Makinda na Bunge la kelele za taarifa, mwongozo.

Makinda na Bunge la kelele za taarifa, mwongozo.

Bunge la 10 likiwa ndio lipo katika mkutano wake wa nne limekuwa na changamoto nyingi ambapo suala la nidhamu isiyoridhisha miongoni mwa wabunge, imekuwa ni miongoni mwa kero ambayo wananchi wanaona isipodhibiwa mapema inaweza kuleta madhara.
Hata hivyo, suala la nidhamu kwa wabunge limeonekana kujitokeza kwa mara nyingine katika mkutano huu jambo ambalo limemlazimu Spika wa Bunge, Anne Makinda, kulikemea mara kwa mara.
Miongoni mwa mambo ambayo yanaviashiria vya kiwango cha nidhamu ni masuala ya kuomba mwongozo wa spika na taarifa mara kwa mara wakati wabunge wenzao wakichangia ama kuhoji masuala mbalimbali.
Lakini cha kusikitisha zaidi ni pale baadhi yao kuwasha vipaza sauti na kuzungumza bila kuruhusiwa na Spika ama mwenyekiti wake kwa kadri kanuni za Bunge zinavyowataka.
Hali hiyo inaonekana kumkera spika Makinda na kulazimika kuwataka wabunge kuacha mambo ya ovyo wanapokuwa katika vikao vya Bunge kwani wanatia aibu kwa watu wanaowatazama.
Vile vile, anawaasa wasome vizuri bajeti ili watakapochangia watoe hoja za msingi.
Anaelezea moja ya kikao ambacho wabunge walifanya vituko vya ajabu kiasi cha yeye (Makinda), kushindwa kuendelea kuangalia mwenendo wa kikao hicho wakati akiwa nyumbani kwake.
“Hii ni aibu kubwa na sijui kwanini mnajidharaulisha kwa wananchi, mnajua watu huko nje wanawaheshimu sana, sasa mkifanya mambo ya ovyo wanawadharau na mjue haya yote yanayofanyika humu yanaonekana, mimi mwenyewe nilikuwa naangalia lakini nikashindwa kuendelea kwani nilikuwa naona vitu vya ajabu ajabu,” anasema Makinda.
“Hapa bungeni kuna utaratibu wa kuzungumza, mtu akiwa anazungumza wengine mnapaswa kumsikiliza lakini jana (juzi), mtu mmoja anachangia na wengine wanazungumza utadhani mko Kariakoo, “anasema akionyesha kukerwa na tabia hiyo iliyofanyika wakati kiti chake kilipokaliwa na Mwenyekiti wa Bunge, George Simbachawene.
Katika kikao hicho, kilichoongozwa na Simbachawene, wabunge walikuwa wakiwasha vipaza sauti vyao na kutoa maneno ya vijembe kwa wenzao na wengine wakizomea wachangiaji.
Hali hiyo ilimpa wakati mgumu mwenyekiti huyo ambaye alikuwa akilazimika kuwakatisha wabunge waliokuwa wakiomba mwongozo ili kuwabana wazungumzaji walioonekana kuwakejeli wengine.
“Waheshimiwa wabunge tutumie muda wetu kujadili huu mpango uliombele yetu, nikiruhusu kila mtu asimame atoe mwongozo muda wote tutakuwa tumeupoteza bure, naomba tuwe makini,” anasema.
Hali hiyo inajitokeza tena kwa mara nyingine hata baada ya Spika kukemea na hiyo inamfanya kukemea tena kwa mara nyingine ambapo anawataka wabunge hao kujiheshimu kwa kuwa watu wanaowatazama wamekuwa wakimpigia simu mara kwa mara kueleza kukerwa na mambo yanayojitokeza bungeni.
Hata hivyo, hayo yote yanatokea wakati wabunge wakiwa katika kipindi cha muhimu ambacho wananchi waliowapigia kura wanawategemea kuchangia hotuba ya bajeti.
Wakichangia katika bajeti hiyo ambayo iliyotarajiwa kupitishwa jana, wabunge wameonekana kutofautiana huku wengine wakitishia kutoipitisha ikiwa masuala muhimu waliyoishauri serikali hayatajumuishwa kwenye bajeti hiyo.
Wabunge hao bila kujali vyama wanavyotoka wamekuwa wakielezea mazuri na mabaya yaliyomo kwenye bajeti hiyo na kuishauri serikali kuyaingiza kabla ya bajeti hiyo haijapitishwa.
Mbunge wa Mbozi Magharibi (Chadema), David Silinde, anasema serikali ilitangaza mikoa na wilaya mipya lakini cha kushangaza kwenye bajeti haijawekwa; na kutangaza kutounga mkono bajeti hiyo.
“Wananchi wa jimbo langu wamenituma kuja kukataa hii bajeti kama mikoa na wilaya mpya iliyotangazwa haitatengewa fedha, inaonekana serikali ilitangaza mikoa na wilaya mpya kisiasa kuwaridhisha wananchi ili ipate kura nyingi lakini baada ya uchaguzi mmeitelekeza,” anasema.
Anasema hii ni serikali ya ajabu inayotaka kukusanya mapato yake kwa makosa ya barabarani kwa kuongeza faini ya 50,000 iliyopendekezwa kwenye bajeti badala ya kubuni vyanzo vipya. Nyongeza hii ni eneo lililopingwa na wabunge wengi wakieleza kwamba inalenga kutengeneza mazingira ya rushwa kwa askari wa usalama barabarani.
