Makapuku Forum

Makapuku Forum

6a2546b09972359f8a431b584773a6c1.jpg
67105df82a86bb8c497f7769b1d5665b.jpg
Walikuwa ni akina nani?
 
Vijijini huko Kolomije nyoka jambo la kawaida sana na nimeshawakanyaga mno japo nina bahati hawajawahi kuning'ata. Hata hivyo nina urafiki wa ajabu na nge na nilikuwa sipitishi mwezi bila kung'atwa. Muziki wake nao si wa mchezo hasa akikung'ata sawasawa.

Naenda kuanza form one boarding naweka tu sweta mgongoni akanitandika. Aisee safari ya masaa manane kwenye basi nilikwenda naugulia maumivu...
Aisee ilikuwa safari ya maumivu hiyo
 
Come on Mukongoman! Una batophobia? Ndege huwa unapanda na huogopi? Ulianza anzaje kuogopa haya majengo marefu?

Ila hizi phobia zingine hizi hata sijui zinaanzaje. Mimi siku hizi nikiona mende chumbani silali aisee mpaka nimtafute nimuue. Nikilala bila kumuua basi nitaota limende likuuuubwa linaninyemelea sasa hata kulikimbia siwezi. Hapo mwanaume ni kutoka jasho balaa. Ajabu wadudu wengine na hata nyoka sina tatizo nao kabisa. Huwa nashangaa sana kwa sababu nimekulia kijijini na mende kibao and it was no big deal.
Nimecheka sana
 
Hapo sasa. Basi tusiwalalamikie wazungu kwa kupotosha historia yetu wakati sisi wenyewe wala hatujui tuanzie wapi.

Hapa maktabani kwangu nina vitabu vya Mashujaa wa Tanzania, Historia ya Wasukuma na Mila na Desturi za Wachaga lakini vyote vimeandikwa na wazungu kabla ya uhuru. Naweza kuwa na-scan na kuviweka pole pole kufuatia topic. Havina copyrights.
Ruksa kutushirikisha
 
KUMTEGEMEA MUNGU KUNA FAIDA

ISAYA 40

29 Huwapa nguvu wazimiao ,humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo

Pale unapochoka fikra unapowaza sana unapokata tamaa ndipo Mungu anapokupa nguvu na kinga za kila shambulizi pia kukuvusha juu ya hali uliyo nayo ,hivyo pambana na hali hiyo kwani Bwana anatamalaki na kukupa utulivu na ushindi ili kumshinda adui anapotaka kukudhuru

Tumuombe Mungu atusaidie tumkabidhi Mungu njia zetu zote naye hatatuacha

TUOMBE

MUNGU BABA MWENYEZI tunakushukuru sana kwa ulinzi wako na yote unayotutendea,Mungu,umetutoa mbali tunakushukuru sana.

Ponya wagonjwa,fariji wafiwa,fariji wajane na yatima,tembea nasi Baba nyoosha mapito yetu,peke yetu hatuwezi

Tunajikabidhi miili na roho zetu tukinge na hatari zote za mwili na roho.

Roho Mtakatifu Mfariji wetu tufundishe ,tuongoze,tuonyeshe njia sahihi ya kuishi maisha ya kumpendeza Mungu

Asante kwa kila linakotokea maishani mwetu

Tunaomba yote kwa jina la Yesu mpatanishi na mwokozi wetu .

Amen


Muwe na siku njema,wiki njema,mwezi mwema.....MBARIKIWE
Amen

Ubarikiwe Mama mchuchu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom