Werrason
JF-Expert Member
- Nov 5, 2014
- 13,223
- 39,924
Nilimuomba Mungu anipe nguvu nae akanipa magumu nijifunze kuwa imara.
Nilimuomba Mungu anipe Hekima na Busara nae akanipa matatizo ya kutatua.
Nilimuomba Mungu Nuru na mwangaza nae akanipitisha katika kiza kinene.
Nilimuomba Mungu anipe ujasiri nae akanipitisha sehemu za hatari niweze kujiokoa.
Nilimuomba Mungu anijaalie moyo wa subira nae ananipitisha katika nyakati ambazo suluhu pekee ni kusubiri.Nilimuomba Mungu anijaalie upendo nae akanipa watu wenye matatizo niwasaidie.
Nilimuomba Mungu furaha nae akanipa nyakati za kulia ili furaha ikija niithamini.
Nilimuomba Mungu anipendelee nae akanipa nafasi mbali mbali.
Nilimuomba Mungu kila kitu ambacho kingefanya nifurahie maisha badala yake akanipa maisha ili nifurahie kila kitu.
Hajanipatia vyote nilivyo taka bali amenipatia kila ninachohitaji.
Kila nyakati katika maisha yetu zina maana japo kuna wakati zinaumiza lakini Mungu anajua kwa nini anakupitisha hapo...huwezi kuwa bora kama hujapitia nyakati mbali mbali kwenye maisha...kadri unavyovuka ndivyo unazidi kuwa bora!
Oh Praise to Lord.