Makapuku Forum

Makapuku Forum

1990 - Georginio Wijnaldum anazaliwa.

Kiungo wa zamani wa Fayernood, Newcastle ambaye kwasasa anakipiga Liverpool na timu ya taifa ya Uholanzi.

1988 - Kyle Naughton anazaliwa.

Beki wa kulia wa Swansea kutoka nchini Uingereza.

Pia aliwahi kukipiga Tottenham.

1983 - Philip Lahm anazaliwa.

Beki wa kulia wa klabu ya Bayern Munich.

Ametwaa Kombe la Dunia mwaka 2014 akiwa nahodha wa Ujerumani.

Pia ametwaa ubingwa wa Ulaya mwaka 2013 akiwa na klabu yake ya Bayern.

Ni zao la akademi ya Bayern Munich na hajawahi kuhama klabu.

Mmoja kati ya wachezaji wachache wenye nidhamu ya hali ya juu kwani hajawahi kabisa kupewa kadi nyekundu licha ya kucheza kwenye idara ya Ulinzi.

Kwangu mimi huyu ni shujaa asiyeimbwa kwani amekuwa nyuma ya mafanikio ya klabu na timu yake ya taifa, hapewi sifa anazostahili. ( He is so underrated )

1983 - Arouna Kone anazaliwa.

Straika wa zamani wa Wigan na timu ya taifa ya Ivory Coast ambaye kwasasa anakipiga Everton.

1977 - Maniche anazaliwa.

Kiungo wa zamani wa Porto, Chelsea, Benfica, Inter Milan, Atletico Madrid na timu ya taifa ya Ureno.

Alitwaa taji la ligi ya mabingwa ulaya mwaka 2004 akiwa na Porto ya Mourinho.
Naona leo siku ya Playerz tena.

HBD to all Playerz
 
1974 - Leonardo Dicaprio anazaliwa.

Ni msanii wa movie toka nchini Marekani, moja kati ya movie zake ni Titanic na Blood Diamond.
95ee02ddb328c1e06e59511ff5e254c7.jpg
37070e1d6a9bffe4f52f91b7f8b12f46.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom