Makapuku Forum

Makapuku Forum

Smothie, hii ndo nliitamani sana mana huwa naishiaga kuiona kwenye movies tu
Ulitumia natural yogurt, ndizi na nini?? Mi leo ningetengeneza sema sasa tatizo
1468071321531.jpg
 
SIKU MBILI ZILIZOPITA – SHAMBA
KAMA NI SURA YA HASIRA basi ilionekana wazi kwa Madam S alipokutana na vijana wake ndani ya nyumba yao ya siri huko Gezaulole. Kikao hiki kiliitishwa haraka sana baada ya tukio lisilotegemewa kutokea kutokea eneo la Darajani katika Barabara ya Nyerere, saa sita mchana kweupe.
Kamanda Amata alikuwa kajiinamia kama awazae jambo wakayti wengine wakijaribu kuchanganya akili kwa hili na lile juu ya hilo.
“Lakini mi nilisema kuwa mtu Yule asilindwe na askari wa kawaida kwani ana mbinu nyingi za kujiokoa,” Chiba akaeleza.
“Yeah ni kweli lakini kumbuka pia sisi si kazi yaetu kulinda watuhumiwa,” Madam akamjibu. Ukimya mwingine ukatawala.
“OK!” sauti ya Madam S ikawazindua vijana wale watano waliokuwa katika lindi la mawazo ya sintofahamu.
“Lazima tumsake na kumtie mkononi, mtu mmoja hawezi kutunyanyasa sisi tena wanataaluma wa kazi hii. Tutamsaka na kumleta tena hapa, Chiba jaribu kufuatili wapi anaweza kuwa ameelekea ili tuone la kufanya,” Madam akatoa amri na Chiba akaondoka eneo hilo kuelekea kati kachumba chake maalum.
“Usione niko kimya yaani huyu bwana ananiumiza kichwa, nikikumbuka jinsi nilivyompata kwa shida, we acha tu!” Kamanda Amata alimwambia Madam S huku akitoka eneo hilo.
“Najua lakini naamini tutampata tena,”
“Ndiyo tutampata lakini kwa jinsi ile ina maana huyu jamaa bado ana nguvu sana na hatujui kajipanga namna gani,”
“Unalosema ni kweli, kwani hata mbinu iliyotumika kutekwa kwake mbele ya mikono ya polisi haijawahi kutokea na wala hatukutegemea,” Madam alimweleza Amata huku wote wakitembea kwenye ujia mrefu ndani ya jengo hilo.
† † †
CHIBA alikuwa ametingwa kwenye mitambo yake, kompyuta kadhaa zilimzunguka na mashine nyingine mbalimbali. Ndani ya chumba hicho aliweza kuikusanya dunia yote na kuiweka ndani ya kioo kimoja cha kompyuta.
Msako wake aliuanzia palepale eneo la tukio, Banda la Ngozi, akijaribu kufuatilia uelekeo wa helkopta iliyombeba mtuhumiwa wao mara rtu baada ya kutekwa kukombolewa kutoka katika mikono ya polisi, ndani ya gari ya chuma alipofungwa minyororo miguuni na mikononi na kuacha askari sita wakiwa hawana maisha.
Chombo chake kilimuonesha uelekeo wa Kaskszini Mashsriki yaani maeneo ya Mbweni mpaka Bagamoyo, lakini alishangaa kila akifika eneo Fulani la Mbegeni ule mtambo ulikiuwa unashindwa kueleza uelekeo sahihi wa kile chombo, akajaribu na kujaribu lakini alishindwa. Akashusha pimzi ndefu na kujiegemeza kitini kabla ya kunyanyua simu na kumjulisha Madam S juu ya hilo. Ilichukua dakika moja tu mwanamama huyo kuwasili ndani ya chumba hicho maalum cha mawasiliano. Baada ya kuongea mawili matatu na Chiba walifikia azimio la kumsaka mtu huyo iwe angani au ardhini. Kikao kikaitishwa tena na wote wakakutana.
“Haya kama alivyotueleza Chiba, sasa hapa tunakwenda kimakundi, kundi moja na la kwanza litakuwa angani hili ni Scoba na Amata, kundi la pili Gina na Chiba mtakuwa ardhini mkifuatilia kwa chini na la tatu ni mimi (Madam S) na Jasmine tutakuwa katika uokoaji. Hivyo basi sasa tuingie kazini.
JESHI LA WANAMAJI KIGAMBONI
KAMANDA AMATA NA CHIBA waliwasili katika kambi hiyo majira ya saa kumi jioni wakiwa tayari kwa shughuli hiyo ngumu. Wakati huohuo Chiba na Gina walikuwa tayari katika gari wakielekea Tegeta mpaka Mbweni kuendeleza msako.
