Makonda na Drama za Watumishi wa Umma

ntemintale

JF-Expert Member
Sep 6, 2016
952
1,872
Paul Makonda ni Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi. Bila kuathiri Muundo wa Utumishi Serikalini, yeye Makonda ni Kiongozi wa Chama Cha Siasa Kama ilivyo kwa Chadema, TLP na CUF. Kwa hiyo chain of Command ya Utendaji wa Serikali haimtambui Mwenezi wa Chama Cha Siasa kuwa ni Reporting Unit kwenye Chain of Commnd ya Serikali.

Kitendo cha kuwasimamisha hadharani watumishi wa Serikali na kuwahoji Kisha kutoa maelekezo na hukumu ni Kinyume cha sheria kanuni taratibu za Utumishi na utawala bora.

Tutafakari kidogo, Je mwenezi wa Chadema, CUF, TLP na vyama vingine navyo vikiamua kuwahoji Watumishi hadharani, tutakuwa na utaratibu wa aina gani?

Serikalini kuna taratibu zilizo wazi za kupeleka malalamiko na mamlaka za kinidhamu zipo kutenda haki ikiwemo Kukata Rufaa.

Hizi Drama za Makonda kwa Watumishi zina lengo lipi. Kumbuka hata watumishi wa Serikali nao ni watu na wana haki sawa ya kuheshimiwa na wajibu wa kutenda haki
 
1706387919287.jpg
8
1706387919287.jpg
1706387919287.jpg
1706387919287.jpg
1706387924419.jpg
1706387924419.jpg
 

Attachments

  • 1706387929448.jpg
    1706387929448.jpg
    53.8 KB · Views: 3
  • 1706387936305.jpg
    1706387936305.jpg
    78.8 KB · Views: 5
Ni kweli, kwa umati uliojitokeza Kahama kuja kumiliki, mimi mpaka nimeovopa!, amepolelewa kama Masiha alivyopokelewa ile siku anaingia Jerusalem, halafu siku chache baadaye ndio ilawa vile!.
P
Tumekuelewa wachache Sana

Ukweli kinachoenda kutokea ni kibaya
Hapo akipita mwanasiasa mwingine na kuwafumbua macho Wananchi itakaa vizuri

Wananchi wataulizwa swali moja tu
Alipopita yule Bwana wangapi walisaidiwa Onyesheni mikono juuu
Wangapi hawakusaidiwa nyoosheni mikono juuu

Hapo utakuwa mwisho wa maigizo!!!
 
Umati ambao unaamini kwamba Paul Makonda atautatulia shida na kero zinazowakabili ambazo zimeshindikana kutatuliwa kwa muda mrefu.

Shida zilizoletwa na Viongozi na Watawala wa Serikali ya Chama cha Mapinduzi.

Tujiulize, kwa nini kila anayepewa Kipaza sauti anailalamikia Serikali na Watendaji kuwa ni Madhalimu?

Kwa nini Mwenezi wa CCM hapokelewi na Mabango ya kuisifia na kuipongeza CCM?

Wote, wote kabisa, wanawalaani Watendaji wa Chama na Serikali.

Babati, Jeshi la Polisi linamvunjia Nyumba Mwananchi bila "Demolition Order" ya Mahakama, mithili ya Polisi wa enzi za Makaburu, Afrika Kusini.

Paul Makonda anauthibitushia Ulimwengu kuwa "Tanzania is a Failed State"

Serikali ya CCM kazi yake ni kudhulumu na kunyanyasa Wananchi.

Katika macho ya Wananchi, Serikali imepoteza uhalali wa kutawala.

Wananchi wanataka Samia aondoke, Makonda atawale.
 
Paul Makonda ni Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi. Bila kuathiri Muundo wa Utumishi Serikalini, yeye Makonda ni Kiongozi wa Chama Cha Siasa Kama ilivyo kwa Chadema...
Waswahili wanasema ukishaanza kula nyama ya binadamu uwezi kuiacha.

Tunamuiliza Makonda yu wapi Ben Saanane?
 
NCHI HII HAISHEMU KATIBA WALA SHERIA ZA UTUMISHI KUNA SIKU MAKONDA ATAMFUKUZA KAZI WAZIRI MKUU

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app

Sitashangaa siku akihoji Mamlaka ya Rais ambaye ni Mwenyekiti wa CCM.

Anachokifanya Makonda kuhoji watumishi wa umma hadharani ni sawa na kuhoji Mamlaka ya Kiongozi Mkuu wa Serikali amabaye ndie Rais na Mwenyekiti wa CCM.

Yaani hii ni kuidhalilisha Serikali.

Kwa kifupi Makonda anatemgeneza Umaarufu Binafsi, kuna siku atachukua Fomu ya kugombea cheo kikuu
 
WaTanzania wanaamini ili shida zikuishe ambatana na mwenye tabia kama za yule malaika aliyetupwa duniani na Mungu alimwambia walio wako watakufuata.
 
Ni kweli, kwa umati uliojitokeza Kahama kuja kumiliki, mimi mpaka nimeovopa!, amepolelewa kama Masiha alivyopokelewa ile siku anaingia Jerusalem, halafu siku chache baadaye ndio ilawa vile!.
Ukweli ni kwamba, wananchi wana shida na matatizo mengi yanayohitaji utatuzi. Na wanaamini kwamba serikali ina nafasi kubwa na muhimu ktk kutatua shida zao. Kinachohitajika ni kiongozi atakayewasikiliza shida zao, na wakamwamini kuwa ana nia nzuri ya kutaka kuwaondolea matatizo yao. Kuna viongozi wameshajiondoa kwenye kundi la kuaminiwa, ndiyo maana wakienda kwa wananchi hawapati mtu.
Kwa sasa Makonda anaonekana ni miongoni mwa hao wanaoaminiwa na wananchi, kueleza matatizo yao, na kutegemea kwamba atawasaidia kupata ufumbuzi.
 
Back
Top Bottom