“Ile faini ya 20,000 ilikuwa haifiki serikalini zinaishia kwa polisi wanaozitoza sasa serikali imewaongezea ulaji maana hata hizi 50,000 hazitafika, ni jambo la aibu serikali kutegemea mapato ya makosa ya barabarani.”
Mbunge wa Viti Maalum, Amina Mwidawi, (CUF), anasema haoni tofauti kati ya bajeti ya mwaka huu na iliyopita kwani kinachoonekana serikali imenakili ile ile kwa kuwa hakuna jambo jipya.
Anasema serikali haiwezi kufikia malengo ya milenia MDGs kama imeshindwa kukabiliana na baa la njaa kwani mikoa mingi wananchi wanaishi kwa kubahatisha kutokana na ukosefu wa chakula.
Anasema ukuaji wa uchumi unawanufaisha watu wachache wa juu hivyo kuwapa matumaini wananchi kwa takwimu za kukua kwa uchumi hakutawasaidia ila wanachohitaji ni maisha bora.
Mbunge wa Bukoba Vijijini (CCM), Jasson Rweikiza, anasema bila umeme shughuli nyingi zinasimama hivyo serikali lazima ihakikishe inawekeza vya kutosha kwenye nishati hiyo.
Anasema wananchi wa jimbo lake wamechoka kuona nyaya za umeme zinapita juu yao lakini kwa miongo kadhaa sasa wanausikia umeme redioni.
Anasema lazima serikali iweke mkakati wa kuwasaidia wananchi wa kipato cha chini kuunganishiwa umeme kwani wengi hawana uwezo wa kulipia sh 500,000 wala 1,000,000.
Anasema hata wizara ya afya imetengewa fedha kidogo hali ambayo itasababisha mambo mengi kukwama yakiwemo ya jimbo lake.
“Naisubiri bajeti ya wizara ya afya, tutashikana mashati hapa na haitapita kwa kweli, hospitali yetu inasifa zote lakini haijatangazwa kuwa hospitali teule kwanini, waziri na watendaji wake nadhani wamenisikia tutashikana mashati hapa.”
Albert Ntabaliba wa Manyovu (CCM), anasema nidhamu ya kazi imepotea na watu wengi wamekuwa wakifanyakazi kwa mazoea tu.
Anasema lazima serikali ianzishe utaratibu wa kuwatimua watumishi wazembe na wale ambao wamekuwa kama mchwa wa fedha za umma badala ya kuwalea.
“Wala rushwa wasichekewe, wafukuzwe wakibainika la sivyo kazi hazitafanyika, miradi mingi inakwama kutokana na watendaji kuiba fedha za miradi tutawavumilia mpaka lini.”
Kange Lugola Mwibara (CCM), anasema kasi ya kupambana na umaskini bado haitoshi kabisa na alishauri serikali iweke mikakati ya kuutokomeza sio kuupunguza.
Anaishauri pia serikali iunde mamlaka ya kuutokomeza umaskini ili kuhakikisha wananchi walio wengi hawaishi tena kwenye umaskini wa kutupa.
“Sitaki kusikia mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyewe, watu hawa maskini hawakopesheki kila wanakoenda wanakataliwa hivi wao sio Watanzania, lazima tutafute namna ya kuwakopesha maskini.”
Mbunge wa Chonga, Haroub Mohamed Shamsi, anasema bajeti haina uhalisia wala haionyeshi kuwa itatekelezeka na imewekwa kwa ajili ya kuwafurahisha wananchi wapate matumaini.
Steven Masele Shinyanga Mjini (CCM), anasema wanaokejeli bajeti ya serikali kuwa inategemea fedha za kuomba omba wasijisahau na kudhani hiko ni kikao cha harusi kinachotegemea michango ya ndugu na jamaa.
“Hili ni Bunge jamani sio vikao vya harusi, bajeti ni halisia na fedha zitapatikana.”
Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde, (CCM), anataka Gereza la Isanga liondoke katika Mkoa wa Dodoma kwa maana ni laana inayokwamisha maeneo ya mkoa huo. “gereza hili lihamishiwe maeneo mengine na ikiwezekana lipelekwe Tabora.”
Akizungumzia kuhusiana na wazo la serikali kuhamia Dodoma, Lusinde anasema haiwezekani kuwa na wimbo wa kuhamia Dodoma wakati serikali haionyeshi kwa vitendo dhamira ya kuhamia mkoani hapa.
Anahoji ni kitu gani kinachowafanya kutohamia Dodoma na kwamba utekelezaji wa lengo hilo bado ni tatizo kwa viongozi wa ngazi za juu.
Anasema imefika wakati viongozi wanaong’ang’ania Dar es Salaam wafukuzwe kama hawataki kuhamia Dodoma ama serikali ifute kauli yake hiyo.
Wabunge wanachangia mjadala wa bajeti na ule wa maendeleo kwa itikadi za vyama, wale wa upinzani wanakosoa maeneo kadha wa kadha wakionyesha wasiwasi juu ya utegemezi wa bajeti kutoka kwa wahisani na kutokuwepo kwa ubunifu wa vyanzo vipya vya mapato.
Wakati wabunge wa CCM wamejielekeza zaidi kwenye kutetea bajeti na kukejeli michango ya upinzani; hata pale inapokuwa na tija.
Huu ndio Mkutano wa nne wa Bunge ambao kwa kweli umeacha historia ya kuwachefua baadhi ya wananchi kutokana na nidhamu inayoonekana katika mhimili huo wa dola.
 
