The Mediator!
Ungeweka rejea ya maneno aliyotamka Werema ingekuwa na mvuto wa pekee!
Kwa ambao hawakubahatika kumsikia Werema habari hii inakuwa kizungumkuti!
Nampongeza sa spika wa bunge letu tukufu Mh Anne Makinda kwa kulitendea bunge haki japo hata kwa mara chache sana.Jana mama huyu alionyesha ujasiri wa hali ya juu sana pale alipomueleza bila kupindisha maneno kuwa Mwanasheria mkuu wa serikali amelikosea bunge hivyo anapaswa kufuta kauli ya ke kama alivyodaiwa na naibu kiongozi wa kambi ya upinzani Mh Kabwe Zuberi Zitto.
Hapa ndipo nilipoona kumbe kama Mh Makinda akiamua anaweza sana.Kwa hili hatuna budi kumpongeza ingawa ni kazi yake kufanya hivyo kwani bunge haliongozwi kama alivyokuwa akifanya awali.
Kiukweli Mwanasheria mkuu wa serikali Mh Fredrick Werema amepotoka sana maadili.Yaani anafikia kuwatusi wabunge ndani ya bunge letu tukufu.Hapa inabidi tujiulize hivi huyu muheshimiwa anajua kilichompeleka bungeni?Ameidhalilisha sana ofisi yake kwani imeonekana kana kwamba ofisi yake imejawa na watu wengi wa aina yake.
Unajua bungeni ni sehemu ya kutungia sheria za nchi na pia ni sehemu ya kuwatetea wananchi kwa kero walizonazo dhidi ya serikali yao.Sasa si vizuri kuwakashifu waheshimiwa wabunge ambao wanawakilisha mawazo ya wananchi.Kufanya hivyo ni sawa na kuwadharau wananchi.Kweli mh Werema inabidi aombe radhi kwa kuwatukana wananchi kwa maneno yake yasiyo na hata chembe ya busara.Hapa kwa mtazamo wangu rais Kikwete amechemka sana kumteua huyu gwiji wa tasnia ya sheria.
Mwisho napenda kuwaasa waheshimiwa wabunge hasa wa chama tawala nikimaanisha CCM wawe na tabia ya uzalendo wa nchi yetu kwani chama hakitawasaidia sana zaidi ya kujinufaisha wao na pindi muda wao utakapopita asi taifa kama taifa litakuwa limeangamia kwa uzembe wao.
Mungu ibariki Tanzania.

Tehe teh teh!Jana alionekana kama stress zimepungua, inawezekana alikuwa na appointment mahali.
Wakati wa wa jioni jana wabunge wakichangia finance bill 2011 Mh. Anne Makinda alifanya kazi bila upendeleo wowote pale alipowanyamazisha bila kuangalia usoni wabunge dhalimu wa CC-Magamba akiwemo , Ole sendeka, Kingwangala wa Nzega na wengineo waliokuwa wanakatiza wenzao wa CDM kutaka mwongozo wa spika.
Jana Spika hakuwa akimwangalia mtu usoni kwani ilikuwa ni kanyaga twende iliowaacha wabunge wa Kijani waliozoea kubebwa mgongoni wakigaragara chini huku akiweka maslahi ya Taifa mbele. Kwa namna hii basi atakuwa amemshinda hata Mzee wa Kasi na Viwango"SIX"
Wakati mwingine nahisi labda mzimu wa shutuma dhidi yake ambazo Tindu lissu amekuwa akishupalia umeanza kumfanya anaweweseka.