Makinda na Bunge la kelele za taarifa, mwongozo.

Sikupata nafasi ya kuangalia mjadala wa bunge jana kwa muda mrefu. Lakini nilibahatika kufuatilia zile debate za mwisho mwisho. Nilichojifunza ni kwamba vifungu vingi vinapitishwa kwa sababu tu wabunge wa CCM wako wengi na sio kwa uzito wa hoja.

Nilibahatika kuona mjadala kwenye kifungu cha adhabu za makosa ya barabarani na jinsi Mh Tundu Lissu alivyotoa hoja nzito ili kurekebisha kifungu hicho na kuacha kiwango cha 20,000. Majibu yaliyotolewa na Waziri wa Fedha yalinishangaza, nikajiuliza inawezekanaje mtu mwenye akili akatoa majibu yale. Alisema kwa kuwa kiwango cha adhabu kimeongezeka basi kiwango cha makosa kitapungua na hivyo kupunguza mapato kutokana na adhabu hizo. Aibu ilioje!!!!!

Ninaona kabisa kuwa CCM wanawapa nchi hii wapinzani na hasa CDM. Wanadhani wapo pale kwa ajili ya kutetea bajeti ipite tu. Wanashindwa kuelewa kwamba baada ya hapo kuna upande wa utekelezaji. Baada ya hapo kuna bajeti tena ya mwaka ujao. Kutetea tu bajeti na kupitisha kutokana na wingi wao bila kujali maslahi ya wananchi wanajipiga kitanzi wenyewe.

Lazima wajue kuwa wananchi sio wasaulifu kiasi hichi. Tutakumbuka tena haya wanayotetea kwenye bajeti ijayo wakati wanawasilisha utekelezaji wa bajeti hii. Nadhani kuanzia hapo watajifunza kuwa huwezi kuwaongopea watu wote kwa wakati wote. Nawapongeza wapinzani wote walioikataa bajeti hiyo kwa sababu za msingi walizozitoa. Kwani baadaye tutapata ushahidi wa nani alikua anasema kweli, mwaka mmoja sio mkubwa sana na 2015 sio mbali hata kidogo.
 
Kanuni zipo wazi. Spika akiacha kuendesha bunge kwa Mrengo wa Kichama atafanya vizuri. Lakini pia kile walichofanya Chadema ya kumshitaki kimemfanya atafakari, je ni kweli natenda haki hata kwa asilimia 20? Tunatarajia Spika awe huru katika kuendesha vikao bila kuingiliwa na Serikali.
Nashauri Spika awe kama jaji kuwa hata asipochaguliwa tena aendelee kulipwa posho za kuishi mpaka Mungu atakapomchukua. Hii itafanya wanasiasa wengi wanaokuwa Spika wawe jasiri wasiogope serikali!!
 
hatuwez kumpima makinda kwa siku 1, na km analegeza ili akina lissu wamuhurumie na wakishamuhurumia awageuke? Huyu mama hana lolote jema.
 
Sasa nimetambua ni kwa nini spika wa bunge inashauriwa awe mwanasheria... Hii inamaana atakuwa na uwezo mkubwa wa kuliongoza bunge sio mpaka itokee kwamba wamemshitaki kama sasa ndo anakumbuka kutimiza wajibu wake kama kiongozi wa nchi na sio wa chama. Hongera mama Makinda kwa kukumbuka shuka mapema ya saa 7 usiku maana inawezekana ungekufa kwa malaria kwa mbu wa upinzani tulivyokuwa tunahasira nawe ushauri wa bure jaribu hata kama unapendelea isiwe too much kama ilivyokuwa utasaidia sana kujenga nchi kupitia bunge hili la 10. Tukumbuke mwamko wa watz wa leo kufuatilia Bunge haujawahi kujitokeza huko nyuma katika historia ya nchi hii na watz hawa wanahasira na magamba kwa kuwa wanaamini ndo chanzo cha umasikini hivyo magamba wanakazi mara 50 ya kujisafisha japo wao hawalitambui hili
 
Mbona maelezo yako yanapingana
amekosea kumteua gwiji wa sheria kivipi maana kama ni gwiji rais asingekosea

Ndio maana nikasema kwa mtazamo wangu huyu jamaa ni gwiji wa tasnia ya habari lakini kumbe hana kabisa busara za kujenga hoja zake.Kwa hili naona kama rais amechemka kumteua kwa kuwa hana msaada sana kwa rais.Huwa anaishia kumdanganya tu rais katika masuala ya sheria.Mfano mzuri ni uandikwaji wa katiba mpya.

Vipi umenielewa hapo mr rocky.
 
