NUKUU YA LEO
Football is a simple game. Twenty-two men chase a ball for 90 minutes and at the end, the Germans always win.
Soka ni mchezo rahisi. Wanaume ishirini na mbili wanakimbiza mpira kwa dakika tisini na mwisho wajerumani watashinda daima.
Haya maneno yaliwahi kutamkwa na Mwanasoka na mchambuzi wa soka wa kiingereza Gary Wiston Lineker aliezaliwa mjini Leiceter Uingereza . G.W. lineker alizaliwa 30/11/1960.
Gary Lineker amecheza jumla ya michezo 567 na kufunga magoli 330.
Gary amechezea klabu za mpira 5, Leiceter city, Everton, Barcelona, Tottenham na Nagoya Grampus Eight na Timu ya Taifa ya England.
Garry alisema maneno hayo mwaka 1990 walipotolewa sem-final kwa penalti na ujerumani magharibi baada ya kumalizika dakik 90 wakiwa 1-1.
Garry ndio mchezaje wa kiingereza tuu ambaye amechukua kiatu cha dhahabu kombe la dunia( alikuchukua golden boot Fainali za mwaka 1986).
Lakini vile vile ndio mcheza wa kiingereza alieweza kuchukua kiatu cha mfungaji bora kwa timu 3 tofauti za Uingereza..yaani leiceter city, everton na Tottenham Hotspurs
Gary hakuwa kupewa kadi hata moja ya njano wala nyekundu katika maisha yake ya soka.. na kupitia hilo mwaka 1990 FIFA walimzawadia tuzo ya FFPA yaani Fifa Fair Play Award.
Ni mshabuliaji wa kihistoria katka taifa la uingereza na atabaki kuwa moja wa washambuliaji wazuri wa kiingereza.
[emoji460][emoji460][emoji460][emoji460][emoji460][emoji460][emoji460][emoji460][emoji460][emoji460][emoji460][emoji460][emoji460][emoji460][emoji460][emoji460][emoji460][emoji460][emoji460][emoji460][emoji460][emoji460]
Habari za jioni.