Makinda na Bunge la kelele za taarifa, mwongozo. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makinda na Bunge la kelele za taarifa, mwongozo.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ADVOCATE NEWBOL, May 26, 2011.

 1. A

  ADVOCATE NEWBOL Member

  #1
  May 26, 2011
  Joined: May 21, 2011
  Messages: 33
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Spika Makinda anasema kwamba, "Baada ya hotuba ya bajeti kusomwa Bungeni, Bunge haliwezi kuibadilisha kitu." Spika kwa lugha nyingine anasema, Bunge halina kazi ya kufanya, na kwa nini walipwa kukaa Dodoma kikao cha bajeti wakati hawana cha kufanya? Siamini, na ndiyo maana nimeshtuka sana na kauli hiyo ya Spika. Spika huyu tena kwa mara nyingine amejidhirisha waziwazi yeye mwenyewe, tena kwa hiari yake binafsi pasipo kulazimishwa wala kushawishiwa na mtu yeyote, kwamba hajui kitui: si kitu huyu. Kanyaboya, ni spika mjima katika karne ya 21 kwa sababu hajui kazi ya Bunge. Nampa dosi murua ya Sheria, ngoja nimuelimishe.

  Kwanza tujiulize je, hotuba ya bajeti nini? Hotuba ya bajeti ni maombi ya serikali (executive) kutoka kwa Bunge (parliament) kwamba serikali inaomba fedha kwa ajili ya matumizi iliyoyaainisha na, katika kufanikisha hilo, serikali hiyo2 inaomba pia Bunge liiruhusu itoze kodi na kukopa ili kupata fedha hizo (tazama Ibara za 137 na 138 za Katiba ya sasa ya Tanzania 1977).

  Katika bajeti, Bunge nalo sasa lina mamlaka ya kikatiba ya (a) kurekebisha maombi hayo fedha ya serikali kwa kuyapunguza au kuongeza nk, na (b) kukataa kabisa maombi yote hayo ya serikali na kuiagiza ilete maombi mapya (tazama Ibara za 90 na 139 za Katiba).

  Kwa kweli hii ni hatari kabisa, kama Spika kiongozi wa mhimili huu muhimu wa Bunge hajui mamlaka ambayo Bunge linayo dhidi ya serikali. Hatari. SIYO KWELI KWAMBA HOTUBA YA BAJETI IKISHAKUSOMWA BUNGENI, BASI, BUNGE HALINA LA KUFANYA: MAMA MAKIND, MBALI NA KUKARIRI KANUNI ZA BUNGE AMBAZO ZINATOKANA NA IBARA YA 89 YA KATIBA, SOMA KATIBA ITAKUSAIDIA KTK KAZI ZAKO...
   
 2. F

  FJM JF-Expert Member

  #2
  May 26, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Chadema mjiandae maana kuna mkakati mkubwa sana wa kuzuia hoja zenu ili serikali isiumbuliwe kama Lissu alivyowaumbua Mwanasheria mkuu na Celina Kombani.

  Kwa taarifa nilizonazo ni kwamba wakubwa wamedhamiria kufanya maamuzi kuwa maoni yote juu anything yatolewe wakati wa kamati za bunge. Kwa maana hiyo akishasoma mwenyekiti wa kamati ya bunge basi hakuna mtu anaruhusiwa kusema kitu tofauti especially kama ulikuwa ni mjumbe kwenye hiyo kamati. Lakini kama tujuavyo wenyeviti wengi wanatoka ccm na kazi yao kubwa wanapopewa miswaada na taarifa nyingine za serikali huwa wanaishia kuangilia comma na full-stop!

  Mama Makinda yuko kwenye special mission - kurudisha fikra za zama kimoja. dangerous woman.
   
 3. mfereji maringo

  mfereji maringo JF-Expert Member

  #3
  May 26, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 1,003
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  wanajimaliza hao, wananchi tunafatilia, na tutawajua wanaotutetea na wanaotunyonga.
   
 4. m

  m.o.d.y Member

  #4
  May 26, 2011
  Joined: May 22, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ana makinda kama kaptula la marx na nyerere.
   
 5. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #5
  May 26, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,834
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Ni dhairi Magamba wamekiri RACHEL ni Magamba; Hao hao ndio walimpandikiza Makinda, je na yeye sio gamba? Rostam alikiri kumfuata mama Iringa kumpa dili la Usupika!!!!! Tujadili Hili!!
   
 6. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #6
  May 26, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wewe sasa ndio hujui kitu, karudie tena kumsikiliza alivyosema !
   
 7. m

  m.o.d.y Member

  #7
  May 26, 2011
  Joined: May 22, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wewe unayejua tuambie kasema nini? Nahitaji kufahamu vizuri.
   
 8. Tajy

  Tajy JF-Expert Member

  #8
  May 26, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 298
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hv hawa watu wako humu kwa maslah ya nani,kila kitu chenye ukweli wanaropoka tu utafikir ushuzi wa maharage yaliyo chacha.Kwa nn msiangalie maslahi ya nchi kwanza na yenu mkayaweka baadaye!cjui ni watu wa karne gan hawa,yaani basi tu!niseme hawana akili kabisa!empty mind(think twice,ritz and etl)
   
 9. m

  mndeme JF-Expert Member

  #9
  May 26, 2011
  Joined: Sep 2, 2008
  Messages: 322
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  ni ombwe la uongozi tz hili......naona makinda nae ni gamba linalohitaji kuvuliwa na magamba wenzake akina RACHEL
   
 10. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #10
  May 26, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Anawaka kama e'Kibonomwe (kihaya au kinyankole).
   
 11. Wanitakiani

  Wanitakiani JF-Expert Member

  #11
  May 26, 2011
  Joined: Apr 18, 2008
  Messages: 644
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nadhani una chuki binafsi na huyu mama! mnyonge mnyongeni lkn haki yake mpeni. Kwa hili sikuungi mkono maana umepotosha Wanajamii, hakusema hayo uliyoyapamba kwa lugha nzuri. Alieleza utaratibu mzima na mchakato wa bajeti na hakusema kuwa baada ya bajeti kusomwa Bunge haliwezi kubadilisha kitu. Kwani Bunge lina uwezo wa kupitisha au kutopitisha bajeti ya serikali iwapo ina tatizo. Bunge huishauri serikali na maoni yake mara zote tumeona hufanyiwa kazi na Serikali. kama yeye hataki unadhani wabunge wote watakubali kukaa kimya na kutobadilisha popote hata kama kuna utumbo?
   
 12. Komeo

  Komeo JF-Expert Member

  #12
  May 26, 2011
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 2,393
  Likes Received: 423
  Trophy Points: 180
  Umeshaelezwa kuwa utuambie nawe ulivyomsikia huyo maza alivyosema, ukiingia mitini haikusaidii.
   
 13. A

  ADVOCATE NEWBOL Member

  #13
  May 26, 2011
  Joined: May 21, 2011
  Messages: 33
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nakushkuru kwa kukubaliana na mimi kwamba Bunge lina uwezo na mamlaka ya kikatiba ya kurekebisha bajeti ya serikali ikiwa ni pamoja na kuikataa yote, au siyo? Mimi sina nongwa na MAKINDA, MTANZANIA MWENZANGU
   
 14. M

  Mmongolilomo Senior Member

  #14
  May 26, 2011
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 135
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kiukweli hata mimi niliogopa baada ya kusikia maneno yale. Kwa maana nyingine anaongoza bunge huku akiwa hajui kazi ya Bunge. Duh ni sawa na gari bila dereva lazima lipate ajali.
   
 15. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #15
  May 26, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Ndugu zangu Thinktwice na Wanitakiani,, advocate newbol katika thread yake kasema haya ndo yaliyotamkwa na Spika mama Anna makinda. nyinyi mnasema hakusema hivo, Je alisemaje? mnaweza kuandika hapa aliyosema ili tuwianishe na hivo kujipa uwanja wa kuchangia vizuri? Tafadhali
   
 16. g

  gervase Member

  #16
  Jun 7, 2011
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 41
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Fikiri kidogo hali itakuwaje bungeni pale mbowe atakapoanza kubomoka mipango ya wapinzani. Hapo lisu akijiandaa kumwambia makinda kwa mjibu wa kanuni za bunge, kifungu namba....kinga ya kutodhalilishwa mbunge... Hapo kabwe hajasimulia alichokiona kariakoo. Ebu fikiria Godbless lema atakapoomba mwongozo wa spika... Makinda hataomba feni iwekwe chini ya kiti ipoze moto? Au mnadhani itakuwaje? Mziki huu ataucheza kweli?!
   
 17. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #17
  Jun 7, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Huu mziki usipime mimi nahisi huyu mama anaweza kuomba ajiuzuru uspika.
  Ila c unafahamu udictator wake? Kwake hamna kinacho shindikana na ukizingatiwa amewekwa pale na wakuu wa magamba
   
 18. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #18
  Jun 8, 2011
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  only kama amepitia unyago:becky: !! muziki wa chadema mkubwa bwana!!
   
 19. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #19
  Jun 8, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  hahahahahaa! ukipitia unyago lazima upate mume!!! mumewe ni nani?
  this means hajapitia unyago! hawajui wala hajui jinsi ya ku-deal na wanaume kama friends, na kama mume, hajui hata maneno ya kuongea mbele ya mwanaume mwenye hasira mpaka mwanaume huyo ajinyamazie kwa kuona kijike kimesema jambo la maana.
   
 20. m

  mkulimamwema Senior Member

  #20
  Jun 8, 2011
  Joined: Apr 14, 2011
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yangu macho na masikio tu.
   
Loading...