Makapuku Forum

Makapuku Forum

1/Lake Hillier
cf00833476c23a93e2febce658f0f0a0.jpg
cb723f0191d12b2da06c0a2f05829332.jpg

Hili pia lipo Australia
Rangi yake ni ya kudumu hata maji yake yakichotwa bado hubakia vilevile
Wanasayansi hadi leo hawajui sababu
.
.
.
.
.
Shukrani kwa waliosapoti mada
Tukutane kesho
Mwisho
..........
Shukrani mkuu Bitoz kwa kumi bora
 
Muziki: It is Almost Furahiday

Habari Makapuku wenzangu, poleni na mihangaiko ya siku nzima na kama kawaida, kesho ni siku nyingine tena na kama jua halikung'aa leo basi nani anayajua ya kesho.

Karibuni tena katika ka-kipengele kafupi ka muziki na hasa tukijikita kwenye utamu wa gitaa. ndiyo, tunaangalia udonoaji wa gitaa katika muziki/wimbo ambao bahati mbaya sana huwa nauchagua (labda wakati mwingine unaweza kupendekeza wimbo ambao unadhani gitaa linasikika vizuri na tukauangalia pamoja)

Hongera Timu ya Taifa ya Vijana, kazi nzuri na n9i ninyi wenyewe ndo mtaamua hatma yenu katika soka.

Leo tupo Africa Mashariki na tunasogea kwa majirani na watani zetu waKenya. Hapo tunamkuta mwanamuziki maarufu kwa nyimbo za kiharakati na hasa mapambano dhidi ya rushwa na ulevi wa madaraka.

Anaitwa Eric Wainaina, inawezekana huyu ndiye akawa ni mwanamuzi mwenye mafanikio makubwa zaidi katika EAC (siongelei mafanikio ya kifedha, mafanikio ya kimuziki ni zaidi ya mwanamuziki kumiliki fedha- fiat money etc), keshafanya muziki na wanamuzi wakubwa duniani akiwemo Baaba Maal, Angelique Kidjo na Chakachaka.

Keshatumbuiza katika tamasha la World Cup 2010 (yote ufunguzi na ufungaji). Mshindi wa tuzo za Kora na kashiriki matamasha kadhaa maarufu duniani ikiwemo Sauti za Busara.

Huyu ndiye Eric Wainaina, ambaye hupiga gitaa na muziki wake ni mchanganyiko wa Benga muziki asili ya Kenya na ladha za EAC hususani pande za Kongo.
Anajulikana zaidi kwa wimbo wake Nchi ya KItu Kidogo, wimbo ambao ulimpa nafasi ya kufanya kazi na UN na mashirika yake katika harakati za kupambana na Rushwa.

Ninapenda anavyopiga gitaa lake na ninakushirikisha usiku huu kumsikiliza katika wimbo wake wa Nchi ya Kitu Kidogo


Sina elimu juu ya gitaa ila gitaa ninalolisikia lina sauti nzuri utatujuza ni gitaa gani hilo.

Afande ukitaka ya soda burudika na Fanta
 
Karibu tena. Uliondoka kabla sijawa mwenyeji sana hapa Makapuku. Wakati ule nilikuwa nachungulia tu na kupotezea. Kamwe sikuota kuwa siku moja patakuja kuwa kimbilio langu la kuondoa stress na kujifunza mambo mbalimbali kuanzia historia (Dikteta Mussolini anatusomesha sawa sawa), muziki (tunafundishwa na Obe), Habari za magazetini (Shululu), top ten pamoja na Je Wajua (Madenge na makapuku wengineo), Mambo ya imani (Mtumishi Blessed Hope anahakikisha hatuendi motoni), Ulimbukeni wa Mapenzi (Shedede na "mkewe") pamoja na utani na vichekesho visivyo na mwisho kutoka kwa akina Shunie, Husna, Tumosa, Sakayo na mumewe) na makapuku wengine.

Hongera kwa kumaliza masomo na karibu tena. Bila shaka tutafaidika na ulichojifunza huko Israeli. Hata kama ni zile ishu za jamaa wa Mossad we tumegee tu. Blessings!
aiseee nimejikuta nacheka sana
shimba ya porini kwema lakini
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom