Makomandoo wa Bongo

Makomandoo wa Bongo

Huyu hata mie nilimsikia kuwa alichanganyikiwa kwenye mafunzo ya Kikomandoo huko Izrael. Ila wengi wanamkubali kuwa alikuwa na uwezo wa kumuona mtu kwa nusu sekunde na atakukumbuka.

Kuna vijana waliiba mahindi na kwenda kuchoma msituni. Wengine walikaa doria wakiangalia kama kuna mtu anakuja. Walipokuja kumuona huyo, wakapotea msituni na kumuacha peke yake. Aliitisha kambi nzima ya jeshi na kuwachoropoa mmoja mmoja. Ila mwisho akajisifu kuwa kama Wanajeshi basi kashatengeneza maana jinsi vijana waliyoondoka hapo na kwa mwendo wa chui na kupotelea vichakani, hadi alijisikia raha. Kwa sababu hiyo akawaachia huku akiwaambia kuwa wasirudie tena maana yeye siku zote yupo hatua moja mbele ya KURUTA/SERVICE MAN.
Ah ah ah ah ah, huyo ndio Mtono na wengine kama yeye ambao watu wa kawaida hawawajui au hawaelewi nini maana ya kuwa Commando (mwanajeshi). Watu wengi sana wameathirika na hizi filamu za kina commando John, Rambo n.k. Wanashindwa kutofautosha ukweli na maigizo.

Tanzania imepeleka askali wengi sana nje kwenye mafunzo ya kijeshi, na kiitelejinsia... Vijana wengi wa zamani walipelekwa Israel (Japokuwa Mwalimu alisema hatuna uhusiano nayo), Cuba, Bulgaria, Canada, Urusi, UK n.k. Naweza kusema jeshi la Tanzania ni katika jeshi bora sana katika majeshi ya Afika Mashariki na kati na haswa jeshi la Miguu.

Tumepeleka wanajeshi nchi nyingi kusaidia kuondoa madarakani au kutuliza amani kwa mtutu... Kusini mwa Afrika wanautambua mchango wa jeshi letu, haswa kule Msumbiji, Angola, Namibia, Botswana, vile vile tumepeleka majeshi Burundi, Rwanda, Comoro, Congo zote mbili, Liberia, Nigeria, Seychelles, Sierra Leone. Na kote uko jeshi letu lilifanikiwa vizuri sana... Tena linasifika kuwa ni jeshi lenye nidhamu ya hali ya juu sana na haswa kwa raiya wa hizo nchi. Nakumbuka kisa kimoja cha Waganda, haswa wale walioshuhudia vita vya Kagera (Mtukula), wanasifia wanajeshi wa TZ kuwa wakikuona kama wewe umewazidi umri basi watakuhamkia kwa Shikamoo na kisha ndio watakuuliza wapi askari wa Amini... Na kama ni kijana watakusalimia kwa Habari yako... Tofauti na walivyokuwa Askari wa majeshi mengine, na hayo si uko tu hata uko kwengine wanakozungumza Kiswahili.

Sasa wanao dharau wanajeshi wetu na hususani hao Comandos, ajue kuwa hafahamu lolote linalo endelea humo ndani ya jeshi la Tanzania. Kilichokuwa kikionyeshwa pale uwanja wa Taifa ni moja ya mazoezi ya viungo tu, na wala si mbinu za medani.

Kuna mafunzo mengi sana sana, ambayo hayafai kuonyeshwa kwa raiya wa kawaida kama mimi na wewe, kwa sababu yakionyeshwa, ni sawa na kuwafundisha waharifu...

Kwa ufupi wawaulize waliopitia kozi za kijeshi kule mufindi au Arusha (Monduli) watawaeleza vema.
 
Acha dharau na kujifanya unajua kumbe hujui lolote...! Zile ni demo za kuonesha utimamu wa mwili..,
Hzo shotokan unazoongelea ni ushuzi tu kwa combinations za commando.., hawapigani aina moja ya martial art.., ila kwa ujinga wa baadhi ya watu wanafkiri kinachooneshwa pale ndo final.., style yako ya mapigano ndo ita-determine combination ya commando akupige vp...,
hakuna pigano la kiraia utaweza mpiga commando.., kama huamn jarb, na kama unajisifu una black belt ya karate utatandikwa ngumi moja iloshiba inayopiga push-up 500 daily, ikitua kwny koo utalia kama mtoto kanyimwa jojo, mamaee

mkuu umemaliza niliyotaka kusema!huyu ni kipele tu alitaka aonekane anajua!
 
