Makapuku Forum

Makapuku Forum

1478863095474.png
 
1983 - Philip Lahm anazaliwa.

Beki wa kulia wa klabu ya Bayern Munich.

Ametwaa Kombe la Dunia mwaka 2014 akiwa nahodha wa Ujerumani.

Pia ametwaa ubingwa wa Ulaya mwaka 2013 akiwa na klabu yake ya Bayern.

Ni zao la akademi ya Bayern Munich na hajawahi kuhama klabu.

Mmoja kati ya wachezaji wachache wenye nidhamu ya hali ya juu kwani hajawahi kabisa kupewa kadi nyekundu licha ya kucheza kwenye idara ya Ulinzi.

Kwangu mimi huyu ni shujaa asiyeimbwa kwani amekuwa nyuma ya mafanikio ya klabu na timu yake ya taifa, hapewi sifa anazostahili. ( He is so underrated )
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom