Makapuku Forum

Makapuku Forum

944393e062f18689271bd3700ebe97f9.jpg
 
Waafrika dini tumeletewa tu na meli lakini tunajifanya kumjua Mingu kuwazidi Waarabu na Wazungu
Wazungu wenyewe hawana habari na makanisa wanaona km kupoteza time tu bora kupiga kazi ila sisi haswa Walokole masaa 15 tupo church tunapiga mayowe
NB:
Sijamlenga mtu
Kila mtu na imani yake
.....
Halaf tulivyo wajinga unaambiwa njoo upande mbegu,toa mfano lak moja kuubariki unabii na utaona muujiza wa Mungu, utanunua gari mwaka huu,utajenga nyumba bla blaaa kibao na tunaamini, ila ajabu yake miaka itaenda weee hata kiwanja huna, unajiuliza hivi ni wapi Mungu alisema uombe tu bila kufanya kazi,fanya kazi muombe Mungu atabariki kazi za mikono yako na kukuzidishia
 
NUKUU YA LEO

In counrty caring justice and equality , hosts must be an instrument to protect rights of the majority and never allow that instrument of few caring to themselves and forget the interest of the majority.

"Katika nchi inayojali haki na usawa, majeshi hayana budi yawe ni chombo cha kulinda haki na maslahi ya walio wengi. Na kamwe hayaruhusiwi kuwa ni chombo cha wachache wenye kujali nafsi zao na kusahau maslahi ya walio wengi"


Maneno haya yalipatwa kutamkwa na Aliyekuwa Waziri mkuu wa 2 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bw. Edward Moringe Sokoine aliyezaliwa 01/08/1938 na kufariki tare 12/4/1984

Sokoine alifariki akiwa na miaka 45, kwa ajali ya gari mkoani morogoro katika eneo la Dakawa.

Sokoine alikiwa ni kiongozi shupavu, mwenye kujali haki, mwenye kujali maslahi ya wengi na mwenye kupenda watu..

Ukisoma vizuri hayo maneno ya Sokoine na ukiangalia kinachoendelea nchi sasa hivi utagundua kitu..utaona ukweli wa maneno ya Sokoine..

Tanzania iko mahali pabaya mno japo tunapeana moyo kuwa nchi ina amani, nchi ina haki , nchi ina usawa...its not true, we are lying ourselves.

Majeshi na vyombo vya usalama kwa ujumla vinapaswa kulinda masilahi ya wengi.

Lee/Bitoz niwekeeni picha wakuu

Transcend.
Thanks
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom