Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mimi leo Valentine hii jamani ni kudekeshwa tu na bebi wangu jamani. Msukuma haki ya nani mpaka mniroge!
5e6535df99af4976f6b21016f61fe016.jpg
Kwa makapuku wote. Muwe na sikukuu njema ya wapendanao. Hata wewe unayejiona kuwa hupendwi (kama mimi nisivyopendwa na Shunie), jua kuwa yule mwanamke shujaa aliyekuleta hapa duniani anakupenda sana. Hata kama ameshatangulia kwa Muumba wetu, ukumbuke na kuuenzi upendo wake siku ya leo. Na zaidi ya yote, Mungu Aliyekuumba ana upendo wa ajabu kwako.
3db939deb846bc324b23a27e51deb73c.jpg
Hata uwe umepondeka namna gani, hata uwe unapita katika jangwa lenye ukame wa kutisha namna gani katika maisha yako, maadam ungali ukipumua, matumaini yangalipo and it isn't over. Jipende, wapende wengine, na endelea kumtegemea Mungu. Jangwa hatimaye litakuwa na mwisho na Kanaan yako itaonekana na siku moja utaifikia. Te amo Omnes (I love you all!)
5313aa3c2c55aa50d90075a1b7da165b.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom