Sasa hiyo unaizungumzia Dutch team ya World Cup 1998 pale Ufaransa, walifanya wonders sana, Timu ile iliundwa na wachezaji wengi toka Ajax Amsterdam kama vile Ronald Na Frank De boer, Van Der Sar.
Walifika Nusu wakatolewa kwa matuta, ila mechi dhidi ya Argentina, Denis Bergkamp alipiga goli la kideo sana.
Alipokea pasi ndefu ya juu toka nyuma, jinsi alivyoutuliza ule mpira na kumgeuza beki wa Argentina, Roberto Ayala ilikuwa ni burudani ya nguvu na kamwe haichoshi, kabla ya kufunga goli.
Pitia Youtube ujionee.