Baada ya Kamanda na Chiba kusaini kabrasha Fulani Fulani pale jeshini tayari kuchukua ndege ndogo inayoweza kutua na kuruka majini, walikabidhiwa kofia ngumu za kuvaa na kupewa maelekezo machache na rubani wa jeshi kisha wakaingia katika ndege hiyo ndogo yenye uwezo wa kubeba watu watatu tu. Wkaketi na kufunga mikanda, Scoba kama kawaida yake ndiye alikuwa rubani mkuu wa kuirusha ndege hiyo.
“Hivi wewe kuna kitu hujawahi kuendesha?” Amata akauliza kwa utani.
“Kipo,”
“Kipi?”
“Ungo”.
Wote wakaangua kicheko na wakati huo tayari injini ilikuwa ikizunguka na Scoba akiito ndege hiyo mahala pake kuelekea katikati ya bahari tayari kuruka na kuanza safari ya msako.
Dakika mbili baadae walianza kuliona jiji la Dar es salaam kutoka juu jinsi linavyopendeza. Muda wote walikuwa wakiwasiliana na Chiba na Gina waliokuwa wakisafiri kwa gari kuelekea upande huo. Walipofika eneo ambalo walihisi ndipo hasa wanapopataka, juu kabisa ya anaga la bagamoyo pande za Mbegani kuja Kaole walikuwa wakitumia darubini maalumu yenye nguvu kutazama chini kama wanaweza kuona chochote chenye maana kwao huku picha zile moja kwa moja zikirushwa mpaka kwenye kompyuta ya Chiba ambayo alikuwa nayo ndani ya gari hiyo iliyokuwa ikiendeshwa kwa kasi na mwanadada Gina.
“Mpaka sasa hatuoni chochote zaidi ya misitu na nyumba za wenyeji,” Kamanda alimwambia Chiba.
“Scoba Scoba, shusha ndege chain zaidi angalau futi elfu mbili tuone kama twaweza kugundua chochote,” Chiba akatoa maagizo na Scoba akateremsha ndege hiyo kama alivyoagizwa, wakaanza tena kutazama kwa kile chombo huku ndege hiyo ikizunguka huku na huko bila kutua chini.
“Hey! Amata, hebu cheki pale!” Scoba akamshtua Amata, naye akatazama kwa ile darubini.
“Shiit, kile ni kisiwa sivyo?” Amata akauliza.
“Hiki kisiwa nakijua, kulikuwa na kitu pale cheupe kinang’aa kama paa jipya lakini kimepotea na kuchukua rangi ya uoto uliopo,” Scoba aliongeza.
Kamanda Amata akamwonesha ishara ya kidole ya kwamba aizungushe ndege hiyo na kukizunguka kile kisiwa ikiwa ni pamoja na kuteremka chini zaidi.
“Scoba unaanza kuzeeka, lile ni pori tu!” Amata akamwambia Scoba huku akigeuza ile darubini upande mwingine wa Kaole. Bado ndege ilikuwa haijamaliza kuzunguka kile kisiwa, Scoba aliendelea kutazama kwa makini sana.
“Kwa hiyo tunafanyaje?” Scoba akauliza.
“Tucheki na upande ule kuleeeee,”
“Ok!” Scoba akajibu na kuiweka sawa ile ndege kisha akainyanyua juu ili kuendelea mbele.
† † †
MAHALI FULANI BAGAMOYO
Watu watatu walikuwa ndani ya chumba maalum wamejifungi wakiwa wametingwa kusoma kitu kikubwa kama saa lakini hiki hakikuwa na tarakimu yoyote isipokuwa kilikuwa na mistari duara kadhaa na mstari mmoja wa rangi ulikuwa unazunguka huku na kule.
Mlio wa kitu kama bip ukaanza kusikika ndani ya chumba kile, mlio huo ulianza kusikika kwa mbali sana lakini baadae ukawa na sauti kubwa.
“Vipi?” mmoja akauliza.
“Kuna kitu kama ndege hapa naiona inaelekea upande huu wetu,” akajibiwa. Yule bwana akasogea karibu na kile chombo na kuangalia.
“Mmmhh! Ni ndege hii hebu washa ile camera kubwa tuone,”
Nukta hiyo hiyo, kitu kama antenna kikaibuka kutoka katikati ya mapori na kusimama wima kati ya miti. Ndani ya chumba hicho waliweza kuona picha halisi ya ndege ile.
“Nani hawa?” mwingine akauliza huku akiwa katumbua macho.
“Sijui, hebu toa taarifa kwa mkuu wa kikosi,”
Yule kijana akatoka na kuelekea pembeni kisha akachukua simu na kukoroga tarakimu Fulani.
“Mkuu, kuna ndege tunaiona kwenye rada inaelekea upande huu, hatua gani tuchukue?” Yule kijana akaongea huku akitweta.
“Subiri nakuja hukohuko,” akajibiwa.
Sekunde kumi hazikupita mlango ukafunguliwa na mtu mmoja mwenye tambo kubwa la kimazoezi akaingia; moja kwa moja akaiendea ile meza na kutazama ile picha iliyopigwa ka kamera ya siri.
“Shiit!” akang’aka na kuwatazama wale vijana.
“Ilipue,” akawaamuru.
“Haiwezi kutuletea matatizo tukiilipua?” kijana mmoja akauliza.
“NImesema lipua tena haraka!”
Hakukuwa na lingine, missile equipment ikafunguliwa na kujitokeza juu kidogo ya ardhi lakini ndani ya msitu huo wa mikoko kisha ikafyatuliwa na moja kwa moja ikafuata ndege ile iliytokuwa na Amata na Scoba ndani.
† † †
“Amataaaaaa!” Scoba aliita baada ya kuona kwenye rada yake kuwa wamedunguliwa. Kitendo bila kuchelewa, Kamanda Amata akabonyeza kidubwasha kilicho chini ya kiti chake na vyuma vilivyoshika kiti hicho vikaachiana wakati huo tayari Scoba keshabinya kinobu kilichoandikwa neno ‘Evacuate’. Ile ndege ikafunguka juu na kiti cha Amata kikatolewa nje na kuicha ile ndege.
Hakuna alichokishuhudia zaidi ya mlipuko mkubwa angani na ile ndege kupasuka vipandevipande.
“Scoobbbaaaaa!!!!!” Kamanda Amata alipiga kelele akiwa hewani lakini hakumwona Scoba. Vyuma vilivyoruka kimojawapo kikampiga kichwani Amata akapoteza fahamu akiwa anaelea anagani huku parachute lililokuwa tayari limefunguka likimbeba na kumteremsha taratibu.
Scoba, mara tu baada ya Amata kutupwa nje alifyatua kiti chake lakini alichelewa nukta kadhaa, wakati kile kiti kikimrusha nje lile kombora likawa tayari limeshaipiga ile ndege eneo la kati kati, akajikuta ananasa kwenye vyuma vya ndege hiyo. Akajitahidi na kujifyatua lakini parachute lake liliharibika vibaya, akajitahidi kuliongoza ili adondokee nchi kavu akafanikiwa. Kutokana na kuchanika kwa parachute hilo alifika chini kama mzigo na kujipiga vibaya akatulia kimya bila fahamu.
Amata akiwa hana fahamu alidondokea baharini na kupigwa pigwa na mawimbi mpaka kando kidogo.
Jua la jioni lilikuwa tayari linang’aza sehemu hiyo na misafara ya ndege nayo ilikuwa ikirudi viotani.
† † †
Kioo cha kompyuta ya Chiba kikawa cheusi ghafla, hakuna chochote kilichoonekana.
“Vipi tena?” akajiuliza.
“Vipi kwani?” Gina akauliza.
“Nahisi hatari, maana sauti ya mwisho nilioisikia ni ya Scoba akimwita Amata, hebu weka gari pembeni kwanza,”
Gina akafanya hivyo, ile gari ikasimama kando mwa barabara katika eneo la Boko. Chiba akajaribu kucheza na kompyuta yake lakini hakuna alichoweza kuona zaidi ya ujumbe wa ‘Error’ uliokuwa ukijitokeza mara kwa mara, akaifunga ile kompyuta na kumgeukia Gina.
“Vipi?” Gina akauliza, lakini kutoka katika macho ya Chiba aliweza kuuona mshangao uliokosa mwelekeo.
“Huko hali si shwari, siwapati Amata na Scoba,” Chiba akajibu huku akijiweka sawa kitini na kuinua simu ndogo iliyofungwa ndani ya gari hiyo.
“Unataka kuniambia nini?” Gina akauliza huku mikono yake iliyokuwa imeshika usukani sasa ilianza kutetemeka na alionekana kubana meno yake ama akizuia kilio au akinyima uchungu nafasi ya kujiweka hadharani.
“Mawili, ama ndege ina hitilafu au wamedondoka,” Chiba akajibu na wakati huo tayari simu iko sikioni akimwitikia Madam S.
“Madam anasemaje?”
“Anasema tuwahi na Dkt. Jasmine anakuja na vitendea kazi vya kutosha kwa msaada wa haraka. Gina akaingiza gari barabarani na kutimua mbio kama kichaa kuelekea Bagamoyo. Alipoipita Bunju na kufika kijiji cha Mapinga aliiacha barabara ya Bagamoyo na kupinda kulia kuchukua nyingine ya vumbi kuelekea Mbegani.
