*S O M O LA A S U B U H I*
*J'TATU JULY-18/2016*








*_ELIYA ALIKATAA KUKATISHWA TAMAA_*

*Ikawa mara ya saba akasema ,Tazama , wingu linatoka katika bahari ,nalo ni dogo kama mkono wa mtu . Akanena ,Enenda umwambie Ahabu ,Tandika ,ushuke ,mvua iaikuzuie .* *-1WAFALME 18:44._*
________________________


*_Tunaletewa mafundisho muhimu kutokana na uzoefu wa Eliya. Alipokuwa mlimani Karmeli aliombea mvua , imani yake ilijaribiwa lakini alistahimili katika kufanya maombi yake yajulikane kwa Mungu. Aliomba kwa dhati mara sita na bado hapakuwa na ishara iliyoonesha kwamba ombi lake lilikuwa limekubalika, lakini huku imani yake ikiwa na nguvu alisisitiza ombi lake kwa kiti cha enzi xha neema. Kama angechoka na kukata tamaa mara ya sita , ombi lake lisingejibiwa .... Tunaye Mungu ambaye sikio lake halijafungwa ili lisisikie maombi yetu; Yeye anataka shauku zetu zote ziwe zimefungamanishwa pamoja na mapenzi yake na hapo ndipo atatubariki kwa uhakika kabisa; kwani hapo ndipo hatutajitwalia utukufu wakati baraka zinapokuwa zetu , bali tutatoa sifa zote kwa Mungu. Siyo mara zote ambapo Mungu hujibu maombi yetu tunapomuita kwa mara ya kwanza ; kwani akifanya hivi, tunaweza kulichukulia kirahisi tu kwamba tulikuwa na haki kupata baraka zote na upendeleo ambao alitupatia._*
.


*_Mtumishi alikuwa akimtazama Eliya alipokuwa akiomba.. Alipokuwa akichunguza moyo wake ,alionekana kupungua zaidi na zaidi, kulingana na alivyojitazama mwenyewe na jinsi alivyojiona machoni pa Mungu. Ilionekana kwake kwamba alikuwa sio kitu na kwamba Mungu alikuwa kila kitu : na pale alipofikia hatua ya kuikana nafsi ,huku akimng'ang'ania Mwokozi kama nguvu na haki yake pekee,jibu lilikuja._*


*_Hata mtu awe jasiri na mwenye mafanikio kiasi gani afanyapo kazi maalumu asipodumu kumtazama Mungu wakati mambo yanapotokea kujaribu imani yake , atapoteza ujasiri wake,baada yake kutiwa nguvu kufanya kazi ya Mungu ,atashindwa asipomtegemea kikamilifu Yeye aliye na uwezo wote._*
*U B A R I K I W E*
...................................................