Kitendo cha Anne Makinda kuamua kutuma ujumbe wa watu wanne huko Uingereza wakati huu ambapo bunge la bajeti linaendelea, eti kufuatilia chenji ya malipo ya rada, kinastahili kulaaniwa kwa nguvu zote; kwani siyo kimeingiza nchi yetu katika gharama zisizo za lazima, bali pia kimedhalilisha bunge na nchi yetu kwa jumla. Nasema hivyo kutokana na ukweli kwamba katika miaka ya karibuni serikali imepoteza fedha nyingi kutokana na wizi wa wazi wazi unao wahusisha baadhi ya viongozi na watendaji waandamizi serikalini, na bunge limeshindwa kuibana serikali kwa wizi huo kutokana na ushabiki wa kisiasa. Aidha hata kwenye suala hili la ununuzi wa rada, bunge limeshindwa kuitaka serikali kuwachukulia hatua wale wote wanao husika na wizi huo. Katika hali hiyo, wabunge waliotumwa huko uingereza, hawakuwa na hoja yeyote ya maana ambayo wangeliwasirisha kwa mamlaka husika na wakasikilizwa. Hivyo safari yao hiyo ni ya kutalii tu na wala haina maslahi yeyote kwa taifai
 
Mimi nikifikiria milion ngapi zile za kuifatilia richmond wallah napata kiwewe.......subiri usikie gharama za huo ujumbe wa NDUNGAI
 
Imekuwa ni jambo la kipuuzi kusafiri kwenda kushawishi waliokubali kuturejeshea pesa tulizoibiwa lakini tunashindwa kuwafuata KAGODA na wanaEPA walio hapa hapa nchini. Kama tukiwa na utaratibu mpya wa kuwafuata wajoli (wadaiwa) wetu wote, hata wa ndani, ni jambo jema. Vinginevo this is a sham!!

