Makapuku Forum

Ndege na Boti nimepanda no problem.....ila majengo marefu nitaota sakafu/floor imejengwa kwa mbao nyembamba au zilizooza then zinaanza kuvunjika usiombe kukutwa na bwana pepsi
 
Amen Mama Mchungaji
 
Aisee. Nitafanya hivyo. Hali hii imenifanya niwe msafi sana ili mende wasiweke makazi. Watu wananisifia kwa usafi uliopindukia kimo kumbe hawajui sababu yake. Uzuri hali hii haijitokezi mara kwa mara. Naweza kumaliza miezi sita hata mwaka halafu siku moja nikiona mende tu nightmare zinakuja.

Asante sana mtumishi. Halafu eti wanasema huku Makapuku hakuna lolote la maana!
 
Asante kushukuru,amini utashinda,USIOGOPE,HUKU MAKAPUKU BWANA MIMI NAJIFUNZA MENGI,NAJISIKIA VIZURI KUWA HAPA MUNGU AWABARIKI WALIOWAZA HILI
 
Nyagei, wewe huna phobia yo yote?
Ila kuna siku nilikuwa site huko wilayani Bahi mida ya usiku nilikuwa niko na mrembo wa kigogo jirani nasi kulikuwa na mti, so ili kuweza kumlaghai yule manzi nilipitisha mkono kwa mabega yake ili awe close nami suddenly nilihisi kuchomwa na kitu ila nilipotezea nikidhani ni sungusungu mdudu kumbe ni nge, nilishtuka maumivu yalipozidi na mkono kuanza kuishiwa nguvu, yule manzi nilimuacha na kurejea nilipofikia. Nilijichanja kidogo na kukamua sumu ila sikulala usiku ule na asubuhi ndio mkono hauna nguvu kabisa.

After 20hrs nikapona kabisa
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…