
ZABURI 63
6.Ninapokukumbuka kitandani mwangu,nakutafakari wewe makesha yote ya usiku
7.Maana wewe umekuwa msaada wangu,Ma uvulini mwa mbawa zako nitashangilia.
8. Nafsi yangu inakuandama sana,mkono wako wa kuume unanitegemeza.
TUOMBE
Tunakushukuru Mungu Baba kwa ulinzi wako wa mchana kutwa asante Baba kutufikisha umbali huu,tunaomba toba kwa makosa yote tuliyotenda kwa mawazo ,maneno ,matendo na kutotimiza wajibu zetu mbalimbali uturehemu twakusuhi Baba maana tumetenda dhambi,tunawaombea watu mbalimbali Makapuku family yote,ndugu,jamaa na marafiki wanaomjua Mungu na kumuamini na hata wasiooamini wape nguvu ya kukutafuta kwa bidii,Baba tunaombea wafiwa,waliopata maafa yote ya maporomoko na shida mbalimbali tunazozifahamu na ambazo hatuzifahamu tenda muujiza kwao,wape faraja na matumaini mapya,wagonjwa waponye,wenye dhiki na taabu wape faraja,tunaombea ndoa zote Mungu tunaomba wanandoa wakapendane na kuheshimiana na kuvumiliana na kusameheana katika kila jambo,tunaombea familia zetu amani,upendo,mshikamano watoto wawe watii na hofu ya Mungu itawale,baba tunaomba usiku waleo ukatume malaika wako waweke vituo majumbani mwetu ulinzi wako uwe ngao yetu damu ya Yesu itufunike utukumbatie kama kuku anavyokumbatia vifaranga vyake mwovu shetani ashindwe katika jina la Yesu tunakemea wachawi,wanga,mapepo na nguvu zote za giza zishindwe katika jina la Yesu Damu yaYesu itawale majumbani mwetu na ituamshe tukiwa salama na wazima tayari kukutumikia,asante kwakuwa utatenda sawa na mapenzi yako katika jina lipitalo majina yote jina la Yesu Kristo mpatanishi na mwokozi wetu Amen
Raha ya milele uwape marehemu wote,na mwanga wa milele uwaangazie wapumzike kwa amani Amen
NAWATAKIA USIKU MWEMA

NAWAPENDA SANA
