
ZABURI 63
6.Ninapokukumbuka kitandani mwangu,Nakutafakari wewe makesha yote ya usiku.

Unapolala unatafakari nini?
Je unatafakari shida?dhiki tabu,magonjwa,misiba,kukosa,kufukuzwa kazi,kukataliwa

Usiku wa leo mwambie Mungu ASANTE pamoja na mapito yote na misukosuko ya maisha ,kuuguliwa,tabu kukosa chakula lipo jambo kubwa ambalo Mungu anaendelea kufanya katika maisha yako ambalo utaliona pale utakapomtafakari yeye tu na kumshukuru...Mshukuru Mungu kwa kila jambo naendelea kumtafakari usiku wa leo kwa matendo yake makuu ya upendo na wema.
TUOMBE
Asante Baba kwa wema wako,tunajikabidhi mikononi mwako huku tukiutafakari wema na fadhili zako.
Tunaomba ulinzi wako na uwe nasi malaika walinzi watuzunguke katika vitanda vyetu akitusaidia kukutafakri na kutupa ulinzi wa mwili na roho.
Tunaomba utuamshe salama na utupe amani ya mwili na roho..utupe matumaini.
Tunawakabidhi kwako wagonjwa,yatima,wafiwa naomba faraja itawale.
Naomba katika jina la Yesu mpatanishi na mwokozi wetu
AMEN
.
MBARIKIWE USIKU MWEMA