Nyinyi mnaonisikiliza nawaambieni wapendeni adui zenu watendeeni mema wale wanaowachukieni watakieni baraka wale wanaowalaani na waombeeni wale wanaowatendea mabaya
Mtu akikupiga shavu la 1 mgeuzie pia la pili yeyote atakaekuomba mpe na mtu akikunyang'anya mali yako usimtake akurudishie jinsi mnavyotaka watu wawatendee nyinyi watendeeni wao hivyo hivyo na ikiwa mnawapenda tu wale wanaowapenda nyinyi mtapata tuzo gani? Kwa maana hata wenye dhambi huwapenda wale wanaowapenda wao tena mkiwatendea mema wale tu wanaowatendea mema mtapata tuzo gani? Kwa kua hata wenye dhambi hufanya hayo pia na kama mkiwakopesha tu wale mnaodhani watawalipeni je mtapata tuzo gani ? Kwa kua hata wanye dhambi huwakopesha wenye dhambi wenzao ili warudishiwe kima kilekile
Ila nyinyi wapendeni adui zenu na kuwatendea mema kopesheni bila kutazamia kurudishiwa na tuzo lenu litakua kubwa nanyi mtakua watoto wa mungu alie juu kwa maana yeye ni mwema kwa wale wasio na shukrani na walio wabaya
Muwe na huruma kama baba yenu alivyo na huruma
Huu ni ujumbe wa jumapili kwa makapuku wote wa jf bila kuwasahau wakongwe luka 6/27-36
Mko poa lakini nyote humu makapuku wenzangu i hope mu wazima