
ZABURI 46
1 Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu,Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.

Mungu kwetu ndiyo kimbilio katika kila shida mkimbilie yeye

atakupa msaada ambao hujawahi pata mahali popote.

simama imara katika imani yako.

Omba kwa bidii.

Jitie nguvu kuwa unaweza kumuomba Mungu lolote naye atakutia nguvu ambayo hujawahi kuipata maishani mwako.

Ni yeye alikuumba.

Anajua idadi ya siku zako hapa duniani.

Anajua mahitaji yako yote

Anajua kuingia kwako na kutoka kwako.

Mkimbilie yeye.

Atakutia nguvu.

Atakupa msaada.

Mateso yatakoma.
TUOMBE:
Baba wa mbinguni asante kwa siku mpya ya leo,asante kwa kutuamsha salama tukiwa wazima na afya njema,karibu majumbani mwetu Baba,makazini mwetu,kwenye mashamba yetu,kwenye biashara zetu,kwenye ndoa zetu,kwenye uchumba,kwenye masomo,mawazoni mwetu,linda mifugo yetu Baba mwema.
Ponya wagonjwa Baba kwa namna ya pekee tunamkumbuka Mondray mkono wako ukamguse umponye awe mzima mwili na roho.
Farijiwafiwa,tunawaombea marehemu wote wapumzike kwa amani,waongoze wasafiri nchi kavu,majini na angani wafike salama,bariki vijana wetu wote kidato cha sita wanaoendelea na mitihani wakumbushe yote Baba mwema,wasaidie wenye mashaka na changamoto mbalimbali wakumbatie Baba waondoe mashaka wape nguvu mpya.
Tuimarishe tukupende,tukuheshimu,tukutegemee,tukutwishe fadhaa zetu ni wewe peke yako ambaye una jibu la maswali yetu yote.
Asante Baba kwakuwa utatenda sawa na mapenzi yako,tunaomba yote katika jina la Yesu Mpatanishi na mwokozi wetu Amen
NAWATAKIA SIKU NJEMA
MBARIKIWE SANA