Tarehe kama ya leo:
2010 - Binamu yangu anafariki Dunia kifo cha ghafla.
Hakika ni majonzi na simanzi kubwa alituachia ukizingatia siku ya kifo chake alishinda salama na akiwa na uchangamfu wa kutosha tu. Kumbe usiku wake anaenda kututoka.
Leo ni miaka 7 toka ututoke Duniani, daima unakumbukwa na ndugu, jamaa na marafiki. Pengo lako bado halijazibika.
Pumzika kwa amani, bado tunakuombea na iko siku tutaonana tena. Gone but never forgotten.
Bwana alitoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.
Pole sana mkuu Mussolin5 naungana nawe katika kumuombea binamu mpendwa
NAMUOMBA MUNGU ATUPE UVUMILIVU WA KIMAPENDO,BWANA ALITOA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIBARIKIWE NA DAIMA TUWE NA MATUMAINI,SINA NENO ZURI LA KUSEMA BALI NAOMBA TUUNGANE HAPA :
1 WATHESALONIKE 4
13.Lakini ,ndugu zangu,hatutaki msijue habari zao waliolala mauti,msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini.
14.Maana ,ikiwa twaamini ya kwamba,Yesu alikufa akafufuka vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu Mungu atawaleta pamoja naye.
15. Kwakuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana ,kwamba sisi tulio hai tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana,hakika hatutawatangulia wao walioisha kulala mauti.
16. Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko ,na sauti ya malaika mkuu na parapanda ya Mungu,nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.
17.Kisha sisi tulio hai tuliosalia ,tutanyakuliwa pamoja nao mawinguni,ili tumlaki Bwana hewani na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.
18.Basi farijianeni kwa maneno haya.
Naomba tuamini kuwa Binamu mpendwa wetu amelala na tutaonana siku ya mwisho,nafsi yake ipokelewe na Mungu wetu
"Wale tunaowapenda hawaendi milele,wanatembea pembeni yetu daima,hatuwasikii,hatuwaoni
Lakini wapo daima nasi,tunawapenda,tunawahitaji,tunawakumbuka wanadumu mioyoni mwetu....upendo wetu kwao ni ishara ya uwepo wao maana walituachia upendo"