Makinda na Bunge la kelele za taarifa, mwongozo.

Huyu mama kilaza sana. Kwa alichofanya anataka kumaanisha jambo lolote linalohusu Nyamongo lisijadiliwe bungeni kisa tu kina Tundu walishtakiwa wakiwa huko Nyamongo. Huyu mama ni fisadi mbaya sana. Watu wanauwa raia alafu hataki wawajibishwe. Kwa kifupi huyu mama ni MPUMBAVU SANA!!
 
Hii ya Spika Anne Makinda utendaji wake wa mashaka kujadiliwa kwa kina ndiyo inatakiwa na ikiwezekana apewe mbinyo ajiuzulu baada ya madudu kuwekwa hadharani na kamati hiyo. CHADEMA kwa kweli ni kiboko ya CCM maana kama CCM wakileta za kuleta kutumia wingi wao Bungeni kumtetea Spika Makinda basi CHADEMA leteni kesi kwa wananchi tuamue kama kawaida yetu.
 
Maneno yanayosemwa mara kwa mara kwa jazba na Anne Makinda ni ushahidi tosha kuwa hawezi kazi yake. Cheo cha uspika wa Bunge la Tanzania kimewahi kushikwa na watu tofauti, kuanzia Chief Adam Sapi Mkwawa, Chief Erasto Mang'enya kwa muda mfupi, akarudi tena Chief Mkwawa ambaye alifuatiwa na Samwel Sitta....

Kabla ya Mzee Sitta alikuwepo Pius Msekwa.

Uwezo wa Anne Makinda ni mdogo mno. Hata yeye anatambua kwamba hana uwezo wa kuwa Spekear wa Bunge la JMT na wala hakuwa amejiandaa kuchukua u-Speaker - aliwekwa pale na kundi la Mafisadi. Hakuna sababu ya kumlaumu sana kwani sio kosa lake na hajui alitendalo. Tuwalaumu wabunge wa CCM kwa kumpigia kura nyingi
 
Alhamis ya wiki iliyopita,spika kwa mara nyingine alikingia kifua kinda lake mizengo kujibu swali toka kwa mwanaharakati na mbunge wa CDM Tundu lissu.Tuone movie nyingine ya kesho,Je waziri mkuu ataendelea kuwa kinda la makinda liliofunikwa kwenye mbawa zake likifurahia hifadhi yake?
 
Katika kutafakari mwenendo wa Bunge letu chini ya Spika Anne Makinda, hasa kwa kulinganisha na mtangulizi wake, Samuel Sitta, nimetambua kwamba kinyume na wengi tunavyofikiria, kwa kweli Anne Makinda anasaidia sana upinzani - na hii hata yeye hajui.

Kitendo cha kujitokeza kuzima maswali "magumu" yanayoelekezwa kwa serikali, kupitia kwa mawaziri na hata waziri mkuu, kitendo cha kujitokeza kuwapa nafasi kubwa wabunge wa CCM kubeza upinzani na wakati huo huo kuwabana wabunge wa upinzani wanapojaribu kujibu mapigo, kwa kweli kinaleta matokeo tofauti na lengo lililokusudiwa. kwanza kabisa kinawafanya wapinzani waumize vichwa kupambana vizuri zaidi na mbinu hizi chafu, na kwa hiyo watatumia vizuri zaidi bongo zao na watakuwa wakali zaidi na zaidi, na smart zaidi na zaidi. pili kinawaunganisha kwa haraka zaidi. inafika mahali inakuwa vigumu zaidi na zaidi mtu kujiita mbunge wa upinzani, kisha ukapanda gari la Makinda na wabunge wa CCM. hali hii inaweza kuimarisha zaidi upinzani kama kambi kwa upana mkubwa zaidi. na hii inadhoofisha mbinu ya "wagawanye uwatawale" ambayo inatumiwa sana na CCM.

Mbali ya hayo, wananchi wanaofuatilia mijadala hii, wengi wanaanza kutambua udhaifu mkubwa wa spika Makinda, ambaye signature yake ni kujificha katika "kanuni" na kuwabeza wabunge wa upinzani kwamba hawajui kanuni, wengi ni wageni, na visingizio kama hivyo. lakini kwa mwendo huu anaokwenda, Spika Makinda anazidi kutoa mwanga kuhusu kiini cha tatizo hapo bungeni, kwamba tatizo ni yeye mwenyewe. hii itapelekea kudhoofisha pia serikali ya CCM.

Tatizo lingine kwa CCM ni kwamba waziri mkuu, Mizengo Pinda, na signature yake ya kulialia na kubembeleza, anaonekana kufurahia mbeleko ya mama mdogo Makinda, anabembelezeka na kulala ka usingizi. hii inadhihirishwa na udhaifu wa hoja ambazo amekuwa akizitoa, mfano alipojibu kuhusu suala la posho. hafanyi kazi ya ziada, kama ambavyo angefanya kama angekuwa anapambana vilivyo na hoja za upinzani. hii imetoa nafasi hata kwa mheshimiwa Stephen Wassira kuuchapa usingizi bungeni, hata baada ya kuachiwa mikoba ya kiongozi wa shughuli za serikali bungeni hapo jana! imagine Tundu Lissu anaibuka na kombora kwa serikali, angejibu vipi? lakini mbeleko ya mama mdogo ipo...

