Makapuku Forum

Makapuku Forum

TANZANIA PEKEE NDIO KUNA ABIRIA AINA SABA.( 7 ).
_________________________________________________

1.Yupo abiria anayemtukana Konda ...lakini kumbe nauli ameacha nyumbani.

2.yupo aliyepitiwa na usingizi...huyu anapokurupuka hajielewi....utasikia shushaaaa bwege wee!..........anashushwa kambi ya jeshi!

3 .Yupo mwingine msumbufu na mvivu halafu ana lawama....huyu anakaa mbali na mlango halafu usishangae akaomba msaada kwenye round about.

4.Yupo aliye makini na Safari..yeye anakwenda na Muda, huyu ukimpitisha kituo gari itajikuta Sumatra Head office.

5.Halafu Yule wa siti ya nyuma yeye hukoroma na tiketi mkononi ...huyu haigwi. ...maana mara nyingi hushukia kituo cha mwisho hata kama ni Makaburini.

6.Yupo asiyeelewa jina la kituo..amekariri panauzwa Mananasi Mengi, sasa akikuta Wameweka Matikiti basi ataenda na gari mpaka gereji.

7.Wa mwisho ni Staff...halipi nauli...huyu yeye hana safari maalum, ni kama anafanya utalii wa ndani, huyu hashuki hata kama ni trip ya Mkaa.

kapuku katika ubora wake
Amenishangaza sana huyo staff huku hajaajiriwa sio kondakta sio utingo sio mbeba magunia ya mkaa ..hashuki kwenye gari sijui kazi zake anafanya saa ngapi...duniani kuna mambo!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom