Makonda: Ghalib usinilazimishe kusema uozo wako, achia mali yangu. Walioko nyuma yako nawajua

Pia gsm nae awe makini siasa Ni mchezo fln HV utashanga atakuja kuibuka rais akampenda makonda akamrudisha makonda kwenye power hkn rang wataacha kuona watakimbia nnchi hutujui Nani anakuja kuwa rais ikitokea sukumagang Tena oooh sipati picha hicho kipigo watakachakipata team msoga hawatawalipa warudie

So natoa Rai gsm acha kuwachezea wanasiasa hiki unachotaka kufanya utashinda ila huna uhakika Kam utashninda milel

It's not over untill it's over

Wafanyabiashara ndio wanasiasa wenyewe MKUU.
Sijui Kama unajua unachokiongea.

Siasa ni biashara,
 
Miaka miwili nyuma makonda alikuwa na cheo Cha wazir mkuu kwa.kofia.ya ukuu.wa.mkoa had nape.wazir wa habari alifukuzwa Kaz na makonda

Makonda alikuwa mhimili uliojichimbia chini lakn bahat mbaya miziz chin Imeoza na watu wameshajua hayo toka mwez mach 2021 kilichobaki n kudondoka

SOMO LENYE MWANZO HALIKOSI MWISHO

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Kheri upoteze hirizi kuliko kufiwa na mganga
 
View attachment 2148028
Wakati Wakili wa mfanyabiashara maarufu nchini, Ghalib Said Mohamed (GSM), Alex Mgongolwa ameweka wazi vielelezo vya umiliki wa eneo kiwanja namba 60 lililopo Regent Estate Kinondoni jijini hapa, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amemtaka mfanyabiashara huyo kumwachia mali yake.

Mzozo wa kiwanja hicho umeibuka hivi karibuni, ambapo Makonda ameonekana katika video iliyorushwa kwenye mitandao ya kijamii akisisitiza kuwa eneo hilo ni lake.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumamosi Machi 12, 2022 jijini hapa Wakili Mgongolwa amemtaka mtu ambaye hakumtaja kwa jina, kuweka wazi vielelezo alivyonavyo vya umiliki wa eneo hilo na vielelezo kutoka Wizara ya Ardhi vinavyompa uhalali wa kulimiliki.

Hata hivyo, Makonda alipotafutwa kwa simu leo, amejibu kwa ujumbe wa WhatsApp, akisema; “GSM usinilazimishe kusema uozo wako achia mali yangu. Walioko nyuma yako nawajua.”

Kama hiyo haitoshi, katika ukurasa wake wa Instagram, Makonda aliweka video ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka ambayo pamoja na mengine alieleza haja ya kutaka Jeshi la Polisi kuchunguzwa, kisha akaweka ujumbe:

“Naunga mkono hoja ya Kamati Kuu, ya kuchunguza mwenendo wa baadhi ya maafisa wa Jeshi la Polisi, wanaolipaka tope Jeshi la Jolisi kwa kuwalinda wafanyabiashara MATAPELI wanaodhulumu mali za watu. Naomba tuanze na Dar es salaam na mimi Paul Makonda niko tayari kutoa ushirikianao.”

Madai ya GSM
Akifafanua zaidi kuhusu umiliki wa ardhi hiyo, Wakili Mgongolwa amesema, mteja wake Ghalib Said Mohamed alinunua ardhi wilaya ya Kinondoni, eneo la Regent Estate plot no. 60, title no. 186153/60, kwa lengo la ujenzi wa makazi Novemba 21, 2006."

Vilevile, Mgongolwa amesema Septemba 2017, mteja wake aliingia mkataba na kampuni ya ujenzi iitwayo Group Six International (Contract Class One) kwa ajili ya ujenzi wa eneo hilo wenye thamani ya Sh640 milioni.

"Ghalib aliomba kibali cha ujenzi na manispaa ya Kinondoni walitoa kibali hicho Oktoba 16, 2017 chenye kumbukumbu namba 00020032 kwa Ghalib Said Mohammed kwa ajili ya ujenzi eneo hilo," amesema.

Ameongeza kuwa baada ya kibali hicho kutoka, Group Six walianza ujenzi na walipeleka malipo ya awali ya ujenzi Januari 31, 2018 huku mteja wake huyo akitekeleza sehemu ya mkataba kwa kulipa kiasi cha Sh51.92 milioni, malipo ambayo yana kithibitisho kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Kuhusu mteja wake kuwa na uhusiano wa karibu na mlalamikaji, alisema, "mteja wangu na mtu ambaye kwenye mitandao amekuwa akizungumza kwamba anamiliki eneo hilo, mteja wangu katika kipindi anachozungumza huyo mtu cha mwaka 2012 alikuwa hamfahamu kabisa huyo mtu."

"Mimi leo nathibitisha uhalali wa miliki, unaweza ukawa na uhusiano na mtu lakini sio wa kibiashara wa kuuziana na kuhamishiana miliki licha ya kuingia katika makubaliano ya kuhamishiana miliki,"

Mgongolwa alisema kufahamiana na mtu ni jambo lingine na miliki ni jambo lingine, hivyo ushahidi wa vielelezo kisheria unakingwa na vielelezo hivyo, ambaye anasema ni eneo lake aweke wazi vielelezo vya kisheria.

"Tunatoa changamoto kwa mtu yoyote yule aje akinzane na vielelezo vyetu, huu ni ujenzi kwa mujibu wa mkataba na haujasimamiwa na mjomba au shangazi," amesema Mgongolwa.

Alisema yeye yuko radhi kumsikiliza ili wakapambane, alisema kama kuna mtu anadhani anayo haki katika umiliki huo, lakini kwa sasa hawatafanya chochote na endapo ataendelea na matukio hayo hivyo basi ngazi za kisheria zitafuatwa.

"Hata tunaondokana na hisia tunaenda na uhalisia, yoyote yule anayesema aridhi ni ya kwake iwe kimahusiano au lah, aje na vielelezo kwetu, mtu mwenye dhana tofauti milango ya kimahakama iko wazi, ila kwa sasa hawatakwenda mahakamani," amesema Mgongolwa na kuongeza kuwa wajibu wangu kama mwanasheria ni kuthibitisha umiliki halali kwa mteja wangu.

"Hatua tutakazozichukua kuanzia sasa itategemea na matukio ambayo yatafuata kwani ndiyo yatatupa mwongozo wa nini tukifanye, ikitokea hatua ya kwenda mahakamani tutakwenda, ikitokea kuangalia ngazi nyingine tutalipeleka kwa kuwa maelekezo yetu yako wazi tunatakiwa kulinda haki ya teja wetu sambamba na jina lake," amesema.

Source: Mwananchi

Kwanini Makonda asiende mahakamani kama ana hoja!
 
Nimeamini jamaa ni "Zero Brain", vyote kwa jinsi alivyomilikishwa mali na GSM pamoja na anavyolihandle hili suala..

Kama sheria ipo upande wake, haina haja ya "kupiga mikwara" au "kutunishiana misuli" handarani sababu mahakama ipo..

Nauona mwisho mbaya sana kwake utakaosababishwa na "ukilaza" wake..
Mtu anakujengea nyumba halafu documents anakaa nazo, unaona ni sawa tu! Zero brain indeed!
 
Uoga huo. Nadhan kila mtu anapaswa kudai haki yake na kutetea hadhi yake bila kujali anayekandamiza ni mwanasiasa au sio mwanasiasa. Halafu sukuma gang unadhan ni kitu gani? Una uhakika gani kuwa hao unaowaita sukuma gang ni maswahiba wa Makonda?
Pia gsm nae awe makini siasa Ni mchezo fln HV utashanga atakuja kuibuka rais akampenda makonda akamrudisha makonda kwenye power hkn rang wataacha kuona watakimbia nnchi hutujui Nani anakuja kuwa rais ikitokea sukumagang Tena oooh sipati picha hicho kipigo watakachakipata team msoga hawatawalipa warudie

So natoa Rai gsm acha kuwachezea wanasiasa hiki unachotaka kufanya utashinda ila huna uhakika Kam utashninda milel

It's not over untill it's over
 
Hoja ya msingi ni nani mmiliki wa eneo. Makonda apeleke vielelezo amuaibishe huyu GSM
ETI LEO GHARIB ANAKANA KUMFAHAMU MAKONDA ???