Chini ya Spika Sitta, bunge lilionekana kutoa nafasi kwa wabunge wa upinzani kuibana serikali. hii iliisaidia sana CCM, ingawa hilo halionekani hivyo kwa ma-think tank wa CCM waliochoka. lakini muhimu zaidi - iliwafanya wapinzani wawe katika harmony na spika. hili linaweza kuwa sio advantage kwa upinzani katika mazingira ya mapambano yaliyopo sasa hivi. ni faida zaidi kwa upinzani pale serilkali, baada ya mpambano mkali na upinzani ulioimarika, inapotafuta exit strategy baada ya kugaragazwa, kama ilivyokuwa Arusha. Kwa kuubana upinzani waziwazi, Spika Makinda anatoa rallying-point kwa upinzani na kwa hiyo, bila kujijua, Anne Makinda ni zawadi kwa Upinzani. itumieni vizuri mtafaidi
 
Point noted.Mwisho wa siku watasema kama sio CCM wasingefika walipo.Unamawazo mazuri na hukufunuliwa hili kwa akili ya damu na nyama,juu ya uelewa huo tanzania itapata maendeleo yake kama ilivyotakiwa.
 
naunga mkono hoja, wabunge wenye magamba wamejikuta hawajui kama si kusahau wajibu wao bungeni, kwa kuwa magamba ndiyo chama tawala wamejigeuza watetezi wa serikali zaidi ya kuwatetea wapiga kura wao dhidi ya ukandamizaji wowote unafanywa ama unaotarajiwa kufanywa na serikali yao, kazi imekuwa kumsifu rais kwa sifa za kichina(bandia) wameshindwa kujitenganisha na serikali, hatuyaamini tena magamba na tunayakataa/tutayakataa kwa vitendo, wote semeni AMEN
 
Nimeipenda sana hii analysis yako mkuu,thanks.Wakati wa sitta,kuna baadhi ya wabunge wa sisi em walijitahidi atleast kutokuwa watumwa kwa kuchambua mada kwa kadiri ya uwezo wao na in a way kuto dhalilisha taaluma zao kama ambavyo wanafanya kipindi hiki.KTK Bunge la tisa,you could sense ule utaifa na clear boundary kati ya sirikali na mhimili mwingine wa dola(Bunge),which is no where to be seen now,thats why ninashawishika kuamini kuwa wabunge wa chama la magamba wameamua kwa makusudi(japo wengine ndo thinking yao imefikia limit) kuwapa upinzani umaarufu na serikali yao kugaragazwa vilivyo!
 
Nyie Wabunge wa CCM, mnaingiziwa kete na CDM ambayo siku mtakapokuja kustuka itakuwa too late! Kitu wanachokifanya CDM ni kuwa upande wa Wananchi kuibana Serikali, Nyie wa CCM mmekuwa mkijiona kama ni Viongozi wa Serikali na mmesahau kabisa kuwatetea Wananchi na kwa hili mmeonekana kuyapinga yale mambo mazuri kwa Wananchi ili kusaidia miswaada ya serikali ipite hata kama ni mibaya vipi! Sisi wananchi tunaona kwamba hivi vita ni kati ya Chadema na Wananchi kwa upande mmoja vs CCM kwa upande mwingine.

Kwa kifupi mnadhani mnajenga kumbe mnabomoa. Ngojeni matokeo yake mtayaona 2015.
 
Nimeipenda sana hii analysis yako mkuu,thanks.Wakati wa sitta,kuna baadhi ya wabunge wa sisi em walijitahidi atleast kutokuwa watumwa kwa kuchambua mada kwa kadiri ya uwezo wao na in a way kuto dhalilisha taaluma zao kama ambavyo wanafanya kipindi hiki.KTK Bunge la tisa,you could sense ule utaifa na clear boundary kati ya sirikali na mhimili mwingine wa dola(Bunge),which is no where to be seen now,thats why ninashawishika kuamini kuwa wabunge wa chama la magamba wameamua kwa makusudi(japo wengine ndo thinking yao imefikia limit) kuwapa upinzani umaarufu na serikali yao kugaragazwa vilivyo!

Point muhimu sana hiyo, kwamba kama taifa tunarudi nyuma kutokana na kuwa na watu kama Spika Anne Makinda. Kambi ya upinzani sasa inabidi ijizatiti kubeba bendera ya taifa na kuongoza umma wa watanzania, na kuziba pengo lililoachwa na wale wabunge wa CCM ambao baadhi walijitokeza kupigania maslahi ya taifa. sasa hivi wanakuwa marginalised and silenced - kisa wenye CCM wanataka kudhibiti upinzani!
 
Nakubali shingo upande kuwa Anne anawasaidia wapinzani. Nasema hivi kwa sababu msingi wa Bunge uko kwenye demokrasia ya kweli. Unapokuwa na spika kama Anne ambae anakibeba Chama tawala wazi wazi, dhana ya demokrasia ya kweli inapotea. Hii ni hatari sana kwa "nascent" democracies kama hizi za kwetu.

Ukweli unabaki pale pale kwamba Spika anatakiwa kuwa neutral na kuendesha Bunge kwa misingi ya kanuni na demokrasia.



 
Nakubali shingo upande kuwa Anne anawasaidia wapinzani. Nasema hivi kwa sababu msingi wa Bunge uko kwenye demokrasia ya kweli. Unapokuwa na spika kama Anne ambae anakibeba Chama tawala wazi wazi, dhana ya demokrasia ya kweli inapotea. Hii ni hatari sana kwa "nascent" democracies kama hizi za kwetu.

Ukweli unabaki pale pale kwamba Spika anatakiwa kuwa neutral na kuendesha Bunge kwa misingi ya kanuni na demokrasia.


kweli kabisa Kaniale, hivyo ndivyo inavyotakiwa iwe. hoja inayojengwa hapa ni kwa vipi wapenda demokrasia bungeni wanaweza kutumia hii adversity inayoitwa ANNE MAKINDA na kuifanya kuwa opportunity kwa maslahi ya taifa?
 
Back
Top Bottom