What is see is that they will come with empty hands!! BAE entered a plea and the Crown Court issued a verdict based on mutual agreement between them. If BAE had not entered the guilty plea, there could have been a court verdict with people serving time in jails and/or huge fines to BAE. All the Government of Tanzania ought to do is seek to know which CBOs will get the money and plan with them the impementation of agreed recommendations. Otherwise Number 10 should keep the money for as long as necessary.
 
It is a bad move na hii yote na kwa viongozi kujiona wanajua kuliko wananchi wa kawaida kwani maamuzi haya yamefanywa bila kuwashirikisha wananchi. wana jf na watu wengine wote inaelekea ushindi unakuja kwa zile email zetu kwani kitendo cha email zetu kutajwa kwenye press conference yao ya jana huo ni ushindi mkubwa kwetu kwamba email zile zinafanya kazi.
 
Kitendo cha Anne Makinda kuamua kutuma ujumbe wa watu wanne huko Uingereza wakati huu ambapo bunge la bajeti linaendelea, eti kufuatilia chenji ya malipo ya rada, kinastahili kulaaniwa kwa nguvu zote; kwani siyo kimeingiza nchi yetu katika gharama zisizo za lazima, bali pia kimedhalilisha bunge na nchi yetu kwa jumla. Nasema hivyo kutokana na ukweli kwamba katika miaka ya karibuni serikali imepoteza fedha nyingi kutokana na wizi wa wazi wazi unao wahusisha baadhi ya viongozi na watendaji waandamizi serikalini, na bunge limeshindwa kuibana serikali kwa wizi huo kutokana na ushabiki wa kisiasa. Aidha hata kwenye suala hili la ununuzi wa rada, bunge limeshindwa kuitaka serikali kuwachukulia hatua wale wote wanao husika na wizi huo. Katika hali hiyo, wabunge waliotumwa huko uingereza, hawakuwa na hoja yeyote ya maana ambayo wangeliwasirisha kwa mamlaka husika na wakasikilizwa. Hivyo safari yao hiyo ni ya kutalii tu na wala haina maslahi yeyote kwa taifai
Sijaona kosa hapo mkuu au kimahesabu uliyopata gharama za safari ni kubwa kuliko balance wanayo claim?
 
Sijaona kosa hapo mkuu au kimahesabu uliyopata gharama za safari ni kubwa kuliko balance wanayo claim?
wakuu mnijuze waliongelea emails kwenye mkutano gani? Na nani alifanya huo mkutano? Kweli magamba wamechoka...
 
Nashawishika kuamini kuwa ufisadi wa Rada ulisaidia Makinda kuwa Spika,na yeye alifaidi ndio maana yupo tayari kutumia njia yoyote hata kama ni kinyume cha sheria kushawishi chenji irudi.Spika anafanya kazi ya serikali,
 
Mkuu umesema ukweli hawana agenda yoyote mezani wamekuwa weupe kweli kweli kana kwamba hawajui tatizo limeanzaje na kwa nini limefikia hatua ya sasa. Matumizi mabaya ya fedha yetu.
 
May be natakiwa kuelimishwa. Kwani pesa ni za bunge au government? Kazi ya bunge ni kuisimamia goverment ila si kufanya kazi kwa niaba yake. Nilitegemea viongozi wa govenment waende kufatilia na si bunge. Naomba ufafanuzi kwa wanaoelewa jambo hili.
 
Ni wazi Anne Makinda si spika mwenye uwezo wa kuongoza bunge la kizazi hiki kilicho ndani ya multiparty democracy.She has always striven to indiscriminately defend interests of her party (CCM) even at the expense of national interest.History will judge her, let us wait and see, it is only a matter of time she will fall into oblivion.
 