NDUGU WATANZANIA GHARIB NA MAKONDA NI KAMA MWIZI NA MFICHA MALI ZA WIZI WOTE NI MAJAMBAZI.HALAFU NINAJIULIZA INTEREST YA MANGE KIMAMBI UPANDE WA GSM AMEKUWA MTETEZI WAKE MKUBWA SANA.HILI JAMBO LINAFIKIRISHA SANA.

WATANZANIA TUNA AKILI ZETU HUU SI WAKATI WAKUSHIKANA AKILI.

KATIKA HILI KILA MMOJA ALE MSHAHARA WAKE HAKUNA MALAIKA HAPA BALI KUNA VISASI VYA AWAMU YA TANO,MWENYE KUHISI NI MUDA WAKE WA KULIPIZA NA ANAEHUKUMIWA KWA HISTORIA YAKE.

IUNDWE TUME HURU WOTE WAENDE JELA
 
Makonda kumbuka kuwa yatima hadeki, ulifanya kazi na kujimilikisha mali kwa mgongo wa jiwe. Sasa mambo yamebadilika mzee
 
Kwa hiyo kauli yake nchi zenye akili angetiwa mbaroni kwa "obstruction of justice"
 
Bila bila? Wakati amenisurika kupigwa Bomba, na hana mamlaka ya kuambia askari wafungue kesi yoyote, now toothless.

R.I.P Mkurugenzi wa Jiji ndugu Kabwe, jamaa anarostiwa akiwa mzima
Aliyekuwa mkurugenzi wa JiJi ilikuwaje ? Tujuee apo
 
Makonda anaongea uozo wa GSM 🤣? subiri waje wale wote aliowadhulumu, kuwateka etc na watakao mchoma ni wale wale alioshirikiana nao kufanya uharamia wake ,huyu alikuwa na akili kama ya Sabaya tuu ila watamshughulikia tuu na wameshaanza maana kisharushiwa kesi na sasa nyumba, kweli ubaya haulipi
 
View attachment 2148028
Wakati Wakili wa mfanyabiashara maarufu nchini, Ghalib Said Mohamed (GSM), Alex Mgongolwa ameweka wazi vielelezo vya umiliki wa eneo kiwanja namba 60 lililopo Regent Estate Kinondoni jijini hapa, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amemtaka mfanyabiashara huyo kumwachia mali yake.

Mzozo wa kiwanja hicho umeibuka hivi karibuni, ambapo Makonda ameonekana katika video iliyorushwa kwenye mitandao ya kijamii akisisitiza kuwa eneo hilo ni lake.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumamosi Machi 12, 2022 jijini hapa Wakili Mgongolwa amemtaka mtu ambaye hakumtaja kwa jina, kuweka wazi vielelezo alivyonavyo vya umiliki wa eneo hilo na vielelezo kutoka Wizara ya Ardhi vinavyompa uhalali wa kulimiliki.

Hata hivyo, Makonda alipotafutwa kwa simu leo, amejibu kwa ujumbe wa WhatsApp, akisema; “GSM usinilazimishe kusema uozo wako achia mali yangu. Walioko nyuma yako nawajua.”

Kama hiyo haitoshi, katika ukurasa wake wa Instagram, Makonda aliweka video ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka ambayo pamoja na mengine alieleza haja ya kutaka Jeshi la Polisi kuchunguzwa, kisha akaweka ujumbe:

“Naunga mkono hoja ya Kamati Kuu, ya kuchunguza mwenendo wa baadhi ya maafisa wa Jeshi la Polisi, wanaolipaka tope Jeshi la Jolisi kwa kuwalinda wafanyabiashara MATAPELI wanaodhulumu mali za watu. Naomba tuanze na Dar es salaam na mimi Paul Makonda niko tayari kutoa ushirikianao.”

Madai ya GSM
Akifafanua zaidi kuhusu umiliki wa ardhi hiyo, Wakili Mgongolwa amesema, mteja wake Ghalib Said Mohamed alinunua ardhi wilaya ya Kinondoni, eneo la Regent Estate plot no. 60, title no. 186153/60, kwa lengo la ujenzi wa makazi Novemba 21, 2006."

