Rekodi bado ipo imesimama haijavunjwa.
Kikosi kile cha Cameroon mwaka 1990 kilimfanya marehemu Pepe Kalle kutunga nyimbo mahsusi kwa Roger Milla na kikosi kizima cha Simba Wasiofugika ( Indomitable Lions ).
Ikumbukwe mechi ya ufunguzi wa Kombe la Dunia mwaka 1990 pale Italy, ilkuwa ni Argentina ( Mabingwa watetezi ) dhidi ya Cameroon.
Mechi iliisha kwa Cameroon kuifunga Argentina 1-0 , huku Diego Armando Maradona akibanwa vilivyo kabisa ( Man marking ) na Emanuel Kunde na matokeo hayo kuishangaza Dunia.
Cameroon ikaenda hadi robo fainali alitolewa na England. Hivyo kuwa timu ya kwanza ya Afrija kufika robo fainali ya WC.