NUKUU YA LEO.
I have gone to join Ken, if I am that lucky.
Nimeondoka kumfuata ken, nina bahati katika hilo.
Muendelezo wa nukuu ya suicide note ya kevin Carter. Party 3
Tarehe 11 mwezi March 1993 Kevin Carter anafika eneo la Sudan kusini wakiwa na Joao Silva. Walienda sudan wakiwa na vikosi vya umoja wa Mataifa wakati wa njaa kubwa nchini Sudan.Wakiwa kwenye shughuli zao za kawaida ulifika muda vikosi vinagawa chakula , huu ndio ulikuwa muda wa kina kevin na silva kupiga picha.
Inasemekana hapa ndio Kevin Carter anakutana na mtoto mwenye njaa akiwa ameshindwa kutembea kwenda kwenye foleni ya kupokea chakula, wakati huo huo anakuja Kunguru anayeonekana kutaka kumla yule mtoto mdhoofu.
Kevin Carter anampiga picha mtoto akiwa hawezi kutembea na amejiinamia kuonyesha kuwa hawezi tena kutembea wala kuinuka, nguvu zimemuishia na wakati huo huo Kunguru anajongea kwa nyuma tayari kwa kumfanya mtoto kitoweo.
Kevin Carter anakauza hiyo picha kwa jarida la The New York Times, na kwa mara ya kwanza tar, 26 march 1993 picha hiyo inachapishwa. Magazeti mengi yanaichukua na kuichapisha yakionesha kuuzunishwa na hali ya mtoto huyo.
Kuanzia tarehe 27 march 1993, watu wengi ulimwenguni wanawasiliana na gazeti la The new york times kama Yule mtoto alifanikiwa kufika kwenye kituo cha ugawaji wa chakula, Tarehe 30 march 1993 gazeti linatoa majibu kuwa mtoto alisimama kuendelea na safari baada ya mpiga picha kumfukuza kunguru ila bado haifaamiki kama alifika kituoni.
To be continued in 10 hours to come.