Wana JF
Nakuwa na mashaka sana na uongozi wa huyu mama SPIKA kwani kila wabunge wa CHADEMA wanapotoa kauli za kuonyesha kutokuwa na imani na viongozi wa serikali yeye huja na hii kauli yake ya DHIBITISHA KAULI YAKO

lakini pia hata kama wabunge hao watadhibitisha juu ya kile walichokisema Mama huyu ANNA MAKINDA hukalia udhibitisho huo pasipo kuuweka hadharani na hata pasipo kutoa adhabu kwa wabunge aliowataka wadhibitishe hayo waliyo yaongea

kwa mfano
-Mh Lema juu ya waziri mkuu kusema uongo,kimya hadi leo
-Mh Tundu lisu,kimya hadi leo
-Mchungaji msigwa kimya hakijaeleweka
-na sasa ni Mh zito

lakini pia huyu mama ajue kuwa wabunge wa CHADEMA wanapo simama na kuongea huwa wapo makini na wayaongeayo kwa kuwa wanajuwa kabisa watahitajika kutoa udhibitisho,hivyo huwa wanajiandaa

sasa wana jf kwanini mama huyu huwa haweki wazi yale yaliyodhibitishwa?

ama anafanya kazi kwa maelekezo ya watu furani hivyo yupo pale kulinda maslahi ya watu? kama halindi maslahi ya watu fulani kwanini huwa haweki wazi kilichojili?

Bado na mashaka na uongozi wa mama huyu ktk bunge hili
 
Haya yote ni sisi tulioyaleta......kwa kuweka watu walioshiba watetee walala hoi... Huyu mama amekuwa bungeni miaka nenda rudi...kadiri miaka ya bunge inavyoendelea (yaani tangu baada ya enzi za mwalimu) ndivyo nchi inazidi kuharibika.... Ukisema wenzio wanasema tutakufa na CCM... Uchaguzi ukiisha wanaanza kusema maisha magumu...Ngoja tuendelee kuteseka labda siku moja tutampata mkombozi.
 
Pamoja na mambo mengine swala la spika Makinda kuta uthibitisho ni kuficha zaidi weakness zake kiungozi.

Kama mnafuatilia bunge hili vizuri kama swala lilikuwa kuwa na spika mwanamke basi Jennister Mhagama was the best candiadate... Siyo huyo bibi wa miaka 61 ambaye hana uhuru wa kufanya kazi kwa sababu ya kupachikwa ktk hiyo fasi.
 
Wana JFNakuwa na mashaka sana na uongozi wa huyu mama SPIKA kwani kila wabunge wa CHADEMA wanapotoa kauli za kuonyesha kutokuwa na imani na viongozi wa serikali yeye huja na hii kauli yake ya DHIBITISHA KAULI YAKOlakini pia hata kama wabunge hao watadhibitisha juu ya kile walichokisema Mama huyu ANNA MAKINDA hukalia udhibitisho huo pasipo kuuweka hadharani na hata pasipo kutoa adhabu kwa wabunge aliowataka wadhibitishe hayo waliyo yaongeakwa mfano -Mh Lema juu ya waziri mkuu kusema uongo,kimya hadi leo-Mh Tundu lisu,kimya hadi leo-Mchungaji msigwa kimya hakijaeleweka-na sasa ni Mh zitolakini pia huyu mama ajue kuwa wabunge wa CHADEMA wanapo simama na kuongea huwa wapo makini na wayaongeayo kwa kuwa wanajuwa kabisa watahitajika kutoa udhibitisho,hivyo huwa wanajiandaasasa wana jf kwanini mama huyu huwa haweki wazi yale yaliyodhibitishwa?ama anafanya kazi kwa maelekezo ya watu furani hivyo yupo pale kulinda maslahi ya watu? kama halindi maslahi ya watu fulani kwanini huwa haweki wazi kilichojili?Bado na mashaka na uongozi wa mama huyu ktk bunge hili
lao mojaaaa hao wezi wote, mie hata mmoja simwamin wote magamba tu
 
Mashirika ya kiraia yenye nia njema na mstakabari wa taifa letu watuongoze mtaani kuandamana kuonyesha kutokuwa na imani na huyu mama pale bungeni
 
lao mojaaaa hao wezi wote, mie hata mmoja simwamin wote magamba tu


kina nani hao unaowaongelea kuwa lao ni moja tu?

ila pia naungana na wewe kuwa hao wote kina Mh lema na wengine lao ni moja tu,kwani kanini wasipige kelekele na kusema ukweli kuwa tumewakilisha udhibitisho lakini spika kaukalia kwanini wasiseme nao wamekaa kimya? nadhani ni kweli nao wao ni moja,kama sio hivyo bsai wamweleze spika kuwa tunahitaji yale tuliyo kuletea kama udhibitisho yawekwe wazi
 
Back
Top Bottom