Muziki ni Maisha
Makapuku habari za kushinda, najua tumefurahia segment ya 'wadada waliojaariwa maumbo makubwamakubwa' kwa hisani ya
Bitoz , sasa turudi kidgo kwenye mambo ya muziki na kama kawaida ni vionjo vya gitaa huufanya ,muziki uwe na utamu unaopendeza kwa wengi wetu.
Leo tupo hapa nyumbani, na zaidi pande za Bagamoyo. bagamoyo ni mji wa sana aa na unasifika kwa kuwa na chuo kikubwa kabisa na maarufu kwa kufundisha wasanii wa fani tofauti nchini na duniani kwa ujumla. Wapo wasanii wengi wamepita Bagamoyo, bahati mbaya sana wengi hawa hawana jina kubwa sana nchini na nyimbo zao nyingi hazipewi nafasi kwenye vituo vya radio au TV. Kuna sababu, unamjua Jhikoman, Ashimba, na Vitali? wanavuma nje ya mipaka ya Tanzania kuliko nyumbani. Sad.
Anajulikana sana hapa nchini kwa wimbo wake wa
Sumu ya Teja, huyu ni Vitali Maembe. Vitali anajua kuimba, kutunga na kuandika mashairi.
Hupiga gitaa la nyuzi sita, na unapochanganya na sauti yake ya mchomoko basi hutachoka kumsikiza akiimba na kupiga gitaa lake.
Mara nyingi sana na nyimbo zake zote zinamfanya awe ni mwanaharakati zaidi, anapingana na rushwa na kutokana na aina ya muziki anaofanya keshaingia matatani na watawala mara nyingi ikiwemo kupigwa na kufutwa kwa ziara ya album yake yenye jina
Chanjo ya Rushwa.
Ukipata nafasi isikize album hii, ipo bure mtandaoni kwani ilipata ufadhili wa Waswidi na ilikuwa wafanye ziara nchi nzima kugawa hii album lakini wenye mamlka hawakupenda, nadhani iliishia Dar na Bagamoyo tu.
Muziki una nguvu, na hivi ndivyo imekuwa wakati wote, hayupo wa kumpangia msanii nini cha kuimba na kama alivyowahi kusema Steve Biko ' naandika nnachopenda' ndivyo wasanii mahiri wataendelea kuisemea jamii ikiwa wabunge na wanasiasa watakaa kusema matumbo yao.
Msikize Vitali hapa akidonoa gitaa la nyuzi sita
Tujiandae na kusherekea Siku ya Mama