Nimeipenda hii ANALYsis
tatizo la majina kuwa universal ndio hili....
mrisho ngassa na lionel messi wote ni WASHAMBULIAJI
vodacom premier ligue na barclays premier ligue zote ni LIGI KUU ZA SOKA
umoja wa afrika na jumuia ya ulaya zote ni REGIONAL INTEGRATION BLOC
............kweli?
sasa jijibu mwenyewe kama wa kwetu na wa kwao wapaswa wote kuitwa MAKOMANDOO
 
X-paster
nidhamu ipi?
Mbona wanajesh wetu wamekua wakiwapga raia?wanakamatwa na bhang,pembe za ndovu na wiz wa kutumia silaha!wanahusishwa na wiz wa UBUNGO MATAA
 
Jamani nyie acheni kuongea mambo ya historia , ndio jeshi letu limewahi kushiriki operesheni mbalimbali na vita nchi nyingine lakini ni zamani na mbinu zilizotumika kipindi hicho ni tofauti sana na sasa hivi kitekonologia na mambo mengine .

Kwenye historia hata rumi ilikuwa na jeshi bora zaidi liliweza kuteka eneo kubwa leo wapi rumi ? Miaka hiyo wamarekani walikuwa na uwezo wa kuipiga na kuikalia nchi yoyote lakini ona ndege yao ilivyoangushwa Iran Juzi hata uchina iliwahi kuangusha ndege zake za kijasusi .

Je sisi tunafanyiwa ujasusi mara ngapi na kupigwa picha mara ngapi kutokea Juu na sehemu zingine kama kwenye mitandao jamii na forums kama hizi ? tumejiandaaje maana hizi zote ni silaha za kivita .

Juzi hapa raisi wa zamani wa marekani amefika mawasiliano karibu yote hayakuwa vizuri mpaka leo hii baadhi ya huduma zinasumbua za mawasiliano je tumejiandaaje na hujuma au visa kama hivi ?

Komandoo haswa komando units kama zile zinazopambana kwenye uokoaji na shuguli nyingine zinahitaji teknologia za mawasiliano za hali ya juu ili ziweze kutekeleza kazi na wajibu wao vizuri , angalia ile Unit iliyomuuwa osama Bin laden iliandaliwa kwa kipindi fulani na kuwa maalumu kwa ajili ya operesheni hiyo tu na walikuwa wnafuatiliwa live toka ikulu ya marekani na idara nyingine za jeshi la nchi hiyo .

Juzi hapa akaunti ya twitter ya mke wa raisi iliingiliwa ikachukuwa zaidi ya masaa 10 kuweza kurekebisha lakini mchezaji mmoja wa Manchester united alipiga picha ikulu ya marekani na kuweka kwenye twiter yake ikaondolewa ndani ya Dakika kadhaa .
 
Kaka ngoja nikwambie kitu, ile kazi za kuokoa watu baharini komandoo haendi wanaenda kikosi cha waokoaji, kazi ya komandoo ni kushughulikia mahala ambapo kuna kikwazo cha hali ya juu na kusaidia kutengeneza njia za kusogea mbele! upo hapo?

Imagine, tukipeleka wakufunzi (wanajeshi) wengi sana kwa mpigo kwenye mafunzo ya kikomandoo na wakafuzu wote jeshi litakuwa limesimama katika hali ya uimara kabisa!

Mimi nawaamini wale makomandoo kwamba wako fit tusiwadharau, wamefanya pale ambapo ni salama kwetu, tukionesha yaliyo makuu ni sawa na kuanika udhaifu wetu kwa maadui zetu!
 
