Makapuku Forum

Madenge bwana. Inawezekana kweli sijaelewa. Nadhani pia hujaelewa mantiki ya comment yangu. Tukiacha ushabiki wa hizi siasa uchwara na ushabiki usio na tija ndiyo tutaweza kufanya jambo la maana.

Hata hao wanaomuita nadhani wanajua kuwa Manji alishajiengua na hayo makampuni. Ni mbinu ya kawaida kisheria kwa corrupt businessmen; na kujiengua huko kunaweza kuwa kwenye makaratasi tu na nyuma ya pazia bado wakawa wanashikilia madaraka bado. Kwa nini tunaona shida yeye kuitwa na kwenda kusikiliza wanachomuitia? Inakuwa kama vile tayari ameshahukumiwa. Vipi kama wanataka habari tu ambazo wanaamini anazo? Kwa nini sisi "wenye ufahamu" na "wasomi" tunatumia nguvu nyingi kiasi hiki kumtetea? Kwa vile ni bilionea anayeweza kwenda polisi na mawakili wanane wakiwemo wazungu? Ni kwa vile ni kiongozi wa kilabu ya soka? Ni kwa vile ana asili ya nje? Yeye kuitwa polisi na mamlaka hizi ndiyo sheria zimevunjwa? Au kuna vitu vingine ambavyo mnavijua ambavyo wengine hatuvijui? Ningeitwa kapuku kama mimi ni kweli ungekuwa hapa ukipiga makelele namna hii na kulaumu mfumo mzima? Come on man!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…