Wadau nimekuwa mfuatiliaji makini sana wa siasa za inchi yetu TANZANIA,Katika sekta mbali mbali za siasa hasa miimili mitatu ya serikali SERIKALI KUU,BUNGE NA MAHAKAMA,japo kuwa imejaa uozo na mizengwe mingi ya rushwa na ufisadi nimefanikiwa kubaini kuwa kwa upande wa BUNGE uozo mkuu uliopo ni "REDIO CASSETE PLAYER KUWEPO NDANI YA ULIMWENGU WA IPOD,IPAD NA MP3 PLAYERS! Hapa namzungumzia spika wa bunge anna makinda. kwa mtizamo wa haraka sana unaweza ukadhani spika huyu ni mtu wa kujali sana maadili na uwajibikaji pamoja na maslahi ya taifa mbele kwajinsi ya unafiki wake pindi anapokuwa bungeni. lakini ukichunguza kwa kina utagundua kuwa amekuwa ni mtu anaye eendesha bunge kwa maagizo ya watu,au mtu flani huku akihofia nafasi yake kama spika kuchukuliwa na mtu mwingine.mbali na kuwa na shaka na uwezo,utashi na elimu yake huyu mama pia watanzania tulio wengi tunakuwa na mashaka na uongozi wa bunge katika kutetea maslahi ya taifa letu. Kimtazamo spika makinda amekuwa akitaka kuliendesha bunge kiimla na kwa ukali kama yalivyokuwa mabunge ya zamani ambayo hayakuwa na wasomi wengi na changamoto nyingi kama ukilinganisha sasa,ndio mana si ajabu kwa spika kuzima hoja,kimfukuza mbunge,kumfokea mtu yoyote nas pia hata kumkalisha chini kwanguvu mtu yoyote ambaye huonekana kwenda kinyume na matakwa ya hao waliompa uspika! Bunge letu limekuwa kama la KIKOMUNISTI KATIKA ULIMWENGU WA KIBEPARI!
 
Hujakosea kabisa mkuu huyu spika hatendi haki bungeni hata kidogo, ila akae mkao wa kula chadema si mchezo hao jamaa wamejipanga kwelikweli, sidhani kama atamaliza muda wa uspika kwa jinsi wanavyompelekesha nina mashaka ataachia ngazi mapema
 
MBUNGE wa Kasulu Mjini, Moses Machali (NCCR Mageuzi) amemshutumu Spika wa Bunge, Anne Makinda kuwa anaonesha upendeleo wa wazi kwa wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuwakandamiza wa upinzani.

Alitoa hoja hiyo wakati anachangia hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu baada ya Makinda kumtaka aache kutumia neno uhuni katika mchango wake.

Machali baada ya kuelezwa hivyo na Spika, alisema “Mheshimiwa Spika haya maneno makali yanaonekana tu wakati sisi wabunge wa upinzani tunapokuwa tunachangia? Mbona Mheshimiwa Shelukindo (Beatrice) ametumia maneno haya wakati anatusema sisi wapinzani umekaa kimya?

“Mbunge yule katumia maneno makali kwa kutuita sisi ni wahuni, lakini umekaa kimya. Tunaomba kuwe na check and balance maana inaonekana sisi wapinzani ndiyo tunadhibitiwa zaidi kuliko wabunge wa CCM,” alisema Machali.

Katika mchango wake, Machali alisema kuna mambo yanafanywa kihuni ndani ya Serikali dhidi ya wananchi wa Kigoma kwa kuwa, kuna fedha zilitengwa katika bajeti ya mwaka huu ili zikatengeneze barabara ya kutoka Kasulu kwenda Nyakanazi, lakini hakuna utekelezaji.

Baada ya kutoa hoja hiyo, ndipo Makinda alimkatisha na kumtaka atumie maneno mengine kwani hayo sio lugha ya kibunge.

Machali alisimama tena na kurudia maneno hayo, "Hata Rais aliahidi barabara hiyo itajengwa; lakini fedha zimehamishwa hivi huu sio uhuni? Halafu tunaona ujenzi ule umeanzia Nyakanazi kule sio Kigoma," alisema Mbunge huyo.

Kwa upande wake, Shelukindo akichangia katika hoja hiyo, alisema baadhi ya wabunge akimaanisha wapinzani wa ajenda za kijingajinga kutokana na kitendo chao cha kushupalia mambo ya posho.

Shelukindo alisema, baadhi ya wabunge wamekosa nidhamu kwa kisingizio cha siasa na wala hawaheshimu wakubwa kutokana na lugha wanazozitoa wakati wakitoa michango yao bungeni.

Alisema wabunge wanaopinga posho wana ajenda ya kisiasa ya nyuma yake na akadai kuwa wananchi wanajua umuhimu wa posho kutokana na wabunge kusaidia baadhi ya mambo katika majimbo yao.
 
Naona ni haki yake lazima aitete serikali....Hayo ni mawazo yake hana budi kufanya hivyo.
 
Back
Top Bottom