Kuna mambo mengi ya kufanya zaidi haswa kwenye zama hizi za teknologia , msimamo wangu utabaki ule ule kuvunja mawe na matofali sio maonyesho si miaka yote wanafanya hivyo ? toka tumepata uhuru ? Kanda yetu inakabiliwa na tishio la ugaidi sasa hivi mbona hatujaona UNIT KOMANDO ya kupambana na ugaidi kwenye maonyesho hayo ? na hata awareness nyingine kwa watu walioenda kwenye maonyesho hayo ?
 
COMMANDO wa israel anaweza ruka toka kwenye ndege bila kutumia parachute,na huku akitumia breathing techniques za yin and yang anaweza float hewani for sometime bila parachute kabla aja hit the ground

Acha uongo wewe,hakuna komando duniani mwenye uwezo huo wa kuruka toka kwenye ndege bila parachute. Ni lazima kutumia parachute ili uweze kutua katika landing point kwali bila hilo utatua kama tofali na utakufa
 
Mimi nimeshuhudia komandoo wa kiisrael alizunguukwa na Makomandoo wa Hizbullah, alijigeuza kuku ili akwepe ! Hata hivyo walimkamata na kumfanya kitoweo!

Aa! Wapi wewe? Hamna kitu hapa jaribu wakati mwingine kuwa fair kwenye mambo ya msingi bila kuweka chuki wala udini.
 
Kuna mambo mengi ya kufanya zaidi haswa kwenye zama hizi za teknologia , msimamo wangu utabaki ule ule kuvunja mawe na matofali sio maonyesho si miaka yote wanafanya hivyo ? toka tumepata uhuru ? Kanda yetu inakabiliwa na tishio la ugaidi sasa hivi mbona hatujaona UNIT KOMANDO ya kupambana na ugaidi kwenye maonyesho hayo ? na hata awareness nyingine kwa watu walioenda kwenye maonyesho hayo ?
Shy, nakubaliana na wewe. Haitoshi kuwa na makomandoo hodari na waliofunzika lakini kama hawana vitendea kazi bora vyenye kuendana na wakati kiteknolojia, mafunzo yao yanakuwa na manufaa kidogo sana. Wale wa jana wameonesha wako imara, wakakamavu na wana maarifa ya kutosha, lakini je, hiyo inatosha bila vifaa vya kisasa kama wale wa marekani na israeli? Kwa dunia ya leo vifaa vya kisasa vina nafasi kubwa sana katika kufanikisha kazi zao.
 
Jamani eeeh! Kuwa na vifaa vya kisasa havikuhakikishii ushindi kama hao askari hawana hari ya kupigana, ndio maana wanasema human intelligence ndio inayotakiwa kuliko hii ya kutumia artificial intelligence...!

Na hata hizo nchi zilizoendelea kama US na Japani tumeshuhudia zikipata Natural disasters na zimeshindwa kuwaokoa raiya zake. Kama mnakumbuka mwaka 2005 uko Marekani majimbo ya Florida, Louisiana, Mississippi na Alabama, yalipata misukosuko ya Kimbunga cha Katrina na vifo vikatokea na wengi wakashindwa kuokolewa japokuwa nchi ina vifaa bora kabisa na vya kisasa vya hali ya hewa, na ikasemekana kuwa baadhi ya raiya waliachwa kufa kwa makusudi kabisa kwa sababu ni wenye asili ya Afrika... 2011 tornado ikapiga tena na ikaleta maafa...

Japan ni wazuri wa teknolojia, lakini kila leo wanakumbwa na matetemeko na watu wanapoteza uhai...
 
Hatujawahi pata inshu hapa bongo ya kuwatumia tuone kama kweli wako fii kama wenzao huko nje. But I know watakuwa fit coz kama ni training wanatapa kama hiyo ya kwa Obama. So let be assured wako fit.

Huna kumbukumbu, ulikua hujazaliwa au hufuatiliagi mambo yanavyokwebda.
Komandoo Hatib Ghandhi "Mac Ghee" aliekua akitafutwa kwa kosa la kutaka kupindua Serikali ya Nyerere alilazimika kukwepa risasi za akina Mabere Marando enzi hizo akiwa usalama wa Taifa kwa mtindo wa "Samasoti" akibenuka juu ya magari pale Kinondoni Mkwajuni!!
Uliza kwa wanaojua au hata tafuta simulizi au vitabu vya huo uhaini.
Although kina Rambo wamezidisha uongo mwingi kama wa makomandoo watano kupigana na Jeshi la zima la Wa-Vietnam, but kibongobongo hatuwezi kukosa wawili watatu.
 
