Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,076
- 463,978
Ni mke mmoja tu mpaka kifo kiwatenganishe...!
Kanisa Katoliki limetoa amri mpy iliyoidhinishwa na Papa kukazia msimamo wake kwamba Wakatoliki wanapaswa kuishi katika ndoa ya mke mmoja na mume mmoja maisha yao yote.
Waraka huo uliotolewa na Vatican siku ya Jumanne ukiwalenga Wakatoliki bilioni 1.4 unatia msisitizo upekee wa ndoa huku ukieleza waziwazi kwamba mahusiano mengine ya ngono nje ya ndoa hayatakiwi.
Waraka huo ulikosoa waziwazi desturi ya wake wengi hasa miongoni mwa jamii ya Wakatoliki barani Afrika na kusisitiza kwamba ndoa ni kati ya mume na mke mmoja tu.
Pia waraka huo ulikosowa utumadani wa mtu kuwa na wapenzi wengi ulionea hasa katika nchi za Ulaya na Marekani.
Waraka huo unaeleza, "Kila ndoa halisi ni umoja unaoundwa na watu wawili, ambao unahitaji uhusiano wa karibu na kamili kiasi kwamba haupaswi kuingiliwa na mtu mwingine," Waraka huo hauelezei chochote kuhusu talaka, ambayo haitambuliki katika Kanisa Katoliki kwa sababu inaamini kwamba ndoa ni ahadi ya kudumu kati ya mke na mume...!