Vilevile, Mgongolwa amesema Septemba 2017, mteja wake aliingia mkataba na kampuni ya ujenzi iitwayo Group Six International (Contract Class One) kwa ajili ya ujenzi wa eneo hilo wenye thamani ya Sh640 milioni.

"Ghalib aliomba kibali cha ujenzi na manispaa ya Kinondoni walitoa kibali hicho Oktoba 16, 2017 chenye kumbukumbu namba 00020032 kwa Ghalib Said Mohammed kwa ajili ya ujenzi eneo hilo," amesema.

Ameongeza kuwa baada ya kibali hicho kutoka, Group Six walianza ujenzi na walipeleka malipo ya awali ya ujenzi Januari 31, 2018 huku mteja wake huyo akitekeleza sehemu ya mkataba kwa kulipa kiasi cha Sh51.92 milioni, malipo ambayo yana kithibitisho kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Kuhusu mteja wake kuwa na uhusiano wa karibu na mlalamikaji, alisema, "mteja wangu na mtu ambaye kwenye mitandao amekuwa akizungumza kwamba anamiliki eneo hilo, mteja wangu katika kipindi anachozungumza huyo mtu cha mwaka 2012 alikuwa hamfahamu kabisa huyo mtu."

"Mimi leo nathibitisha uhalali wa miliki, unaweza ukawa na uhusiano na mtu lakini sio wa kibiashara wa kuuziana na kuhamishiana miliki licha ya kuingia katika makubaliano ya kuhamishiana miliki,"

Mgongolwa alisema kufahamiana na mtu ni jambo lingine na miliki ni jambo lingine, hivyo ushahidi wa vielelezo kisheria unakingwa na vielelezo hivyo, ambaye anasema ni eneo lake aweke wazi vielelezo vya kisheria.

"Tunatoa changamoto kwa mtu yoyote yule aje akinzane na vielelezo vyetu, huu ni ujenzi kwa mujibu wa mkataba na haujasimamiwa na mjomba au shangazi," amesema Mgongolwa.

Alisema yeye yuko radhi kumsikiliza ili wakapambane, alisema kama kuna mtu anadhani anayo haki katika umiliki huo, lakini kwa sasa hawatafanya chochote na endapo ataendelea na matukio hayo hivyo basi ngazi za kisheria zitafuatwa.

"Hata tunaondokana na hisia tunaenda na uhalisia, yoyote yule anayesema aridhi ni ya kwake iwe kimahusiano au lah, aje na vielelezo kwetu, mtu mwenye dhana tofauti milango ya kimahakama iko wazi, ila kwa sasa hawatakwenda mahakamani," amesema Mgongolwa na kuongeza kuwa wajibu wangu kama mwanasheria ni kuthibitisha umiliki halali kwa mteja wangu.

"Hatua tutakazozichukua kuanzia sasa itategemea na matukio ambayo yatafuata kwani ndiyo yatatupa mwongozo wa nini tukifanye, ikitokea hatua ya kwenda mahakamani tutakwenda, ikitokea kuangalia ngazi nyingine tutalipeleka kwa kuwa maelekezo yetu yako wazi tunatakiwa kulinda haki ya teja wetu sambamba na jina lake," amesema.

Source: Mwananchi
Uozo wa Ghalib hausiani na wewe kupora kiwanja.
Kama ulikua unaujua uozo waks ulipaswa kisheria ukaseme kwa vyombo vya dola.
Wewe Makonda kukaa kimya ni makosa kisheria.
Kaogeleew kwenye huo uozo ufurahi.
Rudisha kiwanja cha watu nadala ya kutoa vitisho
 
Jamani hebu tujaribu kujiuliza swali ivi yule kiongoz wa malaika alietuaminisha yeye ni mzalendo namba moja hakua anajua lolote juu ya huyu mwanae? Kama ndivyo u wap usafi wake ikiwa alifumbia macho anaowapenda? Double standard ya kukemea rushwa ndio alikua anajikosha nayo??
 
Back
Top Bottom