Wakuu nimecheki clip kwa michuzi, kwenye ile segment ya kuvunja vitu, I rest my case.
Nimewakubali.

Hilo tofali limetengenezwa maalum kwa ajili ya hiyo event,
Pengine hata ni la mchanga tupu bila Cement!!!!
Na hizo mbao unajua aina yake.
Nakubaliana na mdau mmoja hapo juu kua siku hizi vita haipiganwi kwa kushikana shikana au kuonana ana kwa ana kama series za kina Jumong na Taesso!!
Watu wanatumia "auto pilot" ambazo zina sensa ya kugundua ujio wa kitu cha hatari kama "missile bomb" na kukikwepa
 
Huna kumbukumbu, ulikua hujazaliwa au hufuatiliagi mambo yanavyokwebda.
Komandoo Hatib Ghandhi "Mac Ghee" aliekua akitafutwa kwa kosa la kutaka kupindua Serikali ya Nyerere alilazimika kukwepa risasi za akina Mabere Marando enzi hizo akiwa usalama wa Taifa kwa mtindo wa "Samasoti" akibenuka juu ya magari pale Kinondoni Mkwajuni!!
Uliza kwa wanaojua au hata tafuta simulizi au vitabu vya huo uhaini.
Although kina Rambo wamezidisha uongo mwingi kama wa makomandoo watano kupigana na Jeshi la zima la Wa-Vietnam, but kibongobongo hatuwezi kukosa wawili watatu.
Alikuwa anaitwa 'Tamim'
 
Alikuwa anaitwa 'Tamim'

Yeah nimekumbuka mkuu!!
But walikua kundi moja na Mac Ghee na mwanzao Kadeghe kama sikosei.
Ingawa si kwa kuwafananisha kwa kiwango cha uongo wa kina Schwarzenneger au War-Bus, but wale hawakua Makomandoo?
 
Hilo tofali limetengenezwa maalum kwa ajili ya hiyo event,
Pengine hata ni la mchanga tupu bila Cement!!!!
Na hizo mbao unajua aina yake.
Nakubaliana na mdau mmoja hapo juu kua siku hizi vita haipiganwi kwa kushikana shikana au kuonana ana kwa ana kama series za kina Jumong na Taesso!!
Watu wanatumia "auto pilot" ambazo zina sensa ya kugundua ujio wa kitu cha hatari kama "missile bomb" na kukikwepa
Hivi mfupa wako wa mkono ni mgumu kupita lile tofali ? Kwa teke lake moja kupitia mazoezi yale anaweza kuvunja mbavu zako ngapi? Hao wanaopigana kwa ndege ambazo hazina rubani bado wanahitaji kuingia uwanja wa mapambano. Ndege bila rubani haiteki eneo! Pia dawa ya ni suicide bombers na ma roadside bombs ! And it works, mpaka leo Afghan hakuna achievement yeyote.
 
Yeah nimekumbuka mkuu!!
But walikua kundi moja na Mac Ghee na mwanzao Kadeghe kama sikosei.
Ingawa si kwa kuwafananisha kwa kiwango cha uongo wa kina Schwarzenneger au War-Bus, but wale hawakua Makomandoo?
Tamim alikuwa Komandoo na aliasi kwa mujibu wa madai ya wabaya wake, usalama wa taifa. Alitoroka jeshi baada vita vya kagera na alikimbilia Kenya, alirudi kuungana na makampten waliopanga kufanya mapinduzi, akina Hans Pope, Maganga na Mac Ghee.
 
Tumeshndwaje kuwatumia kwenye ajal ya meli ya NUNGWI?
Hivi huwezi kupambanua tofauti ya muokoaji na mpiganaji ? Huwezi kuona tofauti ya Askari Magereza na Polisi? Soma soma humu upate ufahamu zaidi!
 
Back
Top Bottom