasi na viumbe wengine wanaosababisha magonjwa na kifo??? Kwanini hawa viumbe wasingefia kwenye yale mafuriko ya Nuhu ili watu wema alio wabakiza waishi kwa amani???.Je hawa viumbe hatari Mungu alimwamuru Nuhu awaingize wawili wawili kwenye safina???

9.JEHANAMU NA MOTO WAKE:
Kwanini Mungu aumbe jehanamu kuteketeza waovu??? Kwani hajui kusamehe???Kwanini huruma yake ina kikomo kwa shetani?. Kama wewe ni mzazi, mwanao akikukosea na hajaomba msamaha, itabadilisha uhalisia kuwa yule sii mwanao??? SHETANI PAMOJA NA WAOVU NI KAZI YA MIKONO YAKE, PRODUCTS OF HIS OWN MIND BEFORE CREATING THEM...So aache kuweka vinyongo na kutamani kulipiza kisasi juu ya kazi yake.

10.KASORO KWENYE MWILI WA BINADAMU:
Kwanini pawepo na mabadiliko hasi kwenye jeni za binadamu(mutation)??? kwani hakujua hicho ni chanzo cha viwete??? Kidole tumbo(appendix) ni cha kazi gani??? mbona hajatoa maelezo namna ya kukitumia??? Na chuchu za mwanaume ni za kazi gani???

TO THE RIGHT WING OR THE LEFT WING WE ARE NEITHER, NOT EVEN AT THE MIDDLE....R.I.P MOBUTU!!!
Mungu akusamehe duuuuuuuh
 
Ndio mna fail watu wa dinii na dini zenu jibu maswali yangu kiifasaha.....
Uwezi ukasema tujibu swali wakati umetoa maelezo we vipi?tatizo lako wewe hujasoma vitabu vya dini lau kama ungewasoma waisrael ndani ya qur an basi usingetoa maelezo dhidi ya waisrael ungejua kwanini waliaidiwa nchi kisha wakatangatanga mpaka leo
 
1. Hakumuumba Shetani. Aliumba kiumbe chema, chenye utashi wa kuamua. Kiumbe hicho kikaamua kuwa Diavolo.

2. Amewatembelea viumbe wake mara kwa mara. Pale Bustanini Edeni. Pia alikatisha kwenye mitaa ya Nazareti n.k.

3....

ITAENDELEA
 
Chamiton, miili yetu sisi binadamu ni dhaifu sana hatuwezi kustahimili tukiviona vya Rohoni, Mungu wetu yupo Kiroho ina maana unamwona kimatendo kama ukifata yale aliyoyaamuru kama Amri Kumi zilivo. Kiufupi tuliwekewa mipaka ya kumjadili Mungu
Iko wapi hiyo mipaka??? Kama Mungu aliituumba kwa sura na mfano wake, ya nini kitishana na kuogopeshana kiasi cha yeye kujificha mbali na sisi???
 
Back
Top Bottom