“Shiiit!” Gina aliendelea kugugumia huku akikanyaga mafuta kama kichaa, mshale wa mwendo kasi ulikuwa katika namba 110 na vumbi lililoachwa nyuma halikuwa la kawaida. Baada ya mwendo wa takribani dakika arobaini na tano, Gina alisimamisha gari karibu na kijiji Fulani, Chiba akajitokeza juu ya gari na darubini yake na kuangalia kwa darubini katika uwanda wa nyasi fupifupi. Baada ya dakika kadhaa akaingia ndani, na kuchukua kifaa kingine kama simu lakini kilikuwa kikubwa zaidi, akakiwasha na kubonya vitu Fulani Fulani kisha akaanza kuangalia, rangi na michoro mbalimbali inayotokea katika kile kioo, baada ya sekunde kadhaa kukawa na kijitaa kinachowaka eneo Fulani la kioo cha kile kidubwasha.
“Gina, twende mbele zaidi,” akamwambia Gina, na ile gari ikaondolewa mahala pale mpaka kwenye njia panda ya kuwenda kwenye magofu ya Kaole na ile ya kwenda Bagamoyo mjini.
“Subiri!” Chiba alimwambia, kisha akamwambia aelekee kulia. Gina moja kwa moja akachukua barabara hiyo na kupita magofu ya Kaole akaendelea mbele mpaka alikokuta njia inaishia na kukutana na mkondo wa maji uliokatisha eneo hilo.
“Tunafanyaje?” akauliza.
“Tuache gari hapa, twende kwa miguu tufuate hii signal inawezekana ni Amata au Scoba, ila mmoja kati yao signal yake imepotea kabisa sijui tutampataje,” Chiba alijibu huku akiwa tayari kakanyaga ardhi ya eneo hilo akichukua hiki na kile ndani ya begi lake kabla hajaliweka mgongoni. Wakiwa bado wanaendele kutafuta hapa na pale katika viochaka hivyo, saa moja baadaye ndipo Jasmine alipoungana nao na kuweka nguvu pamoja jioni hiyo kufanya mtafuto huo mgumu.
† † †
“Hatujapata mwili wa mtu yeyote kule majini!” kijana mmoja kati ya wale watatu waliokwenda kuchunguza yale mabaki ya ndege walifikisha taarifa hiyo kwa Inspekta Simbeye aliyekuwa ndani ya lile meli bovu.
“Isipokuwa tumepata hiki kiboksi cha kurekodi mwenendo wa ndege, taarifa ambazo tumezipata kutoka humu ni kuwa ndege hii ilipoteza mawasiliano angani kwa ghafla kwa kitu kama mlipuko. Baada ya uchunguzi kule chini ya maji, ile ndege imedunguliwa, na kombola lililodunguia ndege hiyo ni Sayyad 2,” kijana mwingine akaelelzea kwa ufasha zaidi.
“Sayyad 2?” Madam S akadakia kwa kuuliza.
“Ndiyo, Sayyad 2 ni kombola la kisasa kabisa kutoka Iran ambalo linatumika na nchi hiyo kwa ulinzi wa anga, lina uwezo wa kutungua ndege ya kila aina.” Akameza mate na kutulia.
“Unataka kunambia kuwa ndani ya nchi hii kuna watu wanamiliki silaha nzito za kivita zaidi ya jeshi, hii ni hatari, ni hatari sana,” Madam S alizungumza huku akionekana wazi kukosa utulivu wa mwili na roho kwa swala hilo.
‘Oh! Shit, atakuwa wapi Amata?’ Madam akajiuliza pa si na kupata jibu sahihi ndani mwake.
“Sawa naomba hiyo taarifa yote katika nakala laini tafadhali,” Mada aliomba huku akilielekea dirisha dogo na kutazama nje kwa nukta kadhaa kabla ya kugutuliwa na sauti ya kijana Yule akiwa tayari na taarifa ile mkononi mwake ikiwa ndani ya CD. Akaipokea na kuondoka katika ofisi ile ya ajabu. Akiwa ndani ya gari yake kwa mwendo wa taratibu kuelekea ofisi ndogo pale karibu na jingo la hazina alikuwa akiwaqza mengi sana mojawapo ni juu ya mkasa wa Scoba na Amata, hakujua ni nini kimempata Amata, akili yake ilikuwa ikisimama na kufanya kazi kwa tofauti ya nukta moja.
Aliingia ofisini na kujitupa kwenye kiti chake cha miguu mitano, akiitazama saa yake ya ukutani ikimwambia sasa ni saa nne usiku.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom