Makapuku Forum

Dawa yake baada ya kuumwa nae ni nini?
Wakati ule kijijini Kolomije ukiumwa na nge walikuwa wanaweka maji ya moto wanakukanda nayo halafu wanaweka tumbaku iliyosagwa (ugoro) mahali ulipoumwa. Sijui kama hii ilikuwa inasaidia cho chote kwa sababu maumivu ndiyo yalikuwa kama yanazidi. Maji ya moto nadhani ndiyo unapanua mishipa ya damu ili sumu isafiri kwa urahisi zaidi lakini ndiyo tiba za jadi hizo. Solace yangu ilikuwa ni katika ufahamu kwamba siwezi kufa kwa kuumwa na nge japo kuna jamii moja ya nge huko Atacama desert ikikutandika unaweza ku-RIP. Maumivu ni makali sana na utake usitake machozi yatakutoka tu hasa ukitandikwa na nge jike aisee ni shida. Na kesho yake ukikosea ukagusa maji ya baridi ngoma inaanza upya...
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…